Je, Ni Ukubwa Gani Wa Uvimbe Wa Fibroid Unaweza Kuwa Hatari Kwako?

Kwenye tumbo la uzazi lenye vivimbe vya fibroid kuna kuna vinyamanyama, ukuaji wake unaweza kusababisha afya kuwa mbaya baadaye. Makala hii leo napenda kuelezea vizuri juu ya vivimbe vya fibroid kwenye tumbo la uzazi.

Vivimbe vya fibroid huwa sio saratani. Unaweza Kwenda kupima na kadi yako ukaandikiwa kuwa una uvimbe unaitwa Leiomyomas na mara nyingi hutokea kwa mwanamke mwenye umri wa kuzaa.

Ukubwa wa vivimbe na idadi yake hutofautiana kwa kila mtu, na uvimbe wa fibroid unaweza kuwa mdogo kama mbegu au mkubwa kama donge kubwa linalokua nje ya mfuko wa uzazi na kuongeza uzito. Wanawake mara nyingi wanapata uvimbe huu bila kuwa na maarifa na wanakuja kutambua tu baada ya kufanyiwa vipimo.

Je, Aina Za Uvimbe Wa Fibroid Zinakuwaje?

Aina za fibroid hutambuliwa kulingana na sehemu uvimbe ulipo. Kama vivimbe vikionekana nje ya mfuko wa uzazi(uterus), vinaitwa Subserosal fibroids. Hata hivyo, vivimbe hivi huota hasa huota ndani ya ukuta wa msuli ambavyo huitwa Intramural fibroid au kama uvimbe umeota ndani ya eneo la uwazi la tumbo la uzazi ambao unaitwa Submucosal fibroid.

Je, Uvimbe Wa Fibroid Husababishwa Na Nini?

Hapa chini kuna baadhi ya dalili zinazoweza kukuonyesha kwamba una uvimbe kwenye tumbo lako la uzazi, nazo ni:

  • Kutokwa na damu nyingi mno wakati wa hedhi
  • Damu ya hedhi kutoka kwa mfululizo kwa muda mrefu bila kukoma
  • Kuhisi kukojoa mara kwa mara
  • Maumivu sehemu za nyonga
  • Kukosa choo
  • Maumivu mgongoni au miguuni
  • Kuhisi maumivu maeneo ya tumbo la chini

Je, Ni Muda Gani Uvimbe Huonekana Kuwa Umekuwa Mkubwa?

Vifuatavyo ni vitu vinavyoambatana na uvimbe wa fibroid vinavyohitaji matibabu kwa haraka Zaidi bila kuchelewa, hasa unapoona:

  • Kutokwa na damu nyingi sana wakati wa hedhi
  • Unapohisi maumivu makali tumboni
  • Tumbo linapokuwa kubwa
  • Unapotokwa na matone ya damu ukeni pale unapomaliza kukojoa.
  • Uke kutokwa na damu
  • Kupungukiwa na damu mwilini

Je, Ni Ukubwa Upi Wa Fibroid Unaweza Kuwa Hatari?

Uvimbe mkubwa, kuanzia sentimita 4 au Zaidi, ambao huota ndani ya msuli wa mfuko wa uzazi(uterus) unaweza kubadiri umbo lake na kuziba mirija ya uzazi. Kama uvimbe ukiota nje ya mfuko wa uzazi(uterus), unaweza kufikia ukuta wa kifua na kusababisha maumivu.

Uvimbe mkubwa wa fibroid pia husababisha hofu kutokwa na damu nyingi mfululizo. Pia husababisha madhara wakati wa ujzuito..

Je, Nini Madhara Ya Uvimbe Wa Fibroid Kwenye Ujauzito?

Ukuta wat umbo la uzazi hupokea kwa urahisi sana wakati homoni ya estrogen na progesterone inapoachiliwa. Homoni hizi pia huchochea uvimbe wa fibroid kwenye ukuta wa mfuko wa uzazi(uterus).

Ukuaji wa uvimbe wa fibroid kupita kiasi kunaweza kudumaza ukuaji kamili wa kiinitete na kusababisha mimba kuharibika. Wanawake wenye vivimbe vya fibroid wakati wa ujauziti wanaweza kuona tumbo la chini kuwa zito sana.

Uvimbe wa fibroid unaweza pia kusababisha mwanamke mjamzito kushindwa kujifungua vizuri, kwa mfano, kama uvimbe uko maeneo ya chini ya tumbo la uzazi, basi ujifunguaji wa kawaida utakuwa wa shida mno. Daktari atakushauri ujifungue kwa njia ya upasuaji.

Vivimbe vya fibroid vinaweza kukua wakati wa ujauzito, kwahiyo daktari anayepima afya na kujali magonjwa ya uzazi ya wanawake lazima awe na tahadhari juu ya vivimbe vya fibroid vinavyosababisha kuharibika kwa ujauzito.

Je, Suluhisho Lake Ni Nini?

James Herbal Clinic tunazo dawa za asili zenye uwezo mkubwa wa kuondoa vyanzo na madhara ya uvimbe. Je, Unahitaji huduma?  Basi wasiliana nasi kwa namba hizi: 0768 559 670 au 0712181626,

Unahitaji kupata masomo na ushauri zaidi, basi ungana nasi katika GROUP letu la WHATSAP, hivyo unaweza kutuma namba yako ya WHATSAP nasi tutakuunganisha.

Arusha-Mbauda.

Karibu sana!