Kwa kawaida unaweza ukabaini tu kuwa hakuna ugonjwa wala maradhi yanayoweza kuendelea usiku kucha. Magonjwa na mardhi mengi husababishwa na uvunjaji wa kanuni za afya, tabia au mienendo mibaya ya ulaji na unywaji, uvutaji sigara au bangi, au kuufanyisha mwili kazi kwa muda mrefu bila kuupumzisha.
Ugonjwa huanza mwilini katika njia zifuatazo:
- Kunakuwa na hali ya kupata mkojo kidogo tu ukiwa wa njano sana, ukiashiria kuwa yawezekana kuna mkusanyiko wa sumu nyingi mwilini mwako.
- Joto la tumboni hushuka na kuwa dhaifu sana. Unakosa hamu ya kula, hivyo ni kiashiria kuwa chakula unachokula huenda hakisagwi vizuri na wakati mwingine kusababisha hali ya kukosa choo, nk.
- Kutokana na sababu mbili nilizozitaja hapo juu, damu kushindwa kuzarishwa kwa kiwango cha kutosha na hivyo hubadirika na kuwa chafu.
- Damu inaposhindwa kupata hewa safi ya oksijeni, basi kabonidioksaidi pamoja na sumu hushindwa kuondolewa katika viungo vya mwili wako.
- Hewa ya kabonidaioksaid pamoja na sumu zinazokuwa zimekusanyika kwenye viungo muhimu vya mwili huizuia nishati ya mwili kuweza kupenya ili kuweza kuvitia nguvu viungo hivyo. Hii ndio maana viungo huendelea kuchoka na kushindwa kufanya kazi na dalili kama vile jasho utaanza kuziona kwenye viganja vya mikono au nyayo za miguu.
- Mkusanyiko wa kabonidioksaidi pamoja na sumu mwilini husababisha viungo vya mwili kuwa dhaifu na kushindwa kufanya kazi kwa ufasaha, hivyo, hupoteza ubora wake na kuongeza hali ya uchovu kwa muhusika.
- Kwa kifupi, mwili wako huwa dhaifu na kuwa rahisi sana kushambuliwa na magonjwa na vimelea mbalimbali.
- Ikiwa kama ugonjwa utadumu kwa muda mrefu, basi huathiri tezi za endocrine na tezi ya kwanza ya endocrine inayosumbuliwa sana huwa ni Thyroid au parathyroid. Kadiri tezi hizi zinavyozidi kuhusika katika utendaji kazi, basi kuharibika kwa tezi moja husababisha pia madhaifu ya tezi zingine kushindwa kufanya kazi vizuri kama ipasavyo. Hii ndio maana ugonjwa unapokaa mwilini muda mrefu bila kutibiwa unaweza kushangaa sehemu zingine za mwili wako zinaanza kuuma au kupatwa na maumivu.
Mwili huhitaji kutoa sumu na vikolombwezo vingine nje pamoja na vimelea wanaosababisha ugonjwa. Vyakula vya matunda kama vile nanasi, matikiti maji, machungwa, pamoja na papai huusaidia mwili wako katika kufanya kazi ya kuondoa sumu na vitu vingine vichafu mwilini mwako.
Unaweza kufanya mazoea ya kula vyakula vya matunda ikiwa kama umeona hali kama hiyo kwa kufunga hata siku 2 tu bila kutumia vyakula vilivyopikwa jikoni. Matunda kama vile nanasi, machungwa au papai husaidia sana kuondoa kabonidaioksaidi pamoja na sumu zilizokusanyika kwenye viungo vya mwili wako kama vile figo, ini, nk, na hivyo kuvifanya viweze kufanya kazi vizuri tena kwa ufasaha.
Kabla Hujaanza Matibabu Je, Huwa Kuna Dalili Au Viashiria Gani Mwilini Mwako?
Kabla hujaanza kufanya matibabu, yakupasa pia kufahamu dalili za mwili wako au ishara zinazojitokeza.
- Yatupasa tuwe makini sana na dalili au ishara zinazojitokeza katika miili yetu kama vile kiu, njaa, kukojoa, nk.
- Mwili pia hutupatia ishara au dalili katika muonekano wa kucheua hasa wakati tumbo linapokuwa limejaa. Utaona sauti ya kwanza, inafuatia na ya pili na ya tatu pia.
- Maumivu au vichomi katika sehemu yoyote ya mwili wako huonyesha hali ya kujaa kwa kabonidaioksaidi, maji, hewa, nk.
- Hali ya mafua mepesi na kukoroma humaanisha kuwa mwili unajitahidi kuyatoa nje majimaji yanayozidi mwilini.
- Hali ya kikohozi huashiria kuwa:
- Mwili unajisikia kuwa wa baridi na kwamba
- Unajaribu kuondoa na safisha uchafu kutoka kwenye koo pamoja na kifuani.
- Hali ya muwasho huonyesha kwamba kunahitajika mtiririko mkubwa wa damu maeneo hayo.
- Hali ya homa huashiria pambano lililoko mwilini mwako, yaani chembe hai nyeupe za damu zinakuwa na pambano kubwa dhidi ya vimelea au ugonjwa.
- Hali ya kuhisi kujinyoosha nyoosha na kupiga miaye huashiria kuwa mwili wako umechoka na unahitaji mapumziko na uweze kupata hewa ya oksijeni.
- Hali ya kukosa hamu ya kula huashiria kuwa kuna hali ya chakula kutokusagwa vizuri tumboni au kukosa choo, na kwamba tumbo pamoja na viungo vingine vinavyohusika na umeng’enyaji vinakuwa na kazi kubwa sana katika kuondosha hali ya chakula kutokusagwa pamoja na kukosa choo au mwili kujishughulisha sana kuliko kawaida katika kupambana na ugonjwa. Uonapo hali kama hii ni vyema ukatumia maji vuguvugu na juisi ya matunda hasa papai itaweza kukusaidia kuondokana na tatizo hili kuliko kushindilia vyakula.
Yafaa sana tuzifahamu ishara hizi za miili yetu na kujaribu kuisaidia ili ijiepushe na magonjwa wala tusithubutu kuzizuia ghafla kwa kutumia madawa yoyote ya vidonge, kwa mfano; unapozuia ghafla hali ya homa kwa kutumia kidonge mara nyingi hujitokeza tena katika ugonjwa mwingine na hata kupooza.
Je, unahitaji tiba ya kuondokana na matatizo haya? James Herbal Clinic tuna dawa nzuri ambayo itakusaidia kujitibu vizuri kabisa.
Kwa mawasiliano tupigie: 0752389252 au 0712181626