Kutokwa na damu ya hedhi isiyo ya kawaida humaanisha kwamba damu ya hedhi inaweza kuwa nyingi sana tena kwa muda mrefu kuliko kawaida au unaweza usione hedhi kabisa. Kutokwa na damu ya hedhi mara mbili ndani ya mwezi mmoja pia huwa ni ishara ya kutokwa na damu ya hedhi isiyo ya kawaida. Hili huwa sio tatizo kubwa sana lakini linaweza kuwafanya wasichana kupungukiwa na damu au kupotea kwa chembe nyekundu za damu.
Ikiwa kama msichana ana tatizo la kutokwa na damu ya hedhi isiyo ya kawaida, inaweza kumaanisha kwamba vipindi vyake vya hedhi huchukua muda mrefu damu kukata au kutokwa na damu nyingi sana kuliko kawaida. Au inaweza kumaanisha kinyume, kwamba damu yake ya hedhi ni nyepesi na vipindi vyake havitpatikani kwa muda sahihi kama inavyotakiwa mara kwa mara.
Kwakuwa kutokwa na damu ya hedhi isivyo kawaida kwa kawaida huwa sio tatizo, na ndio maana madaktari mara nyingi huwa hawana kitu chochote cha kufanya. Lakini wakati mwingine wanachukua tahadhari ikiwa kama tatizo linasababisha kutokwa na damu isiyo ya kawaida. Madaktari pia wanaweza kutibu ugonjwa huu ikiwa kama unasababisha matatizo mengine. Kwa mfano, madaktari wanaweza kuwa na mashaka kwamba msichana anaweza kupungukiwa na damu ikiwa kama anatokwa na damu muda mrefu kuliko kawaida.
Je, Nini Husababisha Kutokwa Na Damu Muda Mrefu?
Mara nyingi, hali ya kutokwa na damu isivyo kawaida hutokea kwasababu ya mabadiriko ya viwango vya homoni mwilini.
Kwa mabinti wadogo, moja ya visababishi vya mabadiriko ya homoni ni pale mwili unaposhindwa kuachilia yai litoke kwenye vifuko vya mayai. Hali hii tunaita yai kushindwa kupevuka(anovulation).
Ile hali ya kuruhusu yai litoke nje ni sehemu ya mzunguko wa hedhi. Ikiwa kama mwili wa msichana hauwezi kuruhusu yai litoke, mabadiriko ya homoni yanaweza kupelekea msichana kutokwa na damu ya hedhi kidogokidogo mara kwa mara au damu nyingi sana ya hedhi kwa muda mrefu.
Hali yay ai kutokupevuka inaweza kutokea baada ya msichana kuanza kupata hedhi. Hii ni kwasababu ishara kutoka kwenye ubongo mpaka kwenye vifuko vya mayai bado hazijakamilika kabisa. Inaweza ikakaa kwa miaka kadhaa mpaka pale vipindi vya hedhi vya msichana vitakapokuwa sawa.
Vitu vingine vinavyoweza kupelekea msichana kutokwa na damu ya hedhi isiyo ya kawaida ni:
- Vivimbe vingi vidogo vidogo kwenye vifuko vya mayai
- Mazoezi mazito
- Kutokupata vyakula vyenye virutubisho
- Msongo wa mawazo
- Kuvimba kwa tezi ya thyroid.
Je, Dalili Zake Zinakuwaje?
Kila mwanamke hupatwa na hali ya kutokwa na damu nyingi ya hedhi kutokana na mabadiriko ya majira. Je, utaweza kufahamu vipi ikiwa kama unatokwa na damu ya hedhi isiyo ya kawaida? Ni daktarin tu ndiye anayeweza kukuambia kwa uhakika, lakini zipo dalili ambazo zinaweza kuashiria kwamba hedhi inayotoka sio ya kawaida, nazo ni hizi:
- Unapobadirisha pedi kila baada ya lisaa limoja
- Kipindi chako cha hedhi kinapoendelea kwa muda wa siku 10
- Kutokwa damu nyingi sana mfululizo.
NUKUU: Kama ukiona dalili hizo, fanya haraka ufike hospitali. Kutokwa na damu mara mbili kwa mwezi au baada ya kumaliza kushiriki tendo la ndoa pia kunaweza kuashiria kuwa unapata hedhi isiyo ya kawaida.
Ikiwa kama hedhi yako itakoma Zaidi ya miezi mitatu, pia fika hospitali uonane na daktari. Kama hupati hedhi, basi ukuta wa tumbo la uzazi unaweza kuendelea kuvimba. Hatimaye utahitaji damu itoke.
Je, Hali Ya Kutokwa Na Damu Nyingi Ya Hedhi Isiyo Ya Kawaida Inapimwa Vipi?
Kwa kawaida ikiwa kama unahitaji kufahamu vyanzo vya tatizo hili, mgonjwa unapaswa ufike hospitalini ukapime mambo haya:
- Tumbo la uzazi
- Vivimbe kwenye vifuko vya mayai
- Magonjwa ya zinaa hasa kisonono
- Damu
Ndugu msomaji ikiwa kama unasumbuliwa na tatizo hili, nakushauri uanze kwamba upate vipimo uweze kuona vyanzo vya tatizo lako, baadaye anza matibabu bila kuchelewa.
Nashukuru sana napenda niishie hapa ili niweze kukuachia kipindi cha maswali na maoni yako.
Pia unaweza ukatuma namba yako ya WHATsAP ili tuweze kukuunganisha na darasa letu uweze kujifunza masomo ya afya kila siku.
Je, Tiba Yake Inakuwaje?
James Herbal Clinic tunazo dawa za asili zenye uwezo wa kuondoa tatizo hili na kukomesha kabisa lisiendelee. Unahitaji huduma, wasiliana nasi kwa namba hizi: 0752389252 au 0712181626.
Arusha-Mbauda,
Karibu sana!