Mbegu za mwanaume zinapokuwa chache maana yake ni kwamba uteute(manii) ule unaoutoa wakati unapofika kileleni huwa unakuwa na mbegu chache kuliko kawaida.
Mbegu chache za mwanaume kitaalamu huitwa “oligospermia”, bila shaka unapoenda hata kupima au kufanya uchunguzi juu ya tatizo hili, utaona kwenye kadi yako yameandikwa maneno kama hayo. Lakini pia kuwapo kwa mbegu kamili za mwanaume huwa kuna sifa zake, ambazo nazo kitaalamu huitwa, “azoospermia.” Hata kama unafanya vipimo ili kujua afya yako juu ya uwezo wa mbegu zako za kiume, utaona kadi yako imeandikwa majibu kama hayo.
NUKUU: Idadi ya mbegu zako zinaweza kukadiriwa kuwa chache kuliko kawaida ikiwa kama zitakuwa mbegu milioni 15 kwa kiwango cha milimita za manii. Kuwa na kiwango cha mbegu chache hupunguza uwezo wa mbegu zako kuweza kurutubisha yai la mwanamke. Licha ya hayo yote, lakini pia wanaume wengi wenye tatizo la kuwa na mbegu chache bado tu wana uwezo wa kumpa mwanamke ujauzito lakini kwa shida sana. Hivyo yafaa kupata tiba na hivyo kurekebisha mfumo wako wa ulaji.
Je, Dalili Zake Zinakuwaje?
Dalili kubwa ya kuwa na mbegu chache ni kutompa mwanamke ujauzito. Kunaweza kusiwepo dalili zingine zaidi zilizo wazi. Kwa upande mwingine, matatizo mengine kama vile kutokuwa na uwiano sawa wa homoni au vichochezi, kuvimba kwa mishipa ya korodani au hali ambayo inaweza kuziba njia ya uwezo wa mbegu kupita, inaweza kusababisha dalili au ishara za tatizo hili. Dalili za kuwa na mbegu chache mojawapo ni;
- Maumivu, au uvimbe kwenye korodani
- Kupungua uwezo wa vichochezi au homoni mwilini.
- Kutokuwa na uwezo wa nguvu za kiume, kwa mfano kufika kileleni mapema au kushindwa kabisa kudindisha.
Ushauri
Ninakushauri umuone daktari ikiwa kama huna uwezo wa kumpa mwanamke ujauzito baada ya kuishi naye mwaka mmoja baada ya harusi, au ikiwa kama una mambo kama yafuatayo:
- Kushindwa kudindisha au kufika kileleni
- Kushindwa kufanya tendo la ndoa
- Kuhisi maumivu au kuwa na uvimbe kwenye korodani
- Matatizo ya tezi dume
- Shahawa kuwa nyepesi na hivyo kurudi nyuma baada ya tendo la ndoa
Je, Chanzo Chake Ni Nini?
Uzarishaji wa mbegu huwa ni mchakato uliochangamana na unahitaji utendaji kazi wa kawaida wa korodani pamoja na tezi za hypothalamus na pituitary, viungo vinavyokuwa kwenye ubongo wako ambavyo hutoa vichochezi au homoni ambazo husababisha utengenezaji wa mbegu.
NUKUU: Mbegu zinapozarishwa kwenye korodani, basi mirija laini huzisafirisha mpaka zinachangamana na manii(semen) na ndipo humwagwa nje kupitia uume mara tu mwanaume anapofika kileleni. Matatizo yoyote yanayojitokeza katika mifumo hii yanaweza kuathiri uzarishaji wa mbegu.
Chanzo cha tatizo hili kinaweza kutokana na mambo kama yafuatayo:
- Kuvimba kwa mishipa inayosafisha mbegu za mwanaume
- Maambukizi ya magonjwa ya zinaa kama vile kisonono, nk
- Ugonjwa wa kisukari
- Matatizo ya mgongo kutokana na ajali
- Matatizo ya saratani kwenye tezi za pituitary
- Kutokuwa na uwiano sawa wa vichochezi(hormonal imbalance)
NUKUU: Na ieleweke kuwa, pia kunaweza kukawa na matatizo yasiyo ya kawaida juu ya muonekano wa mbegu za mwanaume(morphology), jinsi mbegu zinavyosafiri(motility) au utendaji kazi wake. Hivyo basi, ikiwa kama unahitaji kuhakiki na kuondoa tatizo hili, tunakushauri ufike hospitali mapema ili kuweza kupata uchunguzi wa kina.
Je, Madhara Yake Yanakuwaje?
Kwa kawaida madhara ya tatizo hili huwa kama ifuatavyo:
- Kupatwa na msongo wa mawazo kwa muhusika pamoja na mwenzi wake
- Huvunja heshima ndani ya ndoa na hata kusababisha ndoa kuvunjika
Tiba Zake
James & Ferdinand Herbal Clinic tuna tiba nzuri zenye uwezo mkubwa wa kuondoa matatizo ya mbegu kuwa chache au kudhoofika katika mfumo wa uzazi wa mwanaume, nazo ni VITAMAKA, CARD HERB, ASALI YA NYUKI WADOGO pamoja na NEOTONIC.
Je, Unahitaji Kupata Huduma Za Tiba? Tupigie kwa namba hizi: 0752389252/0712181626
Arusha Mbauda
Karibuni sana
Nahitaji huduma hii