Homoni ya progesterone hutengenezwa na mfumo wa uzazi wa mwanamke ambayo hufanya kazi hasa kwa ajili ya kujenga na kurekebisha hali ya ukuta wa ndani wa mfuko wa uzazi(uterus). Homoni ya progesterone huzarishwa na vifuko vya mayai(ovaries), kondo(placenta), pamoja na tezi za adranali.
Ndani ya vifuko vya mayai(ovaries) mahali ambapo homoni ya progesterone huzarishwa huwa kuna tishu(corpus luteum). Hivyo basi, homoni ya progesterone huandaa ukuta wa mfuko wa uzazi(uterus) ili kwamba ngozi laini inayokuwa juu iweze kuwa tayari kupokea yai lililorutubishwa, na kwamba yai linaweza kupachikwa na kuendelea kukua. Pia huzuia misuli ya mfuko wa kizazi isisinyae hali ambayo inaweza kusababisha ukuta wa mfuko wa kizazi ukaashindwa kulipokea yai.
NUKUU: Naomba kina mama mnaosoma makala hii tafadhali zingatia sana na uone maajabu yanayokuwepo pale mimba inapotoka ikiwa bado changa.
Yai lililorutubishwa ambalo hupachikwa ndani ya mfuko wa kizazi(uterus), hutengeneza kondo(placenta). Kondo hili baadaye huzarisha homoni ya progesterone wakati wa ujauzito. Kama yai halijarutubishwa, basi homoni ya progesterone hutengenezwa na vifuko vya mayi(ovaries) siku chache kabla ya hedhi, muda ambao kiwango cha homoni ya progesterone hudondoka vitone vya kutosha vya kutosha ili kuzuia ukuaji wa ukuta wa mfuko wa kizazi na kuufanya uanze kuvuja, na hivyo damu ya hedhi hutoka.
Homoni ya progesterone inaonekana kuwa na athari fulani katika viungo vya wanawake wengine. Katika vifuko vya mayai, homoni ya progesterone na estrogen zinaonekana kuwa zinahusika kwa ajili ya kuachilia yai wakati wa upevushaji wa yai. Inaaminika kwamba, kama yai likirutubishwa, homoni hizi zinafaa sana katika kuzuia yai lingine lisitoke mpaka ujauzito utakapofikia mwisho wake.
NUKUU: Katika mirija ya uzazi, homoni ya progesterone inaonekana kuwa inafanya kazi ya kuzuia misuli ya mirija isiweze kusinyaa mara yai linapokuwa likisafirishwa. Wakati wa ujauzito, homoni ya progesterone pia huamsha ukuaji wa tezi kwenye matiti ambazo huhusika na uzarishaji wa maziwa.
Napenda niishie hapa katika makala hii, itaendelea baadaye…………………………..
Je, Unahitaji huduma? Tupigie kwa namba 0752389252 au 0712181626
Arusha Mbauda