JE, UCHAFU UNAOTOKA UKENI UNAWEZA KUKUZUIA USIPATE UJAUZITO?

Wanawake wengi hushindwa kujali wanapotokwa na uchafu, isipokuwa tu wanakerwa  mara wanapoona nguo ya ndani au chupi kuwa imechafuka. Lakini kumbuka kuwa hali ya kutokwa na uchafu wa kawaida huonyesha kabisa kuwa uko tayari kupata ujauzito. Utoko au uchafu unaotoka ukeni hubadirika wakati wa mzunguko wako wa hedhi, na kama ukiacha kutambua mambadiriko haya, basi utakosa taarifa muhimu ambayo inaweza kukusaidia kupata ujauzito wako haraka.

 

Tokeo la picha la image of a woman swipping the cervical mucus internally  in the vagina

Leo ninapenda kuelezea kila kitu unachohitaji ili kufahamu juu ya aina ya uchafu unaokutoka ukeni unaoitwa, “Uteute”. Napenda nieleze jinsi ute unavyokuwa, je, unakuwa na kazi gani, na je unaweza kuutambua vipi ute huo ili uweze kufanya tendo la ndoa na mwenzi wako, na jinsi gani unaweza kutambua ikiwa kama tayaru uko kwenye siku za hatari.

Je, Nini Maana Ya Uchafu Unaotoka Ukeni?

 

 

 

Uchafu ukeni huwa ni kisafishio kinachotoka nje ya uke. Uchafu huu huwa una kazi ya kusafisha uke ili kuufanya uwe safi, huzuia maambukizi, huondoa kabisa seli zilizozeeka, na kupata ujauzito. Uchafu wenye muonekano kama  kamasi huwa ni aina ya uchafu unaotoka ukeni ambao huonekana mara kwa mara katika mzunguko wa hedhi wa mwanamke. Kizazi makamasi hubadirika wakati wa mzunguko wa hedhi. Sio ute wenye  kutia hamu au hisia, ambao hutengenezwa  pale mwanamke anapokuwa na nyege. Ute wa hisia unaweza kumfanya mwanamke akafurahi pale anapofanya tendo la ndoa, lakini huwa hauna vitu vya uzazi kama ilivyo uteute wa siku za hatari.

NUKUU: Ujauzito, au kunyonyesha, au maambukizi yanaweza pia kuathiri  uzito, rangi na harufu ya uchafu utokao ukeni.

 

 

 

Je, Kwanini Ute Makamasi Ni Wa Muhimu Kwa Ajili Ya Utungaji Mimba?

 

 

 

Kwa kawaida katika kipindi chote cha mzunguko wa hedhi, uke huwa wenye uchachu na haupatani kabisa na mbegu za mwanaume. Lakini aina nzuri ya ute utelezi  inapokuwepo, basi hurutubisha seli za mbegu za mwanaume na kuzisaidia ziweze kudumu muda mrefu ndani ya uke.

Picha inayohusiana

NUKUU: Ute utelezi huonekana katika siku za hatari ili kusaidia mbegu za mwanaume ziweze kusafiri na kukutana na yai lako.

 

Je, Uzazi Wa Mwanamke Unatambuaje Kuwa Ute Utelezi Umekaribia Kutoka?

 

 

 

 

 

Ili yai lipevuke, homoni ya estrogen inapaswa iongezeke. Kupanda kwa kiwango cha homoni estrogen husaidia kutengeneza ute utelezi ili kurutubisha yai, na tofauti za mbegu za mwanaume.

 

 

Unapoona mabadiriko haya kwenye uteute unaotoka kipindi cha siku za hatari, basi huwa kuna mabadiriko mengine yanayojitokeza ambayo unapaswa uyatambue, nayo huwa ni kupungua kwa hali ya chumvichumvi kwenye uteute unaotoka pale yai linapokaribia kupevuka. Katika mizunguko yako yote ya hedhi, uteute unaotoka huwa wenye radha ya chumvichumvi na huwa ni adui wa mbegu za mwanaume. Lakini katika siku zinzoelekea yai kupevuka, ile hali ya chumvichumvi kwenye uteute hupungua.

 

NUKUU: Kiwango cha majimaji  na tindikali au chumvichumvi kidogo huyafanya mazingira ya kuwa mazuri kwa ajili ya mbegu za mwanaume. Homoni ya estrogen huwajibika sana katika hili badiriko. Viwango vya homoni ya estrogen hupanda kwa ajili ya maandalizi ya upevushaji wa yai, na kusababisha uteute kuongezeka kuwa na majimaji na kupungua hali ya chumvichumvi au tindikali. Mazingira haya husaidia mbegu za mwanaume kuweza kuishi kwa siku 3-5.

 

Je, Uteute Wa Siku Za Hatari Unawezaje Kukusaidia Wewe Kupata Ujauzito Haraka?

 

 

Uteute ni njia ya mwili wako kuweza kukutaarifu kuwa yai linaelekea kupevuka muda sio mrefu. Unapokuwa na uhakika kuwa unafanya tendo la ndoa pale siku za yai kupevuka zinapokaribia, basi ni moja ya njia zitakazo kuongezea nafasi ya kupata ujauzito.

Tokeo la picha la image of pregnant woman

NUKUU: Wanawake wengi hungojea kipindi cha hedhi kipite kwanza ndio wafanye tendo la ndoa, lakini njia hii inaweza kukufanya ukachelewa kufanya tendo la ndoa kwenye mzunguko wako wa hedhi, huku siku zako za kupata ujauzito zikiwa zimepita. Japo uteute huanza kubadirika siku kadha wakadha hata kabla hujatumia kipimo, lakini bado ni ishara tosha ya kukuonyesha kuwa ni muda gani unaingia katika siku zako za hatari. Nipende kukushauri tu kwamba, uonapo uteute ule mweupe kama yai la kuku, basi tambua kuwa hizo ndio siku za hatari na unapaswa uanze kufanya tendo la ndoa bila kuchelewa. Jitahidi kabisa hata mara tatu kwa siku mfululizo.

 

 

Je, Unawezaje Kuuona Uteute Wako Wa Siku Za Hatari?

 

 

 

 

 

Unaweza ukauona uteute wa siku za hatari kwa ndani, kwa kuangalia kwenye chupi au baada ya kujitawaza, au ndani ya uke kwa kuingiza kidole ndani. Baadhi ya wanawake hutoa uteute mwingi sana wa siku za hatari, ambao ni rahisi sana kuuona kwenye chupi au wakati unapojitawaza. Wanawake wengine hutoa uteute mchahche tu wa siku za hatari, na inaweza kuwa vigumu kuutambua kwa ndani. Ili uweze kujua kuwa umo ndani ukeni, basi unapaswa uingize vidole viwili visafi ukeni mwako. Toa vidole nje utaona uteute huo.

 

Picha inayohusiana

NUKUU: Hata hivyo utachovya uteute huo ukeni, utauangalia vizuri, na ukumbuke pia kuwa ute ute unaonyesha kuwa uko tayari kupata ujauzito huwa wenye kulendemka kama ute wa yai la kuku, na mara nyingi unaweza kuvutika sana au unaweza kuwa kama majimaji kwa mbali na usivutike.

 

 

Je, Unajuaje Kama Unatengeneza Uteute Wa Kutosha Katika Siku Za Hatari?

 

 

 Baadhi ya wanawake huwa na wasiwasi kama wanaposhindwa kuona uteute wa siku za hatari kwenye chupi zao na kuhitaji kuingiza kidole ukeni, inamaanisha hawana uteute wa kutosha. Hata hivyo, kiwango cha uteute unachokiona huwa sio njia nzuri ya kuhukumu kama unatoa ute wa kutosha ili kupata ujauzito. Uteute wa siku za hatari unaofaa kwa ajili ya kubeba ujauzito ni ule unaokuwa ndani ya uke. Ingiza vidole ukeni, ukiona vimetoka na uteute wa kulendemka unavutika vizuri, tambua sasa kuwa muda wa mchezo umewadia. Changamkia fursa hiyo wewe unayetaka mtoto.

 

 Je, unahitaji huduma kutoka James&Ferdinand Herbal Clinic? Tupigie kwa namba hizi: 0752389252 au 0712181626.

 

Tunapatikana: Arusha-Mbauda na Njombe Makambako

 

Karibuni sana!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *