Na ieleweke kuwa, mwanamke inafaa sana ukawa makini kujali mzunguko wako wa hedhi ikiwa kama unahitaji au unatafuta kubeba ujauzito. Zaidi ya yote ni hivi, ili uweze kuwa mjamzito, jambo la kwanza inapaswa mayai yako yawe yanapevuka kila mwezi.
NUKUU: Ni vyema kabisa kutambua kuwa, hedhi huwa ni dalili au ishara za kukuonyesha kwamba mayai yako yanapevuka kila mwezi. Lakini jambo la kushangaza ni kwamba, wanawake wengi hushindwa kujali jambo hili.
Kulingana na utaratibu wa Mungu kama jinsi alivyouumba mwili wa mwanamke, mfumo wa uzazi sharti kila mwezi upevushe mayai yake. Lakini kunaweza kuwepo na hali ambazo zinaweza kusababisha kutokupevushwa kwa mayai hayo, au kukosekana kabisa uwezo wa yai kupevuka ndani ya kila mzunguko wa hedhi.
NUKUU: Kumbe wakati hali hiyo inapojitokeza, unaweza ukaendelea kudhani kuwa, damu iliyokuwa ikikutoka, yaweza kuwa ndiyo ulikuwa mzunguko wako wa hedhi, kumbe sivyo!!. Na uelewe kuwa, unapopata hedhi lakini yai halijapevuka mle ndani, basi fahamu kuwa huo sio mzunguko wenyewe wa kipindi cha hedhi.
Ikiwa kama unajitahidi kutafuta ujauzito lakini huupati, basi inafaa sana kuelewa chanzo cha yai kwanini linashindwa kupevuka? Hivyo basi, fanya iwezekanavyo ufike hospitali haraka umuone daktari ili kufanya vipimo.
Je, Nini Maana Ya Yai Kushindwa Kuanguliwa?
Kushindwa kuanguliwa kwa yai ni hali ambayo hujitokeza wakati mwanamke anaporuka upevushaji wa yai. Wakati wa upevushaji, kifuko cha yai huliachia yai litoke ili liweze kuanza kusafiri kuelekea kwenye mfuko wa uzazi.
Sio kawaida kwa mwanamke katika miaka yake au umri wake wa kubeba mimba mayai yake yakashindwa kuanguliwa au kupevushwa. Kusema kweli, hiyo hali ya yai kushindwa kuanguliwa au kupevuka inaweza ikajitokeza na ukashindwa kuitambua. Na ndio maana wakati mwanamke anapopatwa na hali kama hii, anaweza akashangaa kuona kwanini anapata hedhi kama kawaida tu na anatokwa damu kila mwezi vizuri tu.
Katika mzunguko wa kawaida, utaona kuwa uzarishaji wa vichochezi au homoni za progesterone huamshwa na kile kitendo cha yai linapoachiliwa au kuanguliwa. Hizi ndizo homoni au vichochezi ambavyo husaidia mwili wa mwanamke kutengeneza vipindi vya hedhi visivyo badirikabadirika. Lakini pale yai linaposhindwa kuachiwa au kuanguliwa, basi kiwango kidogo cha homoni ama vichochezi vya progesterone kinaweza kusabisha mwanamke akatokwa na damu nyingi sana. Na ieleweke kuwa mwanamke anaweza kukosea kipindi hiki hata katika hedhi yake ya kweli.
Hali hii ya kutokwa na damu inaweza pia kusababishwa na kuongezeka kwa ukuta wa mfuko wa kizazi(uterus), unaojulikana kitaalam, “endometrium”, ambao kamwe hauwezi kujiendeleza wenyewe. Ni hali inayoweza kusababishwa na kushuka kwa homoni au kichochezi cha estrogen.
Je, Unaweza Ukajua Kwanini Wanawake Wanapatwa Na hali Ya Yai Kutopevuka Ama Kuanguliwa?
Mzunguko wa hedhi pasipo yai kuanguliwa kwa kawaida huja katika makundi mawili tofauti ya umri:
- Wasichana ambao hivi karibuni walioanza kuja hedhini
Umri unaofuata baada ya msichana kuvunja ungo, mara nyingi inaonyesha kwamba anaweza kupatwa na hali ya yai kutoanguliwa au kupevushwa.
- Wanawake Walio Karibu Kukoma Hedhi
Mwanamke mwenye umri kati ya miaka 40 au 50 huwa yupo katika hatari ya kupatwa na mabadiriko katika homoni au vichochezi vyake. Hali hii inaweza kusababisha mayai kushindwa kuanguliwa au kukomaa.
Wanawake wote kama nilivyotaja kwenye makundi hayo mawili, mara nyingi mabadiriko mengi hujitokeza kwenye miili yao. Mabadiriko ya ghafla kwenye vichochezi yanaweza kusababisha yai kutokuanguliwa au kupevushwa.
Visababishi vingine ni kama vile:
- Uzito wa mwili ambao unaweza kuwa mkubwa au wa chini.
- Kutokufanya kufanya mazoezi
- Tabia ya ulaji
- Msongo wa mawazo wa hali ya juu.
Ikiwa kama unapata hedhi kila baada ya siku 24-35, inamaana kwamba mayai yako yanapevuka au yanaanguliwa.
NUKUU: Hivi sasa, karibia asilimia 12% ya wanawake wana tatizo la kushindwa kupata ujauzito ama kuonyesha dalili za ujauzito. Hali sugu ya kutopata upevushaji wa mayai katika mifumo yao ya hedhi ndio kumekuwa kisababishi kikubwa cha wao kuwa wagumba.
Je, Hali Ya Yai kutokuanguliwa Ama Kupevushwa Inapimwaje?
Kupima hali ya yai kutokuanguliwa ama kupevushwa kunaweza kuwa rahisi sana pale tu mwanamke anapokuwa anakosa hedhi ndani ya mwezi 1, 2 au 3 na kuendelea au hedhi ambazo zinakuja ki makosa kabisa. Lakini hilo sio tatizo la kila mwanamke.
Kwa bahati mbaya, yapo mambo machache ambayo daktari wako anaweza kuyachunguza, ikiwa pamoja na:
- Kiwango chako cha homoni au vichochezi vya progesterone
- Ukuta wa mfuko wa kizazi(uterus).
- Damu yako kwa ajili ya baadhi ya kinga za mwili
NUKUU: Daktari wako pia anaweza kutumia kipimo cha ultrasound kwa kupiga picha ili kuweza kuona kwa ukaribu picha ya mfuko wa kizazi(uterus) pamoja na vifuko vyako vya mayai(ovaries).
Tiba Zake
James Herbal Clinic tuna dawa aina tatu zinazoondoa tatizo la ugumba na mayai kutokukomaa au kuanguliwa, nazo ni, CARD HERB, VITAMAKA na MULTICURE POWDER. Dawa hizi zina uwezo wa kuongeza vichochezi na kukomaza mayai ya mwanamke na kumfanya kupata ujauzito.
Je, unahitaji huduma? Tupigie kwa namba hizi: 0752389252 au 0712181626
Karibuni sana.