Takribani asilimia 5%-10% ya ugumba kwa wanawake hutokana na uvimbe wa fibroid kwenye kizazi. Ukubwa wa uvimbe pamoja na eneo ulipojikita inaonyesha kabisa kuwa huathiri uwezo wa mwanamke kupata ujauzito. Kwa mfano uvimbe wa fibroid unaokuwa ndani ya uwazi wa mfuko wa kizazi(submucosal) au unaweza kuwa mkubwa sana(tuchukulie sentimita 6) au uvimbe unaokuwa ndani ya ukuta wa mfuko wa kizazi(intramural).
Wanawake wengi wenye uvimbe wa fibroid sio kwamba wanaweza kukosa uwezo wa kupata ujauzito. Wanawake wenye uvimbe huu ikiwa pamoja na wenzi wao wanapaswa kutathiminiwa ili kuweza kugundua matatizo mengine wakiwa na uwezo wa kupata ujauzito kabla uvimbe haujatibiwa. Daktari wa mambo ya uzazi anaweza kusaidia kutathimini kama uvimbe unaweza kuzuia ujauzito.
Je, Jinsi Gani Uvimbe Wa Fibroid Unaweza Kupunguza Uwezo Wa Mwanamke Kupata Ujauzito?
Kuna njia nyingi mbalimbali ambazo uvimbe unaweza kupunguza uwezo wa mimba kutunga kwenye kizazi, nazo ni kama ifuatavyo;
- Mirija ya uzazi inaweza kuziba kutokana na uvimbe wa fibroid
- Unaweza ukaharibu ukuta laini unaokuwa kwenye uwazi wa tumbo la uzazi
- Mabadiriko kwenye umbo la mlango wa kizazi kunaweza kuathiri idadi ya mbegu za mwanaume ambazo zinaweza kuingia ndani ya tumbo la uzazi.
- Mabadiriko katika umbo la mfuko au tumbo la uzazi yanaweza kuingiliana na mwendo wa mbegu za mwanaume au kiinitete.
- Mtiririko wa damu kwenye uwazi wa tumbo la uzazi unaweza ukaathiriwa. Hali hii inaweza kupunguza uwezo wa kiinitete kujishikiza kwenye ukuta wa tumbo la uzazi au kushindwa kuendelea kukua na kusababisha mimba kutoka.
Je, Nini Hutokea Kwenye Uvimbe Pindi Mwanamke Anapokuwa Na Ujauzito?
Uvimbe wa fibroid huonekana kwa asilimia 2%-12% kwa wanawake wajawazito, lakini sio uvimbe wote wa fibroid huwa mkubwa sana au kusababisha matatizo kwenye ujauzito. Uvimbe wa fibroid mara nyingi huongezeka kuwa mkubwa na kusababisha matatizo katika wiki 12 za mwanzo za ujauzito.
Je, Kinaweza Kikatokea Nini Kunapokuwa Na Uvimbe Wakati Wa Ujauzito?
Wasiwasi mkubwa katika ujauzito huwa ni kwamba, huenda uvimbe ukaongeza hatari ya mwanamke kujifungua kabla ya muda wake au mimba kutoka. Kwa maana hiyo basi, uvimbe wa fibroid unaweza ukafanya damu kuvuja ndani kusababisha maumivu makali. Huduma ya hospitali lazima itahitajika tu. Pia uvimbe huu unaweza kusababisha badiriko la eneo la mtoto kwenye tumbo la uzazi. Hali hii inaweza kuongeza hatari ya mimba kutoka, au kujifungua kwa njia ya upasuaji.
NUKUU: Jinsi tatizo hili linavyoweza kudhibitiwa inategemeana na hali yako ya pekee pamoja na mapendekezo ya daktari wako. Upasuaji hufanyika mara chache sana wakati wa ujauzito.
Kama mwanamke akibeba ujauzito baada ya kuondolewa uvimbe, anapaswa aonane na daktari wake ili kumsaidia mpaka mimba itakapokua na kufikia hatua ya kujifungua. Yawezekana akajifungua kwa njia ya upasuaji baadaye.
.
Je, Unahitaji Huduma? Tupigie kwa namba hizi: 0752389252 au 0712181626,
Arusha-Mbauda.
James Herbal Clinic pia tunatoa masomo ya afya na ushauri katika darasa letu lililopo katika mtandao wa telegram. Hivyo unaweza ukatuma namba yako ya WHATSSAP ili uweze kupata link yetu na uweze kuingia katika GROUP letu.
Karibuni sana!