Je, Ni Kweli Ugonjwa Wa PID Unaweza Kusababisha Mlango Au Shingo Ya Kizazi Kuvimba?

Kuvimba kwa shingo ya kizazi kitaalamu tunaita, “cervicitis”, ambao ni sehemu ya chini, tena nyembamba inayokuwa mwishoni kabisa ndani ya maeneo ya uke wako.

Dalili utakazoziona za kuvimba kwa shingo ya kizazi ni Pamoja na kupata hedhi mara mbili ndani ya mwezi mmoja, maumivu makali wakati unapofanya tendo la ndoa au wakati unapofanya kipimo maeneo ya nyonga, na kutokwa na uchafu usio wa kawaida ukeni. Hata hivyo, inawezekana kuwa na uvimbe kwenye shingo ya kizazi na usione dalili zozote.

Mara nyingi, kuvimba kwa shingo ya kizazi hutokana na maambukizi ya magonjwa ya zinaa, kama vile pangusa au kisonono. Kuvimba kwa shingo ya kizazi kunaweza kusitokane na maambukizi pia. Kupona kwa uvimbe wa shingo ya kizazi kunatokana na kujua chanzo cha uvimbe huo.

Mara nyingi, uvimbe wa shingo ya kizazi hausababishi dalili au ishara, na unaweza kujifunza kuwa una ugonjwa baada ya kufanya vipimo kwa daktari wako wakati anapochunguza matatizo mengine. Kama ukiwa na dalili au ishara, basi zinaweza kuwa Pamoja kama hivi ifuatavyo:

  • Kiwango kikubwa cha uchafu ukeni usiokuwa wa kawaida
  • Kuhisi maumivu mara kwa mara wakati unapokojoa
  • Kuhisi maumivu unaposhiriki tendo la ndoa
  • Kupata hedhi mara mbili ndani ya mwezi mmoja
  • Kutokwa na damu ukeni baada ya kumaliza kufanya tendo la ndoa, na wala sio hedhi

Je, Nini Chanzo Cha Kuvimba Kwa Shingo Ya Kizazi?

Sababu zinazofanya kuvimba kwa mlango au shingo ya kizazi huwa kama hizi zifuatazo:

  • Maambukizi ya magonjwa ya zinaa kama vile kisonono, pangusa, nk
  • Aleji kutokana na matumizi ya kondom, nk
  • Bakteria kuenea kwa wingi ukeni au kwenye kizazi

Je, Madhara Yake Yanakuwa Ni Nini?

Shingo ya kizazi hufanya kazi kama kizuizi ili kuzuia bakteria na virusi wasiweze kuingia kwenye mfuko wako wa uzazi(uterus). Wakati shingo ya kizazi inapoambukiwa na bakteria, huwa kuna hatari kiasi kwamba mambukizi ya bakteria husafiri na kuingia kwenye tumbo lako la uzazi.

Uvimbe wa shingo yakizazi unaosababishwa na kisonono au pangusa unaweza kuenea na kufika kwenye ukuta laini wat umbo la uzazi na kwenye mirija ya uzazi, na kusababisha maambukizi kwenye via vya uzazi(yaani PID), ambayo yanweza kusababisha matatizo ya uzazi ikiwa kama hayatatibiwa haraka.

Leo napenda kuishia hapa katika makala yetu wapendwa, hivyo niwakaribishe katika kipindi cha maswali na maoni. Pia niwakaribishe katika GROUP letu la WHATsAP, hivyo unaweza ukatuma namba yako ukaunganishwa ili ujifunze zaidi mambo ya afya.

Je, Unahitaji Huduma? Basi unaweza kuwasiliana nasi kwa namba hizi: 0752389252 au 0712181626,

Arusha-Mbauda,

Karibuni sana!

 

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *