Umeshamaliza kufanya tendo la ndoa na mpenzi wako, unapomaliza, ukitazama chini utaona damu kwenye shuka. Huna hedhi na wala hutakiwi kutokwa na damu muda wowote, je nini kinachokufanya kutokwa na damu muda huo?
Wakati mwingine hali ya kutokwa na damu ukeni baada ya kujamiiana inaweza kuwa ya kutisha, lakini pia bado inaweza kuwa ya kawaida sana. Hali hii huathiri karibia asilimia 9% ya wanawake walio katika umri wa kupata hedhi. Ni hali ambayo pia hutokana na maambukizi. Kwa nadra sana huoneka kuwa ni ishara ya saratani.
Je, Nini Visababishi Vyake?
Visababishi vya kawaida vya damu kutoka ukeni baada ya kujamiiana huanzia kwenye shingo au mlango wa kizazi, ambayo ni sehemu nyembamba unapoishi mfuko wa kizazi(uterus) yenye muenekano kama mrija ambao hufunguka ndani ya uke.
Moja wapo ya visababishi hivyo ni kuvimba kwa mlango wa kizazi(cervix) ambao kitaalamu tunaita “cervicitis”. Ni hali ambayo inaweza kuwa endelevu na isiyo na madhara kabisa, au inaweza kutokea kwasababu ya maambukizi ya magonjwa ya zinaa ambayo unahitaji kuyatibu, kwa mfano; pangusa(chlamydia) au kisonono. Aina zote hizi mbili za kuvimba kwa mlango wa kizazi zinaweza kusababisha kutokwa na damu ukeni baada ya kujamiiana.
Sababu ya pili ya kutokwa na damu ukeni baada ya kujamiiana ni kuchomoza kwa mlango wa kizazi. Hali hii huwa ni hatari sana maana inaweza kusababisha wanandoa au wachumba wakaachana kwasababu huwa ni kero. Uvimbe wa tatizo hili mara nyingi huwa ni mdogo, takribani senimita 1 hadi 2. Mara nyingi vivimbe hivi hutokeza kwenye mdomo wa mlango wa kizazi. Vingi huwa ni saratani.
Sababu zingine za kutokwa na damu ukeni baada ya kujamiiana ni hizi zifuatazo:
- Msuguano wakati wa kujamiiana wala hakuna ute ukeni
- Pale hedhi inapoelekea kuisha
- Mambukizi kwenye mlango wa kizazi au ukeni kama vile PID
- Vidonda ukeni
- Dalili za saratani ya shingo ya kizazi
- Ngozi laini ya mlango wa kizazi kuchomoza nje ya kizazi
- Kibofu cha mkojo au mfuko wa kizazi kuchomoza nje ya uke
- Saratani ya shingo ya kizazi
Ukavu unaosababishwa na mambo haya unaweza pia kupelekea kutokwa na damu ukeni baada ya kujamiiana:
- Kunyonyesha
- Kujifungua
- Madawa ya uzazi wa mpango
- Kukoma hedhi, nk
Pale visababishi hivi vingi vinapokosa matibabu na wala havionyeshi madhara kwako, basi fahamu kuwa wakati mwingine hali ya kutokwa na damu ukeni baada ya kujamiiana inaweza kuwa ishara ya tatizo kubwa mno baadaye.
Sababu Hatarishi Za Kutokwa Na Damu Ukeni Baada Ya Kujamiiana
Unaweza kuwa na nafasi kubwa ya kutokwa na damu ukeni baada ya kujamiiana ikiwa kama una:
- Saratani ya shingi ya kizazi au tumbo la uzazi
- Unaelekea kukoma hedhi
- Unanyonyesha
- Unaosha uke wako kwa kutumia sabuni zenye marashi
- Hujaandaliwa vya kutosha pale unapotaka kuanza kujamiiana
- Una maambukizi kwenye mlango wa kizazi kama vile PID,nk
- Una maambukizi ya magonjwa ya zinaa
Je, Vipi Kuhusu Kutokwa Damu Ukeni Baada Ya Kujamiiana Huku Ukiwa Mjamzito?
Kama ni mjamzito, tayari utakuwa unafahamu kwamba mwili wako unabadirika kwa njia nyingi za ajabu. Moja ya njia hizi ni muendelezo mpya wa mishipa mishipa mingi ya damu kuzunguka eneo la mlango wa kizazi. Unapojamiiana, basi mishipa hii inaweza kutokwa na damu mara kwa mara, lakini kiwango kidogo cha damu pasipokuwa na maumivu yoyote haiwezi kusababisha madhara.
Lakini bado, ni vyema kufika hospitali na kuonana na daktari wako unapoona dalili mpaya pindi unapokuwa mjamzito. Na kama wewe ni mjamzito na unatokwa na damu nyingi wakati wa kujamiiana au baada ya kujamiiana, hakikisha unaenda hospitali haraka bila kuchelewa.
Ndugu msomaji wa makala hii naomba niishie hapa, nikukaribishe katika kipindi chetu cha maswali na maoni kutoka kwako.
Pia unaweza kutuma namba yako ya WHASaP ukaunganishwa na kwenye GROUP letu uweze kujifunza zaidi juu ya mambo ya afya.
Je, Unahitaji Huduma? Wasiliana nasi kupitia namba hizi: 0768 559 670 au 0712181626,
Arusha-Mbauda Maua
Karibu sana!
Asante