JE, UGONJWA WA MALENGELENGE(TRICHOMONIAS) WAWEZA KUWA CHANZO CHA PID(PELVIC INFLAMMATORY DISEASE)? JE, NINI CHANZO, DALILI NA MADHARA YAKE?

Malengelenge au Trichomoniasis ni ugonjwa unaoenezwa kwa njia ya ngono kama magonjwa mengine ya zinaa. Maambukizi ya ugonjwa huu yanaweza kutokea hata kwa mtu asiye kuwa na dalili za maambukizi ya ugonjwa huu. Wanawake hupata maambukizi ya ugonjwa wa Malengelenge kutoka kwa wanaume, na wanaume pia huupata kutoka kwa wanawake walioambukizwa. Matumizi ya kondom huzuia maambukizi, lakini sio salama sana japo yanasisitizwa kila mara.

 

Related image

 

Vimelea wa Malengelenge wanaweza pia kukaa kwenye shuka, taulo, au chupi, hivyo unaweza kupata maambukizi ikiwa kama utachangia shuka ama taulo hasa katika vyumba vya nyumba za wageni(guest house).

 

 

Ugonjwa huu sababishwa na vimelea vya jamii ya protozoan vinavyojulikana kama Trichomonas vaginalis. Dalili za Trichomoniasis huanza kuonekana kuanzia siku ya 4 hadi ya 28 baada ya mtu kupata maambukizi ya ugonjwa huu.

 

 

Malengelenge (Trichomoniasis) pia hujulikana kwa majina mengine kama Trichomonas vaginitis au Trich. Nafikiri wapo ambao waliwahi kwenda maabara ama hospitali, baada ya vipimo wakapata majibu kama hayo, “Trich”.

 

 

Ugonjwa huu huonekana sana kwa wanawake kuliko wanaume labda kutokana na wanaume kutoonyesha dalili zozote wakati wa maambukizi au kutokana na majimaji ya kwenye tezi dume kuwa na madini ya zinc ambayo huathiri vimelea hivi vya Trichomonas vaginalis vinavyosababisha ugonjwa huo. Trichomoniasis hupatikana kwa njia ya kujamiana bila kutumia kinga na mtu aliyeathirika ugonjwa huo.

Wanawake wengi wamekuwa wakisumbuliwa na ugonjwa huu, na ili kuufahamu vyema ni bora kwanza tuelezee nini hutokea wakati wa maambukizi au Pathofiziolojia ya ugonjwa huo.

 

Image result for image of trichomoniasis parasite

NUKUU: Umbile la vimelea vya Trichomonas vaginalis ni sawa na chembechembe moja ya damu nyeupe kwa upana, ingawa wakati mwingine ukubwa unaweza kutofautiana kulingana na mazingira. Kuwepo kwa umbile kama mikono kwa nje kwenye kimelea hicho inayojulikana kama flagellum, husaidia vimelea hivi kuingia kwenye tishu za mrija wa kupitisha mkojo pamoja na tupu ya mwanamke na hivyo kuharibu seli aina ya epithelium na kusababisha vidonda katika tishu hizo. Hii ndiyo sababu, watu wanaopata ugonjwa huu huwa kwenye hatari kubwa ya kupata ugonjwa wa Ukimwi (HIV) na magonjwa mengineyo ya zinaa.

 

 

Je, Mgonjwa Huwa Ana Dalili Gani?

 

Watu wengi wenye ugonjwa huu huwa hawaonyeshi dalili. Lakini dalili zinapotokea, nazo kwa kawaida huwa kama ifuatavyo:

 

  1. Kwa Wanawake
  • Mwasho ama kuhisi kuwaka moto sehemu za siri
  • Mashavu ya uke kuwa mekundu
  • Kutokwa na uchafu wa njano wenye harufu mbaya
  • Kotokwa na damu sehemu ya uke
  • Kuhisi maumivu wakati wa kukojoa mara kwa mara
  • Maumivu wakati wa kufanya tendo la ndoa
  • Maumivu ya tumbo

 

NUKUU: Mwanamke anaweza pia kuona dalili hizo hapo juu kuwa mbaya zaidi baada ya kutoka hedhini, pia dalili hizo zinaweza kuchanganyikana na maambukizi ya fangasi. Hivyo napenda kuwasihi sana kinamama kuwa makini waendapo kupata vipimo ili kubaini ugonjwa wa fangasi na wa malengelenge, kwani unaweza kuambiwa una fangasi kumbe ni maambukizi ya malengelenge au unaweza kuambiwa una malengelenge, kumbe ni maambukizi ya fangasi.

 

Kwa upande wa mwanamke, ugonjwa huu huathiri shingo ya kizazi (cervix), mrija wa mkojo, tupu ya mwanamke, kibofu cha mkojo na tezi zinazojulikana kama Bartholin glands na Skene glands.

 

 

 

  1. Kwa Wanaume

 

 

Mara nyingi wanaume huwa wanaonyesha dalili, nazo huwa kama ifuatavyo:

 

 

  • Kutokwa na uchafu kwenye uume

 

  • Maumivu makali wakati wa kukojoa

 

 

  • Kuhisi hali ya kuwaka moto baada ya kufika kileleni baada ya tendo la ndoa.

 

  • Muwasho ndani ya uume

NUKUU: Kwa wanaume vimelea hivi vya Trichomonas vaginalis hupatikana katika sehemu za siri za mwanamume, sehemu ya nje ya mrija wa kupitisha mkojo (anterior urethra), kwenye tezi dume, kwenye mirija ya kuhifadhi na kutoa mbegu za kiume (epididymis) na hata kwenye mbegu zenyewe.

 

 

 

 

Je, Nini Madhara Ya Ugonjwa Huu?

 

 

Ugonjwa huu usipotibiwa mapema na ukawa sugu, huwaongezea wanawake hatari ya kupata saratani ya shingo ya kizazi, lakini pia kwa upande wa wanaume huwaongezea hatari ya kupata saratani ya tezi dume.

.

 

TIBA ZAKE

 

                   

 

James Herbal Clinic tuna tiba nzuri zenye uwezo mkubwa wa kuondoa matatizo ya maambukizi ya ugonjwa wa Trichomoniasis au malengelenge, pande zote mbili kwa mwanaume na mwanamke pia, nazo ni MULTI-CURE POWDER, FRESH HERB na VITAMAKA.

 

 

Je, Unahitaji huduma? Tupigie kwa namba: 0752389252 au 0712181626

 

 

Arusha-Mbauda Pepsi

 

 

Karibuni sana

One thought on “JE, UGONJWA WA MALENGELENGE(TRICHOMONIAS) WAWEZA KUWA CHANZO CHA PID(PELVIC INFLAMMATORY DISEASE)? JE, NINI CHANZO, DALILI NA MADHARA YAKE?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *