JE, UGONJWA WA PANGUSA UNAWEZA KUSABABISHA MIMBA KUHARIBIKA?

Pangusa ni miongoni mwa magonjwa ya zinaa ambayo ni ya kawaida kabisa, ambayo huwapata wanawake wengi kila mwaka. Kama ukipimwa ukakutwa na maambukizi ya ugonjwa wa pangusa huku ukiwa mjamzito, basi utakuwa na maswali mengi mno ya kujiuliza.

Can Chlamydia Cause a Miscarriage?

NUKUU: Hapa kuna kile tumekiandaa ili uweze kuelewa juu ya madhara ya ugonjwa wa pangusa unapokuwa mjamzito, pamoja na vipimo na matibabu yake.

Je, Ugonjwa Wa Pangusa Unasababisha Mimba Kuharibika?

Kuna baadhi ya shuhuda kwamba ugonjwa wa maambukizi ya pangusa wakati wa ujauzito yanaweza kusababisha mimba kuharibika.

Mnamo mwaka 2011, utafiti wa damu, sampuli za uteute ukeni na kwenye kondo kutoka kwa wanawake uliofanyika kule nchini Uswis, ilionekana kwamba kiwango kikubwa cha dalili za maambukizi ya ugonjwa wa pangusa zilionekana kwa wanawake ambao mimba zao ziliharibika.

Je, Matokeo Ya Ugonjwa Wa Pangusa Na Ujauzito Ni Nini?

Inaonyesha kwamba, ugonjwa wa pangusa usipotibiwa ukaisha unaweza kusababisha vihatarishi vya matokeo mbalimbali kwwenye ujauzito.

Madhara hakika yanayoambatana na maambukizi ya ugonjwa pangusa ni pamoja na:

  • Mtoto kuzariwa akiwa na uzito mdogo
  • Kujifungua kabla ya muda kuwadia
  • Kondo kupasuka na mimba kutoka

Mtoto wako pia anaweza kupatwa na maambukizi ya pangusa wakati unapojifungua ikiwa kama hujatibiwa maambukizi yakapona. Mtoto mchanga anapozariwa akipatwa na maambukizi ya ugonjwa wa pangusa, yanaweza kusababisha maambukizi machoni na kwenye mapafu.

Maambukizi ya pangusa yaliyopita yanaweza kupelekea baadaye ukawa na matatizo ya uzazi. Maambukizi ya pangusa yamekuwa yakihusika kama mojawapo ya visababishi vya matatizo ya uzazi duniani kote.

Unapopata maambukizi ya pangusa pia kunaweza kukuongezea viahatarishi vya mimba kutunga nje ya kizazi. Hii ni kwasababu maambukizi ya ugonjwa wa pangusa huongeza vihatarishi vya maambukizi katika via vya uzazi(PID) na michubuko kwenye mirija ya uzazi ikiambatana na mimba kutunga nje ya kizazi.

Je, Maambukizi Ya Ugonjwa Wa Pangusa Wakati Wa Ujauzito Yanakuwaje?

Unaweza kuchukua hatua kujikinga wewe mwenyewe pamoja na mtoto wako msiweze kupatwa na maambukizi haya kabla na wakati wa ujauzito wako. Kama ukipata maambukizi, ni vyema ukapata vipimo na kuanza matibabu haraka iwezekanavyo.

Kufanya vipimo na kuanza matibabu ya ugonjwa wa pangusa(au na magonjwa mengine ya zinaa) ni sehemu mojawapo muhimu sana ya kuhakikisha afya ya ujauzito. Hata hivyo, kupima maambukizi kunaweza kuwa kazi ngumu kwasababu wanawake wenye maambukizi ya pangusa huwa mara nyingi huwa hawana dalili.

Wanawake wenye maambukizi ya pangusa ambao wanaonyesha dalili mara nyingi huwa ni hizi:

  • Kutokwa na uchafu mbaya ukeni
  • Kutokwa na damu ukeni baada ya tendo la ndoa
  • Kuhisi miwasho ukeni
  • Kuhisi hali ya kuwaka moto wakati wa kukojoa

Je, Ili Kujua Kwamba Una Maambukizi Haya Unafanyaje?

Kwa kawaida vipimo vya maambukizi haya ni rahisi sana. Mara nyingi kinachohitajika ni sampuli ya mkojo au uteute unaotoka ukeni. Unapaswa kupimwa maambukizi haya mara ya kwanza unapoenda Kliniki. Ikiwa kama tatizo hili litazidi kuwa kubwa, basi itabidi upimwe tena katika miezi mingine inayofuata.

Hivyo ndugu msomaji naomba makala hii naomba iishie hapa, nikaribishe kipindi cha maswali na maoni yako, karibu sana!

Pia unaweza ukatuma namba yako ya WHATsAP tukakuunganisha na GROUP letu uendelee kujifunza maswala ya afya.

Je, Unahitaji Huduma? Basi wasiliana nasi kwa namba hizi: 0752389252 au 0712181626.

Arusha-Mbauda Maua,

 

Karibuni sana!

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *