Maambukizi ya UTI ni ya kawaida kabisa. Yanaweza yakatokea mahali popote ndani ya njia ya mkojo ambayo ni pamoja na figo, mirija ya mkojo, kibofu cha mkojo. Maambukizi mengi katika njia ya mkojo husababishwa na bakteria na huathiri kibofu cha mkojo pamoja na mrija wa mkojo.
Pale njia ya mkojo inapoathiriwa, inaweza kusababisha maumivu makali kila unapomaliza kukojoa. Unaweza kuwa unahisi kukojoa kila mara, hata baada ya kuwa umeshatoka chooni kukojoa. Mkojo wako unaweza kuonekana wenye rangi ya ukungu na wenye harufu isiyo ya kawaida pia.
Maambukizi ya UTI yanaweza kusababisha pia mkojo wenye damu. Lakini pale tatizo lako linapopata matibabu, basi damu damu kwenye mkojo inaweza ikatoweka kabisa.
NUKUU: Katika makala hii, tutajadili jinsi UTI inavyoweza kusababisha damu kwenye mkojo, ikiwa pamoja na dalili zingine, halafu utapata maelekezo ya matibabu kutoka katika James Herbal Clinic Au Herbal Shop.
Je, Dalili Za UTI Zinakuwaje?
Maambukizi ya UTI mara nyingi yanaweza yasisababishe dalili. Kama ukipatwa na dalili za maambukizi haya, basi yanaweza kuwa kama ifuatavyo:
- Maumivu makali baada ya kukojoa
- Kuhisi kama moto wakati wa kukojoa
- Kutoa mkojo kidogo
- Kushindwa kukojoa
- Kuhisi kukojoa mara kwa mara
- Kujihisi kukojoa hata kama umemaliza kukojoa
- Kuhisi maumivu maeneo ya tumbo la chini, au kwenye nyonga au kiunoni
- Kukojoa mkojo wenye harufu mbaya
- Kukojoa mkojo wenye rangi ya ukungu
- Kukojoa mkojo wenye damu(mwekundu, wenye rangi ya pink au kama coca cola)
Dalili hizi hujionyesha katika hatua za awali. Lakini kama maambukizi ya UTI yakiwa yameshaenea kwenye figo, basi unaweza pia kuhisi dalili hizi zifuatazo:
- Homa
- Kiuno kuuma
- Kuhisi kichefu chefu
- Kutapika
- Uchovu
Je, Nini Husababisha Kutokwa Na Damu Wakati Wa Maambukizi Ya UTI?
Unapokuwa na UTI, bakteria huathiri ukuta wa njia ya mkojo. Hali hii hupelekea kuwepo uvimbe na muwasho, na kusababisha chembe nyekundu za damu kuvuja na kuingia kwenye mkojo.
Kama kuna kiwango kidogo cha damu kwenye mkojo wako, haiwezi kuonekana kwa macho ya kawaida. Kuna njia inayotumika kuweza kuchunguza nayo ni darubini. Daktari anaweza kuona damu kwenye mkojo pale anapotumia kipimo cha darubini.
Je, Yaweza Kuwa UTI Au Kipindi Cha Hedhi?
Kama uko hedhini, unaweza ukashangaa kama mkojo wako wenye damu unasababishwa na UTI au damu ya hedhi.
Pamoja na kutokwa na mkojo wenye damu, UTI na vipindi vya hedhi vinachangia dalili kama vile;
- Maumivu ya kiuno
- Maumivu ya nyonga au tumbo la chini
- Kuhisi uchovu(hasa pale UTI inapokuwa sugu)
Lakini kama kuna damu nyingi itakayopelekea kubadiri hata rangi ya mkojo, basi mkojo wako utaonekana kuwa mwekundu au kahawia kama Coca Cola.
Ili kubaini ni kitu gani kinachokusumbua, basi tafakari dalili zote ulizo nazo. Unaelekea kupata hedhi ikiwa kama;
- Tumbo linaunguruma au uzito wa mwili kuongezeka
- Matiti yanauma
- Kichwa kinagonga
- Unakosa usingizi
- Una wasiwasi au mashaka
- Una mabadiriko kwenye hisia za mapenzi au hamu ya tendo la ndoa
- Una matatizo ya ngozi
- Una hamu na vyakula mbalimbali
NUKUU: Dalili hizi haziambatani na dalili za maambukizi ya UTI. Ukijumlisha, kama uko kwenye kipindi cha hedhi, hutaona damu ya hedhi tu pale unapokojoa. Bali pia utaona matone ya damu meusi mara kwa mara yakikusanyikana kwenye chupi yako yakiwa na damu ya hedhi.
Asanteni sana mnaosoma makala, naomba niishie hapa. Je, unahitaji huduma? Tupigie kwa namba hizi: 0752 389 252 au 0712 181 626.
Arusha Mbauda
Karibuni sana.