Upungufu wa nguvu za kiume ni kutokuwa na uwezo wa kudindisha au kusimamisha uume kwa ajili ya kufanya tendo la ndoa. Uume unapokuwa unadindisha vizuri halafu siku zingine unaishiwa nguvu, hilo linaweza lisiwe tatizo sana. Lakini kama upungufu wa nguvu za kiume utakuwa tatizo endelevu, hata hivyo unaweza kusababisha msongo wa mawazo, na inaweza kuathiri ujasiri wako na kuchangia matatizo katika mahusiano ya ndoa.
NUKUU: Matatizo yanayojitokeza kwenye nguvu za kiume yanaweza pia kuwa ishara za tatizo la msingi la afya yako ambalo linahitaji matibabu pamoja na sababu hatarishi ya ugonjwa wa moyo.
Kama una tatizo la la kupungukiwa nguvu za kiume, nakushauri ufike hospitali ukapate ushauri kwa daktari hata kama unaaibika. Wakati mwingine kutibu tatizo la msingi inatosha kurejesha uwezo wa uume kudindisha. Hivyo basi, matibabu kwa njia ya mimea ya asili inatosha kabisa kuondoa tatizo hili.
Je, Dalili Zake Zinakuwaje?
Dalili za upungufu wa nguvu za uume zinaweza kuendeleza;
- Kupata shida ya kutokudindisha
- Tatizo la kutokusimamisha
- Kupungua kwa hamu au hisia ya tendo la ndoa
Je, Unapaswa Umuone Daktari Kipindi Gani?
Kufika hospitalini na kuonana na daktari ni jambo zuri sana unapoanza pale unapokuwa na matatizo ya kukosa nguvu za kiume. Muone daktari wako ikiwa kama:
- Una matatizo ya nguvu za kiume au matatizo ya uzazi kama vile kufika kileleni mapema au kuchelewa kufika kileleni.
- Una ugonjwa wa kisukari, moyo au tatizo jingine linalopelekea kukosa nguvu za kiume.
Je, Visababishi Vyake Vinakuwaje?
Hisia za tendo la ndoa kwa mwanaume ni mchakato tatanishi ambao hujumuisha ubongo, homoni au vichochezi, hisia, neva za fahamu, misuli pamoja na mishipa ya damu. Hali ya uume kushindwa kusimama inaweza kutokana na viungo hivyo vya mwili nilivyovitaja. Vile vile, msongo wa mawazo pamoja na afya ya ubongo inaweza kusababisha au kuharibu uume na kushindwa kusimama.
Wakati mwingine mchanganyiko wa matatizo ya mwili na ubongo husababisha kupungua kwa nguvu za kiume. Kwa mfano, tatizo kubwa la mwili ambalo hupunguza hamu ya tendo la ndoa linaweza kusababisha wasiwasi katika kutengeneza uwezo wa uume kusimama. Wasiwasi au mashaka yanapojitokeza yanaweza kupelekea kuishiwa kabisa nguvu za kiume.
Je, Ni Sababu Zipi Za Mwili Zinazopelekea Uume Kuishiwa Nguvu?
Katika hali nyingi, uume kuishiwa nguvu husababishwa na jambo la mwili. Visababishi vya kawaida ni pamoja na;
- Ugonjwa wa moyo
- Mishipa ya damu kuwa na damu iliyo ganda(atherosclerosis)
- Lehemu nyingi(high cholesterol)
- Shinikizo la juu la damu
- Kisukari
- Unene au kitambi
- Kuongezeka kwa kiwango cha insulin
- Uvutaji sigara
- Majeraha ndani ya uume
- Kukosa usingizi
- Kupungua kwa homoni ya testosterone
Je, Ni Sababu Zipi Za Ubongo Zinazopelekea Uume Kuishiwa Nguvu?
Ubongo hufanya kazi kubwa sana katika kuchochea mtiririko wa matukio ya mwili ambayo husababisha muundo, ukianza na hisia za mapenzi. Mambo mengi yanaweza kuingiliana na hisia za mapenzi na kusababisha hali mbaya kabisa ya uume kuishiwa nguvu. Mambo haya ni pamoja na;
- Wasiwasi
- Huzuni au matatizo mengine ya akili
- Matatizo ya mahusiano ya ndoa kutokana na msongo wa mawazo, kutokuwa na mawasiliano, nk.
Je, Madhara Yake Yanakuwaje?
Madhara yatokanayo na upungufu wa nguvu za kiume ni pamoja na:
- Kutomridhisha mwanamke wakati wa tendo la ndoa
- Msongo wa mawazo au wasiwasi
- Kuwa na aibu
- Matatizo ya mahusiano
- Kutokumpatia mimba au ujauzito mke wako
Je, unahitaji huduma? Tupigie kwa namba hizi: 0752389252 au 0712181626.
Arusha-Mbauda
Karibuni sana!