Unaweza usijue kuwa
una tatizo la mbegu kuwa nyepesi mpaka pale utakapoanza kutafuta mtoto na ukashindwa kufanikiwa. Vipimo vinaweza kuonyesha kwamba una mbegu chache kuliko idadi ya kawaida ya mbegu. Lakini zipo tiba mbalimbali nyingi za kuondoa tatizo hili.
Je, Nini Maana Ya Mbegu Kuwa Nyepesi(Oligospermia)?
Mbegu kuwa nyepesi imaanisha kwamba una chache chini ya mbegu milioni 15 katika mililita 1 ya manii. Mbali na kujulikana kama idadi ndogo ya manii, lakini bado inaweza kuwa chache zaidi ya kiwango nilichoonyesha hapo juu.
Je, Tofauti Inakuwaje Kati Ya Mbegu Kuwa Nyepesi Na Kukosa Mbegu Kabisa?
Mbegu kuwa nyepesi(oligospermia) inamaanisha kwamba una kiwango cha mbegu kwenye manii kinachopimika , lakini idadi ni ndogo kuliko idadi ya kawaida. Kama unatoa majimaji mepesi(azoospermia) inamaanisha kwamba hakuna mbegu zinazoweza kuonekana kwenye manii.
NUKUU: Kuwa na mbegu nyepesi ni tatizo linalomfanya mwanaume kuwa tasa au mgumba. Unaweza kuwa tasa kama umekuwa ukijaribu kubebesha mimba mwanamke lakini haikuwezekana.
Je, Nini Kinasababisha Mbegu Kuwa Nyepesi?
Yapo mambo mengi yanayoweza kusababisha wewe ukapatwa na tatizo la mbegu kuwa nyepesi au magonjwa mengine yanahusiana na mbegu. Orodha ya visababishi hivi ni kama ifuatavyo;
- Maambukizi ya magonjwa ya zinaa
- Maambukizi katika njia ya mkojo au UTI
- Mirija ya mbegu kuziba
- Joto kali kwenye korodani
- Madawa ya kulevya
- Mazingira yenye kemikali nyingi
- Matatizo ya homoni
- Magonjwa
Je, Nini Dalili Ya Mbegu Kuwa Nyepesi?
Dalili kuu au ishara za mbegu wa nyepesi ni kutokuwa na uwezo wa kumpa mwanamke ujauzito ndani ya mwaka mmoja ukishiriki tendo la ndoa bila kutumia kinga.
Je, Ugonjwa Huu Unapimwaje?
Wahudumu wanaokuwa hospitali watachukua historia ya afya yako pamoja na vipimo. Wanaweza kuagiza vifanyike vipimo vingine kama vile:
- Uchunguzi wa manii pamoja na vipimo vya mbegu kama zinafanya kazi
- Kipimo cha mkojo ili kuhakikisha kama mbegu zinarudi nyuma
- Kipimo cha kuzamisha kwenye viungo vyako vya uzazi
- Kipimo cha mfumo wa endocrine ili kupima viwango vya homoni
- Kupima magonjwa ya kurithi, nk.
Je, Tatizo Hili Tunaweza Kulitibu Vipi?
Tiba ya ugonjwa huu itategemeana na chanzo chake. Unaweza kuzifanya mbegu zako zikawa nzito na zikaongezeka ikiwa kama utaachana na tabia za mitindo mimbaya inayochangia mbegu kuwa nyepesi kama vile ulaji mirungi, unywaji pombe, uvutaji sigara, upigaji punyeto, nk.
Vyanzo vingine vinaweza kuhitaji matibabu mengine. Kwa mfano:
- Unaweza kuhitaji upasuaji mirija ya kupitisha mbegu ikiwa kama imeziba
- Daktari anaweza kukushauri upate dawa za homoni
- Daktari anaweza kukushauri utumie dawa za antibiotic ili kuua bakteria
- Daktari wako anaweza kukushauri uchunguze sana ili kuelewa endapo kama uume wako hausimami au endapo kama unafika kileleni kabla ya muda.
Na hapa ndio mwisho wa makala yetu wapendwa wasomaji, nipende kukaribisha kipindi cha maswali na maoni kwa msomaji.
Je, unahitaji huduma? Unaweza kuwasiliana nasi kwa namba hizi: 0752389252 au 0712181626.
Pia tunatoa masomo ya afya katika Group letu la WHATSAP, unaweza ukatuma namba yako ukaweza kuunganishwa na darasa letu na utapata ushauri bure.
Karibuni sana!