Vifuko vya mayai hutengeneza mfumo wa uzazi wa mwanamke. Kila mwanamke ana vifuko vya mayai viwili. Vifuko hivi vina umbo la yai, lenye sentimita nne kwa urefu, na hulala kwa upande wa tumbo la uzazi pembeni mwa ukuta wa nyonga.
NUKUU: Na ieleweke kuwa vifuko vya mayai huwa vimeshikiliwa sehemu moja na kano zilizoko kwenye tumbo la uzazi lakini havijashikamanishwa kabisa kwenye mirija ya uzazi.
Je, Vifuko Vya Mayai Vina Kazi Gani?
Vifuko vya mayai vina kazi kuu mbili za uzazi ndani ya mwili wa mwanamke, ambazo ni:
- Kuzarisha mayai kwa ajili ya urutubishaji
- Kuzarisha homoni za estrogen na progesterone.
Kazi ya vifuko vya mayai huendeshwa na homoni za gonadotrophin zinazoachia homoni kutoka kwenye neva za seli ndani ya sehemu ya ubongo ambayo ni hypothalamus ambayo hutuma ujumbe wa vifuko hivi kwenye tezi ya pituitary ili kutengeneza homoni kwa ajili ya kupevusha mayai pamoja na homoni ya kuchochea au kuamsha hisia.
Kazi zote hizi hufanyika kupitia mkondo wa damu ili kuendesha mzunguko wa hedhi. Vifuko vya mayai huachilia yai katikati ya kila mzunguko wa hedhi. Mara nyingi, yai moja tu kutoka kwenye kifuko kimoja huachiliwa wakati wa kila kipindi cha mzunguko wa hedhi.
NUKUU: Kumbuka kuwa mtoto wa kike huzariwa akiwa na mayai yote atakayokuwa nayo daima. Na inakadiriwa kuwa anaweza kuwa na mayai milioni 2, lakini inafika kipindi fulani msichana anavunja ungo, na hivyo idadi hiyo ya mayai hupungua na kufikia mayai 400,000 yakiwa yamehifadhiwa kwenye vifuko vya mayai. Kutoka kwenye kipindi cha kuvunja ungo mpaka kufikia kipindi cha kukoma hedhi, huwa ni mayai 400-500 yanayokuwa yamekwisha kukomaa, na kutolewa kabisa kwenye kifuko cha mayai(kwa njia ambayo tunaita upevushaji), na kuwa yapo tayari kabisa kurutubishwa kwenye mirija ya uzazi au tumbo la uzazi.
NUKUU: Katika kifuko(ovary), mayai yote hufungamanishwa kwa pamoja kwenye tabaka moja la seli lijukanalo kama follicle, ambalo husaidia yai kulilinda. Muda huo, mayai hayo huanza kukomaa ili kwamba moja liweze kuachiliwa litoke kwenye kifuko cha yai katika kila mzunguko wa hedhi. Yai linapokomaa, basi seli zinazokuwa kwenye follicle hugawanyika kwa kasi na hivyo, follicle huendelea kuwa kubwa. Follicle nyingi hupoteza uwezo wake wa kufanya kazi wakati kazi hii inapokuwa ikifanyika, ambayo inaweza kuchukua miezi kadhaa, lakini follicle moja huweza kufanya kazi katika kila mzunguko wa hedhi na yai linalokuwa imelibeba huachiliwa wakati kazi ya upevushaji imeshakamilika.
Kadiri Follicle zinavyozidi kuendelea kufanya kazi, ndipo huzidi kuzarisha homoni ya estrogen. Yai linapokuwa limeachiliwa wakati wa upevushaji, follicle inayokuwa tupu inayobakia kwenye kifuko cha yai(ovary), huwa tunaiita , “Corpus luteum”. Hii baadaye huachia homoni ya progesterone kwa kiwango kikubwa na estrogen kwa kiwango kidogo tu.
NUKUU: Homoni hizi huandaa ukuta wa tumbo la uzazi(uterus) kwa ajili ya ujauzito(ikiwa kama yai lililoachiliwa likiwa limesharutubishwa). Kama yai lililoachiliwa halijarutubishwa na ujauzito haujaonekana wakati wa mzunguko wa hedhi, basi corpus luteum huharibika na hivyo uzarishaji wa homoni ya estrogen na progesterone hukoma. Kwakuwa homoni hizi zinakuwa hazipatikani kabisa, ukuta wa tumbo la kizazi huanza kuanguka na kuondolewa kutoka mwilini kupitia hedhi. Baada ya hedhi, ndipo mzunguko mwingine huanza.
Hali ya kukoma hedhi huja baada ya umri wa mwanamke kufikia ukomo wa kuzaa. Hali hii husababishwa na kupotea kwa follicles zote zinazobaki kwenye kifuko cha yai kinachokuwa na mayai. Kunapokuwa hakuna follicles nyingi au mayai, kifuko cha yai huwa hakiwezi kabisa kutengeneza homoni ya estrogen na progesterone, ambazo hurekebisha mzunguko wa hedhi, na matokeo yake hedhi hukoma.
Je, Vifuko Vya Mayai Huzarisha Homoni Gani?
Homoni kuu zinazozarishwa na vifuko vya mayai ni estrogen na progesterone, ambazo zote huwa ni muhimu katika mzunguko wa hedhi. Uzarishaji wa homoni ya estrogen hufanyika katika nusu ya mzunguko wa hedhi kabla ya upevushaji, na uzarishaji wa progesterone hufanyika wakati nusu ya pili ya mzunguko wa hedhi wakati corpus luteum imeshajijenga. Homoni zote hizi huwa ni za muhimu katika uandaaji wa ukuta wa tumbo la mji wa mimba kwa ajili ya ujauzito na upachikaji wa yai lililorutubishwa, au kiinitete.
Je, Kitu Gani Kinaweza Kuharibu Vifuko Vya mayai Ya Mwanamke?
Na ieleweke kuwa, madawa yoyote ambayo huzuia vifuko vya mayai visiweze kufanya kazi vizuri, yanaweza kupunguza uwezo wa mwanamke kupata ujauzito, na wakati mwingine yaweza kumfanya kuwa mgumba.
NUKUU: Vifuko vya mayai hukoma kufanya kazi wakati wa kipindi cha kukoma hedhi. Hali hii hutokea kwa wanawake wengi wenye umri wa miaka 50. Hali hii kama ikijitokeza mapema, kabla ya kufikisha umri wa miaka 40, ndipo hujulikana kuwa mayai hayakomai au machanga au kutokuwa na mayai kabisa.
Je, Ni Magonjwa Gani Yanayojitokeza Kwenye Vifuko Vya Mayai?
Maradhi au magonjwa ya kawaida yanayojitokeza kwenye vifuko vya mayai huwa ni vivimbe vidogovidogo(Polycstic Ovary Syndrome), ambavyo huathiri asilimia 5-10% ya wanawake walio katika umri wa kuzaa. Katika vivimbe vya vifuko vya mayai, follicles hukomaa katika hatua fulani, lakini baadaye hukoma kukua na hushindwa kuachia yai. Follicles hizi huonekana kama uvimbe kwenye vifuko vya mayai mara vinapopimwa kwenye kipimo cha ultrasound.
NUKUU: Tatizo lolote linalojitokeza kwenye vifuko vya mayai humfanya mwanamke ashindwe kupata ujauzito na hivyo kuwa mgumba. Mwanamke kama akikoma kupata vipindi vyake vya hedhi katika umri wake wa kuzaa, hali hii kitalaamu huitwa, “amenorrhoea”. Ni hali inayoweza kusababishwa na mambo mengi kama ifuatavyo:
- Kufanya mazoezi kuzidi kiwango
- Msongo wa mawazo
- Tezi ya pituitary kufanya kazi kuliko uwezo wake
- Uzito wa mwili kuwa mkubwa, nk.
Tiba Zake
James &Ferdinand Herbal Clinic tuna dawa nzuri kabisa zenye uwezo wa kuondoa tatizo hili, nazo ni REDEEMER, CARD HERB na VITAMAKA.
Je, unahitaji Huduma? Basi tupigie 0752389252 au 0712181626.
Mbauda Arusha.
Karibu sana