Neno UTI ni la kiingereza ambalo kirefu chake ni Urinary Tract Infection, yaani maambukizi katika njia au mfumo wa mkojo.
Maambukizi katika njia au mfumo wa mkojo(UTI), huwa ni maambukizi katika sehemu yoyote ya mfumo wako wa mkojo yaani kuanzia figo (kidneys); mirija inayounganisha figo na kibofu cha mkojo(urethers), kibofu cha mkojo (bladder) na urethra; sehemu inayotoa mkojo toka kwenye kibofu cha mkojo hadi nje ya mwili.
NUKUU: Wanawake ndio wako kwenye hatari kubwa ya kupatwa na maambukizi haya kuliko wanaume. Maambukizi yapokuwa kwenye kibofu cha mkojo huwa yenye maumivu makali sana na yanachukiza mno. Hata hivyo matatizo mabaya hujitokeza ikiwa kama maambukizi haya yataenea na kufika kwenye figo zako.
Je, Dalili Zake Zinakuwaje?
Mara nyingi maambukizi katika njia au mfumo wa mkojo huwa hayaonyeshi dalili au ishara, lakini zionekanapo huwa kama ifuatavyo:
- Kuhisi kukojoa mara kwa mara
- Kuhisi maumivu au kuwaka moto wakati wa kukojoa
- Kukojoa mkojo kidogo tu
- Mkojo wenye rangi ya kijivu
- Mkojo ambao huonekana wenye rangi nyekundu, au damu kwenye mkojo
- Mkojo wenye harufu kali
- Maumivu ya nyonga kwa wanawake hasa kwa kwenye maeneo ya nyonga.
NUKUU: Maambukizi katika njia ya mkojo yanaweza yasibainike vizuri katika hali nyingine hasa kwa watu wenye umri mkubwa. Kila aina ya UTI inaweza kujitokeza katika dalili maalumu kutegemeana na sehemu ya njia ya mkojo iliyoathiriwa.
Aina Za Maambukizi Katika Mfumo Wa Mkojo
NUKUU: Kila aina ya maambukizi katika njia au mfumo wa mkojo(UTI) inaweza kuonekana zaidi katika dalili maalumu kutegemeana na sehemu ambapo vimelea wa maambukizi hayo waliposhambulia.
Je, Nini Chanzo Cha Maambukizi Katika Mfumo Au Njia Ya Mkojo(UTI)?
Maambukizi katika njia au mfumo wa mkojo hutokea kwa kufanana wakati bakteria wanapoingia kwenye mfumo wa mkojo kupitia njia ya mkojo na kuanza kuzaliana ndani ya kibofu cha mkojo. Ijapokuwa mfumo wa mkojo umeundwa ili kulinda na kuzuia vimelea wanaovamia, lakini wakati mwingine ulinzi huo hushindwa kufanya kazi yake. Wakati hali hiyo inapojitokeza, bakteria wanaweza kuzaliana na kukua na kushambulia njia ya mkojo.
Hali ya maambukizi kwa kawaida hujitokeza kwa wanawake na kuathiri kibofu na njia ya mkojo.
- Maambukizi Katika Kibofu Cha Mkojo
Aina hii ya maambukizi katika njia ya mkojo mara nyingi husababishwa na bakteria aina ya Escherichia coli (E. coli), aina ya bakteria ambao kwa kawaida hupatikana kwenye njia ya utumbo gastrointestinal (GI).
NUKUU: Tendo la ndoa linaweza kusababisha pia maambukizi haya katika kibofu cha mkojo. Wanawake wote wako katika hatari zaidi ya kupatwa na maambukizi haya kwa sababu ya ukaribu wa njia ya haja kubwa na kijitundu cha kutolea mkojo na kwa sababu ya ufupi wa urethra katika miili yao. ukilinganisha na wanaume.
- Maambukizi Katika Mrija Wa Mkojo(Urethritis)
Aina hii ya UTI inaweza kutokea wakati bakteria wanaokuwa kwenye utumbo wanapoenea kutoka kwenye njia ya haja kubwa mpaka kwenye njia ya mkojo. Pia, kwakuwa njia ya mkojo ya mwanamke iko karibu na uke, hivyo basi maambukizi ya magonjwa ya zinaa kama vile pangusa, kisonono, nk, yanaweza kusababisha kuvimba kwa njia ya mkojo.
Je, Nini Vihatarishi Vya UTI?
Maambukizi katika njia ya mkojo mara nyingi yamekuwa yakiwapata wanawake, na wanawake wengi wamekuwa na maambukizi zaidi ya moja katika maisha yao. Vihatarishi vya maambukizi ya UTI kwa wanawake huwa kama ifuatavyo:
- Mwili Wa Mwanamke
Mwanamke ana njia ya mkojo fupi kuliko ya mwanaume, ambapo bakteria husafiri kwa muda mfupi tu na kufika kwenye kibofu cha mkojo.
- Tendo La Ndoa:
Wanawake wanaofanya tendo la ndoa mara kwa mara huonekana kupatwa na maambukizi ya UTI kwa urahisi kuliko wale wanaokaa muda mrefu bila kushiriki tendo la ndoa.
- Kukoma Hedhi
Baada ya kukoma hedhi, kupungua kwa mzunguko wa vichochezi vya estrogen(estrogen hormone) husababisha mabadiriko katika njia ya mkojo hukufanya kuwa katika hatari zaidi ya kupatwa na maambukizi. Hivyo basi, baadhi ya wanawake wanaofika hatua ya kukoma kwa hedhi mara nyingi hupatwa na maambukizi ya ugonjwa wa UTI. Lakini James Herbal Clinic tunayo tiba nzuri kwa ajili ya kuondoa tatizo hili.
Je, Nini Madhara Ya Ugonjwa Wa UTI?
Tatizo hili linapotibiwa mapema kwa mume na mke, au mtu na mpenzi wake na kwa uhakika, maambukizi hayo huwa hayasababishi madhara tena. Lakini tatizo hili linapokaa muda mrefu bila kutibiwa linaweza kusababisha madhara makubwa kama ifuatavyo:
- Maambukizi kujirudia mara kwa mara yaani mara mbili au zaidi ndani ya miezi 6 au mara nne ndani ya mwaka mmoja
- Figo kuharibika kabisa kutokana na maambukizi haya
- Mwanamke mjamzito kujifungua mtoto mwenye uzito kidogo sana au kujifungua mtoto kabla ya muda kukamilika
- Njia ya mkojo kuwa nyembamba hasa kwa wanaume na hivyo kusababisha mkojo kushindwa kutoka kwa shida
Je, Unawezaje Kujihadhari Na Ugonjwa Huu?
Unaweza kuchukua hatua hizi ili kupunguza vihatarishi vya maambukizi ya UTI:
- Kunywa maji mengi ya kutosha. Mazoea ya kunywa maji mengi husaidia kuufanya mkojo wako kuwa mwepesi na kukuhakikishia kuwa utakojoa mkojo mwingi mara kwa mara ili kuruhusu bakteria kuondolewa kwenye njia yako ya mkojo kabla madhara hayajaanza kujitokeza.
- Mwanamke unapojitawaza au kujipangusa baada ya kukojoa au kujisaidai haja kubwa, kumbuka kupangusa maeneo hayo kuanzia mbele kwenda nyuma. Kwa kufanya hivyo kutakusaidai kuzuia bakteria wanaokuwa sehemu ya njia ya haja kubwa kuingia katika eneo la uke pamoja na njia ya mkojo.
- Hakikisha unaenda kukojoa haraka mara tu unapomaliza kufanya tendo la ndoa na mwenzi wako. Pia kunywa maji angalau glasi 1 ili kusaidia mkojo utoke haraka kwa nguvu.
- Jihadhari sana na vipodozi kama vile powder, marashi, nk usije ukaweka katika maeneo ya uke.
Tiba Zake
James Herbal Clinic tuna tiba nzuri zenye uwezo mkubwa wa kuondoa matatizo ya maambukizi katika njia ya mkojo(UTI) pande zote mbili kwa mwanamke na mwanaume, nazo ni NEOTONIC, FRESH HERB na MULTICURE POWDER
Je, unahitaji huduma? Tupigie 0752389252/0712181626
Arusha-Mbauda
Karibuni sana!
Thanks