JE, NINI DALILI ZA KUKARIBIA KUKOMA HEDHI?

Hali ya kukaribia kukoma hedhi huonekana katika dalili zake, nayo huja ili kuomuonyeshea muhusika kuwa sasa uwezo wa kuzaa umefikia mwisho.

Wanawake huanza kukoma hedhi katika umri tofautitofauti. Unaweza ukaona dalili zinazoelekeza kuwa unafikia kukoma hedhi, kama vile vipindi vya hedhi kubadirika badirika, wakati mwingine unapofikisha umri wa miaka 40. Lakini wanawake wengine huanza kuona dalili hizi wakiwa bado na umri wa miaka 30 na kuendelea.

Tokeo la picha la image of women with 30 years old

NUKUU: Kiwango cha homoni ya estrogen ambayo ndio homoni kuu ya mwanamke, hupanda na kushuka mwilini mwake hasa wakati wa kufikia ukomo wa hedhi. Mzunguko wa hedhi unaweza kuwa mrefu au mfupi, na unaweza kuanza kuwa na mzunguko wa hedhi ambapo vifuko vya mayai havitoi mayai. Unaweza ukapatwa na hali ya kukoma kwa hedhi kama  dalili, kwa mfano;

 

 

  • Kutokwa na jasho jingi mida ya usiku

 

  • Kukosa usingizi

 

 

  • Uke kuwa mkavu

 

 

Unapopitisha miezi 12 bila kuona hedhi, basi hapo utakuwa umeshafikia ukomo wa hedhi, na zile dalili za kuonyesha kuwa unakaribia kufika mwisho wa hedhi zitakuwa zimeisha.

 

 

 

Je, Dalili Zake Zinakuwaje?

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Kupitia mabadiriko ya ukomo wa hedhi, baadhi yanaweza yakajulikana mwilini na mengine yasijulikane. Unaweza ukapatwa na mabadiriko kama yafuatayo:

 

 

 

 

 

  1. Vipindi Vya Hedhi Kubadirikabadirika

 

 

 

 

 

Kwakuwa mpevuko wa yai huwa hautabiriki, basi urefu wa muda katika vipindi unaweza kuwa mrefu au mfupi, na damu inaweza ikatoka nyepesi au nzito, na unaweza ukaruka vipindi vingine usivione

 

Tokeo la picha la image of women with irregular periods

Endapo kama utakuwa na badiriko endelevu la siku 7 au zaidi katika urefu wa mzunguko wako wa hedhi, basi utakuwa umefikia hatua ya kukoma hedhi mapema.

 

 

  1. Kutokwa Na Jasho Na Kukosa Usingizi Nyakati Za Usiku

 

 

Kutokwa na jasho usiku huwa ni jambo la kawaida wakati wa kufika ukomo wa hedhi. Kiwango, urefu pamoja na marudio hutaoutiana. Matatizo ya kukosa usingizi mara nyingi hutokana na kutokwa na jasho au mwili kuwa wa moto sana, lakini wakati mwingine usingizi huwa hautabiriki hata kama hakuna jasho.

 

  1. Mabadiriko Ya Hali Ya Moyo

 

 

 

Mabadiriko ya moyo(mood swings), kukasirika, msongo wa mawazo unaweza ukatokea pale mwanamke anakaribia hali ya ukomo wa hedhi. Chanzo cha dalili hizi inaweza kuwa ni kukosa usingizi hali ambayo inaambatana na kutokwa na jasho. Mabadiriko ya moyo yanaweza pia kusababishwa na mambo yasiyoambatana na mabadiriko ya homoni.

 

 

 

 

  1. Matatizo Ya Uke Pamoja Na Kibifu Cha Mkojo

 

 

Pale  viwango vya homoni ya estrogeni vinapopungua, tishu za uke zinaweza kupoteza unyevunyevu wake na kushindwa kutanuka, na kupelekea muhusika kuhisi maumivu makali wakati wa kufanya tendo la ndoa. Homoni kidogo ya estrogen pia inaweza ikaondoka na kusababisha maambukizi kwenye uke au mkojo kuingia kwa urahisi tu.

 

  1. Kupungua Uwezo Wa Kupata Ujauzito

 

 

 

Pale upevushaji wa mayai unapokuwa wa kubadirika badirika, basi uwezo wa kupata ujazuto mwanamke hupungua. Hata hivyo, kadiri unavyozidi kupata vipindi vya hedhi, inaonyesha ujauzito unaweza ukapatikana kwa urahisi. Ikiwa kama unataka kujihadhali na hali ya kubeba ujauzito, basi unaweza ukatumia uzazi wa mpango kwa njia mbadala mpaka pale utakapoona hupati hedhi kwa muda wa miezi 12.

 

 

  1. Mabadiriko Katika Tendo La Ndoa

 

 

Wakati hali ya kukoma hedhi inapokaribia, hisia na hamu ya tendo la ndoa kwa mwanamke hubadirika. Lakini kama ulikuwa na uwezo wa kufanya tendo la ndoa na kuridhika kabisa kabla ya kufikia ukomo wa hedhi, basi hali hiyo inaweza ikaendelea pale unapokaribia kukoma hedhi na kuendelea.

 

 

  1. Mifupa Kupoteza Uwezo Wake

 

 

 

Kutokana na hali ya kushuka kwa viwango vya homoni ya estrogen mwilini, muhusika huanza kupoteza kwa haraka sana uwezo wake wa mifupa kuwa imara  na hivyo kuongeza uhatari wa mifupa kuwa laini, ugonjwa ambao husababisha mifupa kuvunjika kwa urahisi.

 

 

  1. Kubadirika Kwa Viwango Vya Lehemu

 

 

 

Kupungua kwa viwango vya homoni ya estrogen kunaweza kupelekea kuwapo kwa mabadiriko mabaya kwenye viwango vya lehemu kwenye damu hali ambayo husababisha kuongezeka kwa uhatari mkubwa katika ugonjwa wa moyo. Muda huo, mafuta au lehemu ya kawaida hupungua kwa wanawake wengi wanapofikia umri mkubwa, hali ambayo pia huongeza uhatari wa magonjwa ya moyo.

 

 

 

Je, Nini Husababisha Kuwapo Kwa Hali Hii?

 

 

 

 

Unapofikia hatua ya kufikia mabadiriko ya ukomo wa hedhi, uzarishaji wa homoni ya estrogen pamoja na progesterone mwilini hupanda au kushuka. Mabadiriko mengi unayoyapata wakati wa kukaribia kukoma hedhi huwa ni matokeo ya kupungua kwa homoni ya estrogen. Napenda kila mwanamke alifahamu hilo.

 

 

 

Je, Kuna Matatizo  Gani Mwanamke Anapofikia Ukomo Wa Hedhi?

 

Kubadirika kwa vipindi vya hedhi huwa ndio viashiria vya kukaribia ukomo wa hedhi. Wakati mwingine hali hii inaweza kuwa ya kawaida na hakuna kitu kinachoweza kuhusihwa tena. Hata hivyo unaweza kumuonda daktari ikiwa kama;

 

 

 

  • Hedhi inapokaa kwa muda wa siku 7 kuliko kawaida

 

  • Kuja hedhi mara mbili ndani ya mwezi mmoja

 

 

  • Vipindi vya hedhi kutokea chini ya siku 21

 

 

  • Unatokwa na damu nyingi ya hedhi tena ya muda mrefu na kukufanya kubadiri pedi kila baada ya lisaa limoja

 

 

 

Tokeo la picha la image of woman with heavy bleeding

 

NUKUU: Dalili kama hizi zinaweza kuashiria kuwa kuna tatizo kwenye mfumo wako wa uzazi kiasi kwamba utahitaji vipimo na matibabu kwa haraka sana.

 

Je, unahitaji huduma? Kwa mawasiliano tupigie katika namba zifuatazo:

 

Arusha-Mbauda: 0752 389 252 au 0712 181 626

 

Njombe-Makambako: 0744 531 152 au 0716 158 086

 

Karibuni sana!

 

One thought on “JE, NINI DALILI ZA KUKARIBIA KUKOMA HEDHI?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *