Je, Nini Tofauti?
Kama ukipata masumbufu katika njia za siri au wakati unapokojoa, tambua kuwa una maambukizi. Aina mbili za maambukizi ambazo kwa kawaida huathiri maeneo haya huwa ni maambukizi katika njia ya mkojo au UTI pamoja na maambukizi ya fangasi. Aina hizi za maambukizi huwapata wanawake, lakini wanaume nao wanaweza wakapatwa pia.
Japo magonjwa haya ni tofauti, lakini baadhi ya dalili zake, visababishi vyake, na njia za kukinga vyote hufanana. Magonjwa haya yote mawili yanapaswa kuchunguzwa na daktari ili kuweza kutibiwa, na yote haya yanatibika.
NUKUU: Ingawa UTI na maambukizi ya fangasi huwa ni tofauti sana, lakini bado tu unaweza kuyapata yote mawili kwa pamoja. Kusema kweli, UTI inapotibiwa na madawa ya vidonge kwa muda mrefu bila mafanikio yoyote, inaweza kupelekea muhusika akapatwa na maambukizi ya fangasi ukeni. Naomba wenye maambukizi haya muwe na ufahamu ili kujihadhali kukaa na ugonjwa muda mrefu.
Je, Dalili Zake Zinakuwaje?
UTI na fangasi ni maambukiz mawili tofauti. Dalili zake zinaweza kuwa katika eneo la pamoja, lakini zinatofautiana. Dalili za UTI kwa kawaida huathiri njia ya mkojo. Zinaweza kusababisha hali ya kuwaka moto wakati unapokojoa, au unaweza kuhisi kuhitaji kukojoamara kwa mara.
NUKUU: Dalili za maambukizi ya fangasi zinaweza kuwa ni kuhisi maumivu wakati unapokojoa, lakini pia utahisi maumivu na muwasho katika maeneo yaliyoathiriwa. Maambukizi ya fangasi ukeni pia husababisha kutokwa na uchafu ukeni mzito wenye rangi kama maziwa.
- Dalili Za UTI
- Kuhisi maumivu au hali ya kuwaka moto wakati wa kukojoa
- Kuhisi kukojoa mara kwa mara
- Kukojoa mkojo mchafu wenye rangi ya kijivu au damu kwa mbali
- Kutokwa na mkojo wenye harufu mbaya
- Kuhisi homa, kichefuchefu au kutapika
- Kuhisi maumivu maeneo ya tumbo la chini au kiunoni
- Kuhisi maumivu sehemu za nyonga
- Dalili Za Fangasi Sehemu Za Siri
- Kuhisi maumivu wakati wa kukojoa au tendo la ndoa
- Kuhisi muwasho sehemu za mashavu ya uke
- Kuvimba maeneo ya mashavu ya uke
- Kutokwa na uchafu ukeni wenye rangi ya maziwa mgando
- Kupatwa na vidonda au michubuko ukeni
NUKUU: Maambukizi katika njia ya mkojo au UTI ambayo huathiri eneo la chini la mfumo wako wa mkojo huwa mabaya kidogo kwa muhusika. Maambukizi haya yanapokaribia kwenye figo zako yanaweza kusababisha madhara na dalili mbaya kwa muhusika.
Je, Nini Visababishi Vyake?
UTI hutokea pale unapopatwa na bakteria kwenye mfumo wa mkojo. Mfumo wako wa mkojo hujengwa na viungo kama vifuatavyo:
- Figo
- Mirija ya mkojo
- Kibofu cha mkojo
- Njia ya mkojo
Huhitaji kuwa na nguvu nyingi za tendo la ndoa pale unapokuwa na maambukizi ya UTI. Vitu au mambo yanayoweza kusababisha bakteria kujengeka kwenye njia ya mkojo na kusababisha UTI huwa kama ifuatavyo:
- Kinyesi chenye bakteria kama vile E.Coli
- Kujamiiana
- Kupatwa na magonjwa ya zinaa
Maambukizi ya fangasi sehemu za siri hutokea pale fangasi wengi wajulikanao kama Candida Yeast wanapojengeka kwenye eneo lenye unyevunyevu juu ya ngozi, na kusababisha maambukizi.
Mwili wako unaweza kuwa tayari una maambukizi haya ya fangasi, lakini unaweza ukapatwa na madhara pamoja na maambukizi pale yanapojengeka juu ya ngozi. Unaweza ukapata hali hii hata kama hufanyi tendo la ngono. Visababishi vya maambukizi ya fangasi sehemu za siri huwa ni:
- Mabadiriko kwenye kinga ya mwili wako yaliyosababishwa na msongo wa mawazo, homa, ujauzito, nk.
- Utumiaji wa madawa ya vidonge muda mrefu kama vile, vidonge vya uzazi wa mpango, nk
- Shinikizo la juu la damu au kisukari
- Kuvaa mavazi yenye kubana hasa chupi ambazo hujenga unyevunyevu maeneo ya uke.
Je, Maambukizi Ya UTI Na Fangasi Yanakuwaje Ya Kawaida? Je, Nani Huyapata?
Maambukizi katika njia ya mkojo au UTI ni ya kawaida na katika wanawake 25, basi wanawake 10 ndio hupatwa na maambukizi hayo, lakini katika wanaume 25, 3 ndio hupatwa na maambukizi hayo katika maisha yao.
NUKUU: Wanawake hupatwa na UTI kwa kasi sana kuliko wanaume kwasababu njia ya mkojo ya mwanamke ni fupi kuliko ya mwanaume, na ipo karibu uke pamoja na njia ya haja kubwa, hali ambayo husababisha kupatwa na bakteria.
Unaweza pia kuwa kwenye hatari zaidi ya kupatwa na UTI ikiwa kama wewe ni:
- Mjamzito
- Ulitumia madawa mbalimbali ya bakteria
- Umekuwa mzito au mnene
- Umekoma hedhi
- Una kisukari
- Una mawe ya figo au mirija ya mkojo kuziba
- Umedhoofisha mfumo wako wa kinga
Wanawake hupatwa na maambukizi ya fangasi sehemu za siri mara kawa mara kuliko wanaume, na asilimia 75% za wanawake hutapatwa na maambukizi ya fangasi ukeni katika maisha yao. Maambukizi ya fangasi hujitokeza ukeni na kwenye mashavu ya uke, lakini pia unaweza kupata fangasi kwenye matiti ikiwa kama unanyonyesha na kwenye maeneo mengine yenye unyevunyevu mwilini mwako, kama vile mdomoni.
Je, Unapaswa Kumuonaje Daktari?
Maambukizi yote ya UTI pamoja na fangasi yanapaswa yachunguzwe na kupimwa na daktari ili kuyazuia yasiendelee kuwa mabaya. UTI isiyotibiwa inaweza kusababisha maambukizi mabaya kwenye figo. Maambukizi ya fangasi sehemu za siri pia yanaweza kuwa kitu kibaya au dalili zinaweza kutoka kwenye ugonjwa mwingine kama vile maambukizi ya magonjwa ya zinaa.
Je, Vipimo Vinafanyikaje?
UTI pamoja na maambukizi ya fangasi sehemu za siri hupimwa kwa utofauti. UTI hupimwa kwa sampuli ya mkojo. Unaweza ukaambiwa kujaza kikombe kidogo. Maabara itapima mkojo kwa ajili ya kuangalia bakeria Fulani ili kupima ugonjwa.
Katika makala hii naomba niishie hapa, tutaonana katika makala zinazofuata. Nipende kuwakaribisha tu wale wote wenye maswali, unaweza kutuma maswali yako kupitia email au whatsap na utajibiwa.
Unahitaji huduma, unaweza kuwasiliana nasi kwa namba hizi: 0752389252 au 0712181626.
Pia tuna darasa letu zuri kwa njia ya WHATSAP, unaweza kutuma namba yako ukaunganishwa na darasa letu.
Karibuni sana!