Wanawake wengi hupatwa na hali ya kutokwa na damu ukeni mara moja au zaidi baada ya tendo la ndoa. Inaonekana karibia asilimia 63% ya wanawake wanaokaribia kufikia ukomo wa hedhi hupatwa na hali ya ukavu ukeni na kutokwa na damu ukeni au kutokwa na damu kidogo kidogo wakati wa tendo la ndoa.
NUKUU: Kwa nyongeza, zaidi ya asilimia 9% ya wanawake wanaopata hedhi hupatwa na hali ya kutokwa na damu baada ya tendo la ndoa.
Je, Nini Husababisha Kutokwa Na Damu Baada Ya Tendo La Ndoa?
Kutokwa na damu ukeni baada ya tendo la ndoa kitaalamu tunaita, “Postcoital bleeding.” Ni hali inayotokea kwa wanawake wenye umri wowote. Kwa wasichana wadogo ambao hawajafikia muda wa kukoma hedhi, chanzo cha kutokwa na damu baada ya kumaliza kushiriki tendo la ndoa, kwa kawaida huwa ni shingo au mlango wa kizazi.
Kwa wanawake ambao wamefikia kipindi cha kukoma hedhi, chanzo cha kutokwa na damu baada ya tendo la ndoa mara nyingi hutofautiana. Inaweza kutokana na:
- Shingo ya kizazi(cervix)
- Tumbo la uzazi(uterus)
- Mashavu ya uke
- Njia ya mkojo
NUKUU: Kwa upande wa visababishi, saratani ya shingo ya kizazi ndio chanzo kikubwa. Hali hii hasa huwa kwa wanawake wanaokaribia kufikia ukomo wa hedhi. Hata hivyo, hali ya kutokwa na damu ukeni baada ya tendo la ndoa husababishwa na matatizo ya kawaida kama vile;
1. Maambukizi
Baadhi ya maambukizi yanaweza kusababisha uvimbe wa tishu ukeni, ambayo inaweza kupelekea kutokwa na damu baada ya kushiriki tendo la ndoa. Maambukizi haya ni pamoja na;
- Maambukizi katika via vya uzazi, yaani PID kwa kifupi
- Maambukizi ya magonjwa ya zinaa
- Kuvimba kwa shingo au mlango wa kizazi
- Kuvimba kwa uke
2. Sehemu Ya Ndani Ya Uke Kuvimbe(Vaginal Atrophy)
Hali hii huwa ya kawaida kwa wanawake wale wanaokaribia ukomo wa hedhi au waliokoma hedhi kabisa na kwa wale ambao vifuko vyao vya mayai vilishaondolewa.
Kadiri unapozidi kuwa na umri mkubwa, hasa pale vipindi vyako vya hedhi vinapokoma, basi mwili wako huzarisha homoni kidogo sana ya estrogen. Estrogen ni homoni inayohusika kwa ajili ya kurekebisha mfumo wa uzazi.
Pale viwango vyako vya homoni ya estrogen vinapopungua, basi utaona vitu mbalimbali vikitokea ukeni. Mwili wako huzarisha ute kidogo sana unaolainisha uke, kwahiyo uke wako unaweza kuwa mkavu na hatimaye kuvimba.
NUKUU: Viwango kidogo vya homoni ya estrogen pia hupunguza uwezo wa uke kutanuka. Tishu za uke huwa dhaifu zaidi, hupata mtiririko kidogo wa damu, na huchanika na kuchubuka kwa urahisi. Hii inaweza kupelekea muhusika kujisikia mauimvu, na kutokwa damu wakati wa tendo la ndoa. Hivyo hushindwa kufurahia tendo la ndoa
3. Uke Kuwa Mkavu
Hali ya uke kuwa mkavu inaweza kupelekea kutokwa na damu. Uke kuwa mkavu unaweza kusababishwa na mambo mengi kama vile;
- Kunyonyesha mtoto
- Kujifungua
- Vifuko vya mayai kuondolewa
- Kupigwa mionzi wakati wa saratani
- Kufanya tendo la ndoa kabla hujapandisha hisia
- Kujipaka madawa ukeni
- Kemikali kwenye sabuni za kuoshea ukeni
- Matumizi ya madawa fulani kama vile vidonge vya pumu, na vya uzazi wa mpango
4. Vivimbe
Vivimbe wakati mwingine huonekana kwenye shingo ya kizazi au kwenye ukuta wa ndani wa tumbo la uzazi. Uvimbe hutuna na kuning’inia kama tunda. Ile hali ya uvimbe kuning’inia kunaweza kuharibu sehemu ya tishu inayozunguka eneo hilo na kusababisha kutokwa na damu kwenye mishipa midogo midogo.
5. Uke Kuchubuka
Tendo la ndoa, hasa tendo la ndoa la kulazimisha, linaweza kusababisha michubuko midogomidogo au michaniko ukeni. Hali hii hutokea kwa urahisi kutokana na muda wa hedhi kukoma, kunyonyesha au mambo mengine.
6. Saratani Ya Shingo Ya Kizazi
Kutokwa na damu ukeni baada ya tendo la ndoa, inaweza kuwa ni dalili ya saratani ya shingo ya kizazi. Saratani hii huwapata wanawake wenye umri zaidi ya miaka 50 au wale tayari wameshafikia ukomo wa hedhi.
NUKUU: Kama ukitokwa na damu ukeni baada ya tendo la ndoa na tayari umeshafikia umri wa hedhi kukoma, basi unapaswa ufike hospitali ili kupima kizazi chako uweze kuona kama kuna tatizo la saratani ya kizazi.
Je, Madhara Yake Yakoje?
Madhara makubwa kutokana na kutokwa na damu baada ya kushiriki tendo la ndoa si ya kawaida, isipokuwa sababu ni saratani hali ambayo haijatibiwa. Yafuatayo ni baadhi ya madhara yanayowezekana:
1. Kupungukiwa Na Damu
Damu itokayo nyingi au kwa muda mrefu inaweza kusababisha kupungukiwa na madini ya chuma mwilini katika matukio machache sana kwasababu chembe nyekundu za damu mwilini mwako hupungua kwa kupoteza damu. Hata hivyo hii sio kawaida ya kutokwa na damu baada ya tendo la ndoa.
Dalili za kupungukiwa na damu ni kama hizi zifuatazo:
- Kuhisi uchovu
- Mwili kuwa mdhaifu
- Kuhisi kizunguzungu
- Kichwa kugonga
- Ngozi kuwa kupauka na kuwa nyeupe
2. Maambukizi
Ikiwa kama una tatizo la uke kuwa mkavu, basi uko katika hatari ya kuendelea kuwa na maambukizi katika njia ya mkojo yaani UTI.
Je, Unawezaje Kubainisha Visababishi Vyake?
Kutokwa na damu baada ya kushiriki tendo la ndoa kwa kawaida husababishwa na hali ya ukavu ukeni, lakini kuna visababishi vingine zaidi. Kutokwa na damu baada ya kushiriki tendo la ndoa inaweza kuwa dalili ya maradhi mengi.
Daktari wako atapima kwanza ugonjwa wa saratani kwa kuchunguza uke wako na mlango wa uzazi, kwa kuchukua kipimo cha pap smear, na biopsy. Kama saratani ikionekana, basi utapelekwa kwa mtaalamu.
Baada ya saratani kuondolewa kama sababu ya kutokwa na damu baada ya kushiriki tendo la ndoa, basi hatua mbalimbali zinaweza kuchukuliwa ili kubaini visababishi:
- Transvaginal ultrasound
- Kipimo cha mkojo
- Kipimo cha damu
- Kupima uchafu unaotoka ukeni.
- Uchunguzi wa uke na mlango wa uzazi, ama kwa kuibua au kupitia kifaa cha kukuza kinachoitwa Colposcope.
Je, Unahitaji Kuondoa Tatizo La Kutokwa Na Damu Baada Ya Tendo La Ndoa?
James Herbal Clinic tuna dawa nzuri za asili zenye uwezo mkubwa kabisa wa kuondoa vyanzo vya kutokwa na damu baada ya tendo la ndoa, nazo ni PERFECT POWDER na CARD HERB.
Unahitaji huduma tupigie kupitia namba zetu hizi: 0752389252 au 0712181626.
Pia unahitaji kujiunga na darasa letu la WHATSAP unaweza kutuma namba yako ukaunganishwa na darasa letu ili uweze kupata darasa mfululizo.
Arusha-Mbauda
Karibuni sana
nimependa kazi yenu na maelekezo yenu asanteni sana
Barikiwa sana na karibu sana