JE, UNAJUA SABABU YA KUOTA VIVIMBE VIDOGOVIDOGO KATIKA TUMBO LA UZAZI(ENDOMETRIOSIS)?

Ndugu msomaji, baadhi ya wanawake wanaposumbuka na matatizo ya tumbo muda mrefu, waendapo kupima, hupewa majibu ya kadi zao, “Endometriosis”. Ukuta wa ndani wa kifuko cha uzazi unaitwa ‘endometrium.’ Ukuta huu hujengeka na kubomoka kila mwezi na kusababisha hedhi kwa wanawake. Kujengeka na kubomoka kwa ukuta huu wa ndani wa kifuko cha uzazi kunasababishwa na mabadiliko ya kiasi cha hormoni za uzazi mwilini mwa mwanamke.

Matokeo ya picha ya image of endometrium

Endometriosis ni ugonjwa unaosababishwa na uwepo wa tishu zinazofanana na ukuta wa ndani wa kifuko cha uzazi (endometrium) na sehemu nyingine kwenye mwili. Mara nyingi tishu hizi huota katika sehemu zifuatazo:

 

 

  • Kwenye sehemu ya chini ya tumbo la uzazi (pelvis)

 

  • Karibu na vifuko vya mayai(ovaries),

 

 

  • Mirija ya uzazi(fallopian tubes)

 

  • Mfuko wa kizazi(Uterus)

 

  • Kibofu cha mkojo na njia ya haja kubwa.

 

Matokeo ya picha ya image of endometriosis

NUKUU: Kama ilivyo kwa ukuta wa ndani wa kifuko cha uzazi (endometrium), tishu hizi zinazopatikana nje ya kifuko cha uzazi pia hujengeka na kubomoka kutokana na mzunguko wa hedhi. Kwa sababu hii, hata dalili za uwepo wa ugonjwa wa endometriosis hufuatana na mzunguko wa hedhi.

 

 

Je, Chanzo Chake Ni Nini?

 

 

 

 

 

 

Kitu kinachosababisha ugonjwa huu hakijafahamika kwa uhakika lakini inaaminika kuwa kiasi kidogo cha damu kinachoingia tumboni wakati wa hedhi kupitia mirija ya uzazi hubeba seli za ukuta wa kizazi (endometrium) ambazo huota ndani ya tumbo.

 

Kutokana na uwepo wa endometriosis ndani ya tumbo, damu inayotokana na kujengeka na kubomoka kwake kila mwezi hukosa njia ya kutokea. Kwa sababu hii, damu hii huganda na kusababisha makovu katika sehemu za ndani ya tumbo (abdominal cavity). Ugonjwa huu unapoendelea kwa muda mrefu, makovu haya huweza kushambulia kiungo kilichokuwa na endometriosis na kukiharibu.

 

Kwa mfano, endometriosis ikishambulia vifuko vya mayai(ovaries) inaweza kuviharibu na kusababisha mwanamke kushindwa kutoa mayai ili kupata mtoto,au ikishambulia njia ya mkojo inaweza kuiziba njia hiyo na kusababisha mafigo kuharibika , au ikishambulia njia ya haja kubwa inaweza kusababisha maumivu wakati wa haja kubwa. Vilevile endometriosis inayoshambulia ovari inaweza kusababisha uvimbe wa ovari hiyo (ovarian cysty).

 

Matokeo ya picha ya image of endometriosis

Aina mojawapo ya endometriosis ni ile inayopatikana ndani ya msuli wa kifuko cha uzazi. Aina hii ya endometriosis inaitwa adenomyosis. Vilevile endometriosis huweza kutokea kwenye kovu baada ya oparesheni ya kujifungua mtoto ( caesarean section scar). Kovu lenye endometriosis hutoa majimaji wakati wa hedhi na kwa kipindi hicho huwa na maumivu. Mara chache hutokea endometriosis kuwa sehemu zilozo mbali na viungo vya uzazi kama vile kwenye mapafu, jambo ambalo husababisha kukohoa damu wakati wa hedhi (catamenial hemoptysis).

 

 

Je, Dalili Zake Zinakuwaje?

 

 

Dalili za uwepo wa endometriosis ni kama ifuatavyo:

 

  • Maumivu wakati wa hedhi (dysmenorrhoea),

 

  • Kutokwa na damu nyingi ya hedhi

 

  • Siku za hedhi kuwa nyingi zaidi ya siku 5,

 

  • Maumivu makali wakati wa hedhi
  • Kutokwa na damu yenye mabonge
  • Kutokwa na vi nyamanyama(tissue) wakati wa hedhi

 

  • Kushindwa kupata ujauzito (sterility),

 

  • Kuhisi maumivu wakati wa kufanya tendo la ndoa (dyspareunia)

 

  • Kuhisi maumivu wakati wa haja kubwa au ndogo.

 

  • Maumivu ya kiuno, au nyonga

 

  • Ugumba

 

  • Kukosa choo,

 

 

Je,Vipimo Vinatakiwa Vifanyike Vipi?

 

 

 

 

Mwanamke mwenye dalili za endometriosis anatakiwa kupimwa na daktari ili aweze kupewa ushauri wa matibabu.

 

 

 

Zipo aina kuu tatu za vipimo, nazo ziko kama ifuatavyo:

 

 

  • Kupimwa kwa mikono ya daktari,

 

  • Kupimwa kwa njia ya ultrasound

 

 

  • Kupimwa kwa njia ya upasuaji wa matundu madogo (laparoscopy).

 

Matokeo ya picha ya image of a doctor exermining a woman with endometriosis by using ultrasound

 

Je, unahitaji huduma kwa ajili ya Endometriosis? Kwa mawasiliano tupigie kwa namba hizi: 0752389252 au 0712181626,

 

Arusha-Mbauda

 

Karibuni sana!

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *