JE, UNAJUA CHANZO NA DALILI ZA KUZIBA KWA MIRIJA YA UZAZI? JE, NINI MADHARA YAKE IKIWA KAMA HAITAZIBULIWA?

Mirija ya uzazi ambayo pia kitaalamu hujulikana kama “Uterine tubes”huwa ni mirija miwili inayokuwa pande mbili za mfuko wa kizazi(uterus) ambayo hubeba yai lililokomaa kutoka kwenye kifuko cha yai(ovary) na kulisafirisha kwenda kwenye mfuko wa kizazi(uterus). Mirija ya uzazi pia hubeba mbegu za mwanaume zinazokuwa zikiogelea kwenye shingo ya kizazi na kuzisafirisha ili ziweze kukutana na yai la mwanamke.

NUKUU: Mirija ya uzazi huwa ina tishu ndogondogo ambazo kitaalamu hujulikana kama “ciliated epithelia” ambazo hueleaelea kwenda mbele na kurudi nyuma ili kulisaidia yai liweze kutoka kwenye kifuko cha yai(ovary) kila mwezi na kuingia kwenye mfuko wa kizazi(uterus). Tishu hizi zenye muonekano kama vinyweleo fulani pia husaidia yai lililorutubishwa liweze kusafiri na kuingia kwenye mirija ya uzazi mpaka kwenye mfuko wa kizazi(uterus). Kovu lolote au mchubuko unaokuwa kwenye mirija ya uzazi unaweza kusababisha hali ya kuziba kwa mrija ambayo huathiri uwezo wa kuzaa wa mwanamke.

 

Je, Dalili Za Kuziba Kwa Mirija Ya Uzazi Zinakuwaje?

 

Kuziba kwa mirija ya uzazi ni hali ambayo huonyesha dalili zake kwa nadra sana. Wanawake wengi hushindwa hata kutambua kuwa wana tatizo la kuziba kwa mirija ya uzazi mpaka pale wanapokuwa wakijaribu kutafuta ujauzito lakini wasiupate. Hata hivyo katika baadhi ya wanawake hali hii inaweza ikaonyesha dalili zifuatazo:

  • Maumivu makali wakati wa hedhi
  • Maumivu makali wakati wa tendo la ndoa
  • Maumivu wakati wa kukojoa
  • Kutokwa na uchafu ukeni,
  • Mirija ya uzazi kuvimba na kujaa majimaji
  • Maumivu makali chini ya kitovu
  • Maumivu ya nyonga, nk.

 

Je, Nini Husababisha Mirija Ya Uzazi Kuziba?

 

 

Sababu zinazopelekea mirija ya uzazi kuziba huwa kama ifuatavyo:

 

  • Magonjwa ya maambukizi katika via vya uzazi au PID.
  • Magonjwa ya zinaa kama vile pangusa(Chlamydia), kisonono, nk
  • Michubuko au majeraha kwenye mirija ya uzazi kutokana na upasuaji, nk
  • Mimba kutunga nje ya kizazi na kusababisha upasuaji hali ambayo hupelekea michubuko
  • Hali ya kukua kwa uvimbe aina ya fibroid ambayo hupelekea kuziba nafasi ya mirija ya uzazi
  • Mkusanyiko wa usaha au uchafu kutokana na maambukizi ya magonjwa kwenye mirija ya uzazi.

 

 

Je, Mwanamke Anaweza Kuendelea Kupata Hedhi Hata Kama Mirija Ya Uzazi Imeziba?

 

Hali ya kuziba kwa mirija ya uzazi kwa kawaida huwa haiathiri vipindi vya hedhi wala mzunguko wa hedhi zaidi ya kujitokeza baadhi ya maumivu au kukosa furaha.  Hata kama mirija yote miwili ikiwa imeziba, lakini haiwezi kuathiri vipindi vya hedhi. Hata hivyo, magonjwa ambayo husababisha mirija kuziba yanaweza kuathiri vifuko vya mayai pamoja na ukuta wa mfuko wa kizazi, na kwa hali hii, vipindi vya hedhi lazima vibadirike badirike au kutokwa na damu nyingi sana wakati wa hedhi.

 

Je, Unaweza Kuendelea Kupata Ujauzito Huku Ukiwa Na Hali Ya Kuziba Kwa Mirija Ya Uzazi?

 

 

Mirija inapoziba huzuia mwanamke asipate ujauzito kwakuwa huzizuia mbegu za mwanaume zisiweze kulifikia yai la mwanamke, na vile vile hulizuia yai lililorutubishwa lisiweze kufika kwenye mji wa mimba. Upasuaji unaweza ukafanyika ili kuondoa hali ya kuziba, lakini njia hii ya tiba sio ya maana sana kwakuwa inaweza ikasababisha mimba kutunga nje ya kizazi(ectopic pregnancy).  Yafaa sana ukapata tiba za asili ili kuondoa kabisa vyanzo au visababishi na kukuwezesha kupata ujauzito.

 

Tiba Zake

 

James Herbal Clinic tunapenda kuwashauri wapendwa kwamba, ikiwa kama unasumbuliwa na tatizo hili, tafadhari pata tiba zetu nzuri za asili zenye uwezo wa kuondoa vyanzo vya tatizo hili, nazo ni MULTICURE POWDER, FRESH HER na VITAMAKA.

 

Je, unahitaji huduma? Tupigie kwa namba hizi: 0752389252 au 0712181626

 

Arusha-Mbauda

 

 

Karibu sana