JE, UNAJUA CHANZO CHA KUTOKWA NA DAMU YENYE UTELEZI KAMA MAKAMASI UKENI(BLOODY MUCUS)?

 

Je, unatokwa na damu  yenye makamasikamasi au utelezi kabla ya hedhi yako na wakati mwingine ukawa na mashaka kuwa huenda kuwa ni ujauzito?

 

 

Damu yenye utelezi inapotoka kidogo maana yake ni uchafu unaotoka ukeni ukiwa na mchanganyiko na damu kutokana na hali ya ujauzito, upevushaji mayai au sababu zingine. Makala hii leo napenda nielezee visababishi vya kutokwa na damu yenye utelezi na jinsi gani inavyoweza kukutia mashaka au wasiwasi.

Je, Uchafu Wa Kawaida Unakuwaje Na Kwanini Unakuwa Wa Kahawia?

Uchafu wa kawaida unaotoka ukeni huwa umetengenezwa na aina tofauti tofauti za seli pamoja na ute kutoka kwenye shingo ya kizazi. Uchafu wa ukeni unakuwa umetengenezwa na seli aina ya epithelial, ute utokao kwenye shingo ya kizazi, bakteria wa asili wanaokuwa kwenye uke pamoja na viumbe hai wengine.

 

Kwanini Uchafu(Utoko) Wa Ukeni Unaonekana Kuwa Wa Muhimu Sana?

Uchafu utokao ukeni ni wa muhimu kwasababu unasaidia kuzuia maambukizi ukeni. Uke kwa kawaida una bakteria wa asili wajulikanao kwa jila la Lactobacillus ambao husaidia kuuweka uke katika hali ya asidi au uchachuchachu fulani. Uke unaokuwa na hali ya uchachu huzuia maambukizi kwa urahisi.

Je, Utoko Au Uchafu Wa Kawaida Unaotoka Ukeni Unakuwa Wa Rangi Gani?

 

Utoko ama uchafu unapaswa kuwa wa njano, mweupe au wa kahawia. Baadaye tutajifunza jinsi uchafu wa njano au mweupe unavyokuwa katika makala nyingine.

 

Je, Nini Kinasababisha Kutokwa Na Damu Yenye Utelezi Kama Makamasi?

Ikiwa kama una hali ya kutokwa na uchafu ukeni wenye damu kama makamasi, basi vifuatavyo hapo chini ndivyo vyanzo vya ishara unavyopaswa kuvitambua:

 

1. Ujauzito

 

Ikiwa kama una ujauzito, basi kutokwa na damu yenye utelezi kama makamasi huwa ni ishara ya awali kabisa. Hii ni kwasababu ya mgandamizo wa damu baada ya kiumbe kuanza kuumbika tumboni.

Je, Nini Maana Ya Mgandamizo Wa Damu?

 

Baada ya tendo la ndoa katika siku za hatari, huwa kuna nafasi kubwa mno ya kupata ujauzito. Ikiwa kama mbegu zitarutubisha yai, basi ndipo kiinite hutengenezwa.  Kiinitete  hubebwa na kusafirishwa kwenda kwenye kifuko cha uzazi(uterus) ambapo hupandikizwa ama kupachikwa kwenye ukuta wa mfumko wa kizazi(uterus) ambao kitaalamu hujulikana kama endometrium.

Endapo kama hali hii ya mgandamizo itatokea, basi huwa kuna kunatokea hali ya kutokwa na damu kidogo kutoka kwenye ukuta wa mfuko wa kizazi(endometrium) ambayo huchangamana na utoko au uchafu na kuwa kama damu yenye utelezi kama makamasi vile.

 

Je, Unawezaje Kutambua Kuwa Uchafu Huo Wenye Damu Yenye Utelezi Kuwa Unatokana Na Uoteshaji Ama Mpachiko Wa Kiinitete Kwenye Mfuko Wako Wa  Kizazi?

 

Damu yenye utelezi hutoka kwasababu ya hali ya mpachiko au uoteshaji (implantation) kutokea katika siku kadhaa au wiki kabla ya mzunguko wako wa hedhi. Ikiwa kama ulikuwa unapata mzunguko wa hedhi mapema sana ama kutokwa na damu kabla ya mzunguko wako wa hedhi kufika baada ya kufanya tendo la ndoa bila kutumia kinga, basi tambua kuwa hali hiyo ni ya ujauzito.

 

Je, Dalili Zingine Za Ujauzito Zikoje?

Kwa kawaida dalili zingine za ujauzito huwa kama ifuatavyo:

  • Mwili kuchoka
  • Ladha au harufu ya vyakula ama vinywaji kubadirika
  • Kuchoka kwa urahisi sana
  • Hali ya vichomi au maumivu tumboni
  • Matiti kuvimba na kuuma.

 

Je, Unaweza Kupata Wapi Vipimo Ili Kuthibitisha Kuwa Ni Ujauzito?

 

Kama una hali ya kutokwa damu yenye utelezi kama makasi vile kabla ya hedhi, basi hiyo ni ishara ya ujauzito. Kipimo cha ujauzito kinachofanyika wakati unapoona damu kidogokidogo ikitoka, chaweza kuwa hasi. Hii ni kwasababu kiwango cha kichochezi(hormone) au HCG kinachozarishwa na kondo la nyuma(placenta) baada ya kupachikwa kwa kiinitete, kitashuka sana wakati wa upachikaji(implantation).

 

Je, Nini Cha Kufanya?

Nakushauri usibiri wiki moja ipite halafu pata kipimo cha ujauzito.

2. Upevushaji Wa Yai

 

Wakati wa upevushaji, baadhi ya wanawake wanweza kupatwa na hali ya kutokwa na damu yenye utelezi kutoka ukeni mwao. Hali hii hutokana na mpasuko(rupture) wa kifuko cha yai huku kikitokwa na damu kidogo kidogo. Kutokana na upevushaji, damu hii inapochanganyikana na utoko ama uchafu wako wa ukeni, basi uchafu unakuwa wenye damu.

 

Je, Nini Maana Ya Upevushaji?

 

Upevushaji ni hali ya kuachiliwa kwa yai kutoka kwenye ovari baada ya mkomao au  mpasuko wa mfuko wa yai. Yai hili linaporutubishwa na mbegu za mwanaume hukufanya wewe mwanamke kuwa mjamzito.

 

Je, Hali Ya Upevushaji Huanzaje Na Jinsi Gani Unaweza Kuitambua?

Hali ya kutokwa na uchafu wenye damu yenye utelezi kipindi cha upevushaji hutokea majuma 2 kabla au baada ya kipindi chako cha hedhi kukoma. Dalili za kipindi cha upevushaji wa yai huwa ni kutokwa na majimaji meupe yenye kulendemka kama ute wa yai la kuku, vichomi katika tumbo la chini, kuongezeka kwa hamu ya tendo la ndoa na matiti kuuma.

 

Je, Wakati Wa Tendo La Ndoa Inakuwaje?

Hali ya tendo la ndoa inaweza kusababisha uke kuchubuka. Hali hii inaweza kusababisha kutokwa na damu ambayo huchanganyakana na uchafu wako na kuwa wa kahawia au wenye damu.

 

Je, Unaweza Kuwa Na Mashaka Kutokana Na Damu Yenye Utelezi Kukutoka Kwasababu Ya Kufanya Tendo La Ndoa?

 

La hasha! Kutokana na kufanya tendo la ndoa, damu yenye utelezi inapojitokeza hukoma ndani ya masaa au siku chache tu. Ikiwa kama utaona damu nyeusi inatoka baada ya kufanya tendo la ndoa, basi itakuwa ni dalili za uvimbe kwenye mfuko wa kizazi(uterus) kama vile Fibroids. Kwa hali hii usichelewe kabisa. Yafaa sasa ufike hospitali ili kufanya uchunguzi wa vipimo.

3. Maambukizi Katika Sehemu Za Siri Za Mwanamke

 

Je, una hali ya kutokwa na harufu mbaya ukeni? Je, unatokwa na uchafu wenye harufu mbaya? Je, unawashwa sehemu za siri pamoja na maumivu wakati wa tendo la ndoa? Uonapo hali au dalili kama hizo, basi ni rahisi sana kutokwa na damu yenye utelezi kutokana na maambukizi.

 

Maambukizi katika sehemu za uke yanaweza kusababisha kutokwa na damu ya hedhi mara mbili ndani ya mwezi. Maambukizi ambayo unaweza kuyapata ni haya:

 

  • Pangusa (Chlamydia)
  • Kisonono
  • Maambukizi ya fangasi
  • Maambukizi katika via vya uzazi au PID
  • Malengelenge(Trichomoniasis)

 

Je, Nini Cha Kufanya?

 Unapaswa ufike hospitali za wilaya au mkoa haraka sana ili kufanya uchunguzi kupitia vipimo.

4. Uzazi Wa Mpango

 

Ikiwa kama unatumia vidonge vya uzazi wa mpango au ndio umeanza kutumia dawa za kuzuia ujauzito, basi yaweza kuwa sababu ya kutokwa na uchafu wenye damu ya utelezi. Hakuna haja ya kuwa na mashaka sana kwasababu damu inayosababishwa na vidonge vya uzazi wa mpango inaweza kukoma baada ya miezi kadhaa. Hata hivyo ikiwa hali hiyo itaendelea, basi unapaswa umuone daktari wako.

5. Saratani Ya Ukuta Wa Kizazi

 

Je, una zaidi ya umri wa miaka 40 huku ukitokwa na uchafu wenye damu yenye utelezi? Basi yaweza kuwa ni kwasababu ya ugonjwa wa saratani ya ukuta wa kizazi. Na ieleweke kuwa saratani ya ukuta wa kizazi ni hali ya kuvimba  kwa ukuta wa mfuko wa kizazi. Hali hii hutokana na athari ya vichochezi vya estrogen katika ukuta wa mfuko wa kizazi.

Hali yoyote inayoendelea kwa mwanamke ya kutokwa na damu huku akiwa amefikisha umri wa kukoma hedhi(menopause), huwa ni ishara mbaya na uonapo hivyo unapaswa ufike hospitali mapema mno bila kuchelewa ili kupima saratani.

 

Sababu 9 Zinaoweza Kukutia Wasiwasi Kwanini Utokwe Na Damu Yenye Utelezi?

 

Zifuatazo ni sababu zinazoweza kukuweka katika hali ya mashaka kwanini utokwe na damu yenye utelezi:

 

  1. Damu yako inaweza kuendelea kutoka mara kwa mara huku ikiwa na utelezi
  2. Kipindi chako cha hedhi kukaa muda mrefu kuliko kawaida
  3. Kutokwa na damu nyeusi wakati wa hedhi.
  4. Kuhisi maumivu makali wakati wa hedhi
  5. Uke wako kutokwa na harufu
  6. Kuhisi hali ya muwasho sehemu za uke
  7. Kuhisi maumivu wakati wa tendo la ndoa
  8. Kutokwa na damu muda mrefu ikiwa kama ulipitiliza au kushindwa kupata hedhi katika mwezi au miezi iliyopita. Hii inaweza kuwa ishara au dalili ya kuporomoka kwa mimba.
  9. Hali ya homa na kuhisi maumivu katika tumbo lako la chini.

 

Ndugu mpendwa msomaji, haya ndio maswali ambayo yamekuwa yakiulizwa na watu mbalimbali kuhusu kutokwa na uchafu wenye damu yenye utelezi. Bila shaka majibu ndio hayo hapo juu kama unavyoona.

James Herbal Clinic tunatiba za tatizo hili tena kwa uhakika. Ikiwa kama unahitaji huduma tafadhari tupigie kwa namba hizi: 0752389252 au 0712181626

 

Karibuni sana.