Je, Nini Unapaswa Kufahamu Kuhusu Ulaji Wa Udongo?

Geophagia ni neno rasmi la kutamani kula vitu vichafu, ikijumuisha mkaa, majivu au udongo. Kula uchafu kunaweza kupunguza maumivu ya utumbo kwa baadhi ya watu, lakini pia kunaweza kusababisha matatizo ya kiafya kama vile upungufu wa damu na kusababisha sumu.

Watu hula kwa makusudi mara kwa mara vitu ambavyo sio chakula. Watu wanaweza kutamani uchafu kutokana na upungufu wa lishe mwilini, mimba, mitindo ya malezi, au sababu nyinginezo.

Ingawa watu wanaweza kutumia baadhi ya virutubisho wakati wa kula uchafu, tabia hii pia huongeza hatari ya mtu kujawa na sumu mwilini.

Je, Nini Kinachowafanya Watu Kula Udongo?

Mambo yafuatayo hapo chini yanaweza kumfanya mtu kuendelea kula udongo, nayo ni haya:

Ujauzito

Mtu anaweza kula udongo kutokana na ujauzito. Katika utafiti inaonyesha kwamba wanawake wengi wanaokuwa na ujauzito hupenda kula udongo. Baadhi ya sababu ambazo wajawazito wengi wengi hutoa ni pamoja na:

  • Kutamani muonekano na harufu ya udongo,
  • Imani ya kwamba udongo unafanya kazi ya ziada kuongeza madini ya chuma
  • Kuboresha afya ya mtoto
  • Kupunguza kiungulia kinachohusiana na ujauzito na hali ya kichefuchefu
  • Kuchoka
  • Kufurahia ladha ya chumvi ya udongo.

Ulaji vitu hivi una uhusiano na tatizo la afya ya akili | Mwananchi

Umri

Ulaji wa udongo ni jambo la kawaida zaidi kwa watoto, wajawazito, na watu walio na upungufu wa akili. Ni shida ya ulaji ambayo husababisha watu kula vitu ambavyo sio chakula. Hii inaweza kujumuisha vitu kama hivi vifuatavyo:

  • Majivu ya sigara
  • Barafu
  • Karatasi
  • Maganda ya yai
  • Majivu au mkaa

Mambo kama vile mfadhaiko au msongo wa mawazo, kutelekezwa kwa watoto, na kukosa ujauzito kunaweza kusababisha kuwapo kwa tatizo la kula udongo.

Upungufu Wa Lishe

Upungufu wa madini ya chuma na zinki unaweza kumfanya mtu kuwa na tabia ya kula udongo.

Sababu Zingine:

Sababu zingine za hatari katika ulaji wa udongo ni pamoja na hizi hapa zifuatazo:

  • Msongo wa mawazo
  • Tabia ulizojifunza tangu utotoni
  • Hali ya afya ya akili
  • Unyanyasaji wa watoto
  • Kuharibika kwa familia na hivyo kukosa malezi mazuri

Je, Nini Madhara Ya Kula Udongo?

Tabia ya ulaji udongo inapoendelea kwa muda mrefu husababisha madhara haya yafuatayo:

  • Kukosa choo
  • Mwili kupungukiwa na virutubishi
  • Kuwa na kiwango kidogo cha madini ya potasiam
  • Kumeza wadudu au vimelea

Jinsi Ya Kukabili Tatizo La Ulaji Wa Udongo

Watu wenye tabia ya ulaji udongo wanapaswa kufanyiwa vipimo vya upungufu wa lishe.

Mara tu mtu anaporekebisha upungufu wowote wa lishe mwilini mwake, kama vile kutumia tiba lishe (food supplements) zenye virutubishi vya madini ya chuma au zinki, anaweza kuacha kusumbuliwa na tatizo la kutamani udongo.

Hivyo, ikiwa kama unasumbuka na tatizo la kutamani kula udongo, inafaa fika hospitali, muone daktari anayehusika na mambo hayo atakusaidia.

Rafiki msomaji, napenda kuishia hapa, nikukaribishe kwa kipindi cha maswali.

Pia unaweza kutuma namba yako ya WHATSAP ili nuweze kujiunga na darasa letu la masomo ya afya.

Je, Unahitaji huduma? Basi, wasiliana nasi kwa namba hizi: 0768 559 670/0712 181 626,

Arusha-Mbauda

Karibu sana!

 

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *