Je, Mirija Ya Uzazi Kujaa Maji Ni NINI?
Hali ya kujaa maji kwa mirija ya uzazi ya wanawake huitwa hydrosalpinx kwa kitaalamu. Ni tatizo ambalo hujitokeza kwa wanawake kutokana na maambukizi ya magonjwa ya zinaa yasiyotibiwa (pelvic inflammatory disease). Mara nyingi husababisha tatizo la ugumba na maumivu ya kiuno.
Mirija ya uzazi hujishikiza kwenye upande wa kulia na kushoto wa tumbo la uzazi, hupitisha mayai kila mwezi kutoka kwenye ovari kwenda kwenye mji wa uzazi. Urutubishaji wa yai la uzazi hutokea katika mirija hii.
Je, Nini Husababisha Mirija Kujaa Maji?
Mara nyingi mirija ya uzazi kuziba hutokana na mambo yafuatayo:
- Maambukizi ya magonjwa ya zinaa ambayo hayakutibiwa kama vile kisonono na klamidia au PID(Pelvic inflammatory disease).
- TB ya mirija ya uzazi
- Upasuaji maeneo ya kiunoni (pelvic surgery)
- Endometriosis
- Maambukizi ya apendiksi (appendicitis)
- Saratani ya mirija ya uzazi
Dalili Zake
Kwa kawaida wanawake wengi wanaweza wasiwe na dalili zozote, isipokuwa kupata matatizo katika kupata mtoto. Dalili zinazojitokeza mara nyingi huwa ni;
- Maumivu ya kiuno ambayo hujitokeza mara kwa mara hasa siku chache kabla au baada ya kuingia kwenye hedhi.
- Uchafu kutoka sehemu za siri
- Maumivu wakati wa tendo la ndoa
- Kutokuwa na hamu ya tendo la ndoa
- Kutokubeba ujauzito
Je, Unawezaje Kuligundua Tatizo Hili?
Kuna vipimo kadhaa vya kuwezesha kujua kama mirija yako ya uzazi imeziba na kujaa maji navyo ni:
- Hysterosalpingogram, hii ni aina maalumu ya X-ray ya kiuno, ambayo kimiminika maalumu huingizwa ndani ya mji wa uzazi kwa kupitia shingo ya uzazi. Kama mirija haijaziba, kimiminika huweza kupita mpaka ndani ya kiuno na kama imeziba haitaweza kupita. Hii itaonekana kwenye hiyohysterosalpingogram.
- Ultrasound ya kiunoni (Pelvic Ultrasound), hii itaweza kuonesha kama mirija yako imeziba na kujaa maji, na ukubwa wake. Pia itaweza kuonesha kama kuna matatizo mengine kwenye via vya uzazi vya ndani.
- Upasuaji wa Tumbo(Laparoscopy), huu hufanyika kwa kutumia mirija maalumu yenye kamera ili kutazama mirija hiyo. Matundu mawili hutobolewa tumboni ili kupitisha mirija hii.
Je, Naweza Kupata Mtoto?
Tatizo hili likitibiwa unaweza ukapata mtoto. Pale mirija inapokuwa imeharibika sana uwezekano wa kupata ujauzito huwa ni mdogo sana. Njia nyingine saidizi kama In Vitro Fertilization zinaweza kutumika.
Je, Nini Madhara Ya Tatizo Hili?
Mirija ya uzazi ikiziba, mayai ya uzazi hushindwa kusafiri kutoka kwenye ovari kwenda kwenye mji wa uzazi. Hivyo hujitokeza matatizo yafuatayo:
- Ugumba
- Mimba kutunga nje ya mfuko wa mimba (Ectopic pregnancy)
- Maumivu ya kiuno
- Kusinyaa kwa uke na kushindwa kufanya tendo la ndoa(Vaginal Atrophy)
- Kukosa hamu ya tendo la ndoa
- Kuwa mkavu Ukeni, na kuhisi maumivu makali wakati wa tendo la ndoa.
Tiba Zake
James Herbal Clinic tuna dawa aina tatu zinazoondoa tatizo la kuvimba kwa mirija ya uzazi, nazo ni: REDEEMER, NEOTONIC na CARD HERB, Dawa hizi zote ni antioxidants, na ni Anti-inflammatories.
Unahitaji huduma, tafadhari tupigie: 0752389252 au 0712181626