JE, UNAJUA SABABU ZA KUTOKWA NA MAJIMAJI MACHAFU KATIKA VIA VYA UZAZI VYA MWANAMKE? JE, NINI MADHARA YAKE?.

 

Mpendwa  msomaji na ikumbukwe kwamba, kutokwa na majimaji au ute katika via vya uzazi vya mwanamke ni jambo la kawaida wakati ambao mwanamke bado ana umri wa kuzaa, ikiwa ni sehemu ya mwili katika kuondoa sumu au kemikali.

Ute huu kwa kawaida hauna rangi hadi ukikauka juu ya nguo ya ndani ndiyo huashiria rangi nyeupe au njano. Hata hivyo, hali hii huwa kwa kiasi kidogo ambacho hakihitaji mwanamke kuvaa kitu kingine zaidi ya nguo ya ndani ya kawaida ili kuuzuia.

Lakini majimaji hayo huashiria ugonjwa wa hatari yanapokuwa yanaambatana na dalili zifuatazo, naomba uwe makini na uzingatie kabisa:

 

  • Maji maji au ute kubadilika rangi na kuwa kama maziwa mtindi, chokleti, njano, kijani, rangi ya usaha, au rangi ya juisi ya parachichi.
  • Majimaji yakiambatana na harufu mbaya hata kama mwanamke ameoga na kuvaa vizuri. Kuna wakati harufu inakuwa kama shombo la samaki hasa wakati wa kushiriki tendo la ndoa au baada ya tendo la ndoa.
  • Ute unapozidi kiwango chake cha kawaida cha kila siku (abnormal quantity of discharge).
  • Maumivu wakati wa kushiriki tendo la ndoa.
  • Maumivu wakati wa kujisaidia haja ndogo
  • Kuwashwa sehemu za nje na ndani za via vya uzazi vya mwanamke.
  • Via vya uzazi kuwa na rangi nyekundu kuliko rangi yake ya ngozi ya siku zote.
  • Muwasho sehemu za mlango wa via vya uzazi kwa ndani.
  • Maumivu chini ya kiuno, mbele na nyuma, pia chini ya kitovu na hasa kushoto au kulia.
  • Sehemu ya nje ya via vya uzazi kuwa nyekundu na wakati mwingine wekundu huo kuambatana na michubuko, vidonda na maumivu.

 

 

Je, Nini Chanzo Cha Tatizo Hili?

 

 

 

 

Naomba ieleweke hivi kwa kila mmoja wetu, hali hii hutokana na maambukizi au mashambulio katika njia ya uzazi ya mwanamke na si njia ya mkojo,  hutokana na kufanya mapenzi yasiyo salama na mtu ambaye ana magonjwa ya zinaa, hivyo bakteria, virusi au fangasi hushambulia njia ya uzazi.

Maambukizi haya yapo ya aina kuu tatu ambayo kitaalam ni “bacterial vaginosis”, “trichomoniasis” na “monilia”.

 

  1. Kufanya mapenzi kinyume na maumbile na wakati huohuo kuhamia kwenye uke na kuhamisha uchafu na wadudu ambao hushambulia njia ya uzazi.

 

  1. Ulaji mbovu: Utokwaji wa uchafu ni tatizo linalowakumba wanawake wengi wa mijini kwa sababu ya ulaji mbovu. Chakula chenye mafuta kinachochea au kinaamsha seli za mafuta (fat cells) mwili mzima na hivyo husababisha kuzalishwa kwa homoni nyingi za estrogen.
    Homoni hizi zikiambatana na upungufu wa fiber huchochea ukuaji wa bakteria wa ndani ya utumbo. Bakteria hawa wana sifa ya kubadilisha bile acid kuwa homoni za estrogen ambazo zinapozidi sana husababisha tatizo la mwanamke kutokwa na uchafu katika via vyake vya uzazi.

 

  1. Njia za kisasa za uzazi wa mpango (hasa vidonge) zinapotumiwa bila kujali ushauri wa kitaalam na usafi, husababisha kuharibika kwa ukuta wa uke ambao ni ulinzi, hivyo huharibu afya ya uke na huufanya uwe na hali ya alkali(chumvichumvi) ambayo huruhusu au huchochea bakteria na fangasi kuvamia na kuzaliana kirahisi tena kwa kasi. Hivyo, fangasi, hasa candida albicans huzaliana sana na kushambulia sehemu ya uke.

 

  1. Kutowiana kwa homoni za mwanamke: Hali hii inasababishwa na vyanzo vingi, mfano unene au uzito kupita kiasi, ujauzito, wakati wa hedhi, n.k.
    Uchafu wa mavazi na uchafu wa mwili hasa kwa mwanamke ambaye hajui jinsi ya kujisafisha katika via vyake vya uzazi ili kuondoa seli zilizokufa (dead cells)

Je, Nini Madhara Ya Kutokwa Na Uchafu Ukeni?

 

 

 

 

 

Madhara ya kutokwa na uchafu huo kama ifuatavyo:

 

 

  1. Ugumba:

 

 

Hali hii hutokea pale mashambulizi au maambukizi yanapofika kwenye mirija na kuleta uvimbe ambao huziba au kusababisha kutengenezwa kwa maji machafu mazito ambayo nayo huziba mirija na kuharibu mimba kila inapotungwa.
Mwanamke hufikia hali ya kutoa harufu mbaya wakati wote hata kama ameoga na kuvaa vizuri.

 

 

 

  1. Kushiriki Tendo La Ndoa

 

 

 

Hali huwa mbaya zaidi wakati wa kushiriki tendo la ndoa. Jambo hili husababisha mwanamke kuwa na aibu na kujitenga, kutengwa, kujiona hana thamani na unyonge.

 

 

  1. Kupata maambukizi katika njia ya mkojo yaani U.T.I.:

 

 

 

Hali hii ni kwa sababu njia ya uzazi na ile ya mkojo zimekaribiana sana sehemu zinapoanzia kwenye via vya uzazi vya mwanamke. Hivyo, mwanamke kuhisi maumivu wakati wa kutoa haja ndogo au kwenda haja ndogo mara kwa mara, na kutoa haja ndogo yenye rangi ya njano au kijivu ni baadhi ya dalili za ugonjwa wa U.T.I

 

 

 

Je, utokwaji wa uchafu katika via vya uzazi vya mwanamke ni kiashiria cha matatizo au magonjwa gani?

 

 

Utokwaji wa uchafu katika via vya uzazi vya mwanamke ni kiashiria cha magonjwa yafuatayo:

 

  • Kuvimba kwa mirija ya uzazi (salpingitis). Tatizo hili likichelewa kutibiwa, basi mirija huziba na hivyo mwanamke hupoteza uwezo wa kushika ujauzito.

 

  • Mrundikano wa vivimbe vidogo vingi kwenye vifuko vya mayai ya uzazi (polycystic ovarian syndrome). Asilimia 75 ya wenye tatizo hili hupoteza uwezo wao wa kushika ujauzito.

 

  • Kuwa na uvimbe kwenye vifuko vya mayai ya uzazi upande mmoja au pande zote mbili, kushoto na kulia (ovarian cyst).

 

  • Kama utokwaji wa uchafu utaambatana na matatizo ya kukosa hedhi au hedhi kupishanapishana ni kiashiria tosha cha tatizo hili.

 

  • Kujaa maji kwa mirija ya uzazi (hydrosalpinx). Tatizo hili pia husababisha mirija kuziba lisipotibiwa mapema.

 

  • Kushambuliwa na fangasi aina ya candida albicans kwenye njia ya uzazi (vaginal candidiasis).

 

  • Kuvimba kwa kuta za uke, tatizo linaloitwa vaginitis.

USHAURI: James Herbal Clinic tunapenda kuwashauri wale wote wanaosumbuliwa na tatizo hili la kutokwa na uchafu, wazingatie mambo yafuatayo kabla hawajafika katika vituo vya afya;

 

 

  • Kupunguza au kuacha kabisa kutumia vyakula vya sukari au vinywaji vyote vyenye sukari kwa muda wa miezi miwili, kwani fangasi au candida albicans hutumia sukari kama chakula.

 

  • Kuacha kunywa maziwa kwa miezi miwili au zaidi.

 

  • Mwanamke anapokuwa na ugonjwa huu, atafute tiba ya ziada haraka sana ili kuepuka ugumba.

Kwa wale wenye matatizo ya kutokwa na uchafu sehemu za uke, na wengine wote wenye magonjwa sugu, mnakaribishwa James Herbal Clinic:

Kwa mawasiliano tupigie: 0752389252 au 0712181626