Hali ya ugumba inatafsiriwa kama vile mwanamke kutokushika ujauzito angalau mara moja kwa mwaka japokuwa anafanya tendo la ndoa kila mara lakini bila mafanikio.
Visababishi vya ugumba wa mwanamke vinaweza kuwa vigumu sana kuvipima na kuvitambua. Zipo tiba nyingi sana ambazo zinategemeana na chanzo cha ugumba. Wanandoa wengi wenye matatizo ya ugumba wanaweza wakafanikiwa kupata ujauzito hata bila kutumia tiba.
Je, Dalili Zake Zinakuwaje?
Dalili kuu za tatizo la ugumba kwa mwanamke ni kutokuwa na uwezo wa kupata ujauzito. Mzunguko wa hedhi ambao huwa mrefu(yaani siku 35 na zaidi), au mfupi(yaani chini ya siku 21), au mzunguko wa kubadirika badirika au kutokuona hedhi kabisa inaweza kumaanisha kwamba huna uwezo wa kupevusha mayai. Kunaweza kusiwepo na dalili zozote za nje.
Je, Nini Husababisha Hali Ya Ugumba Kwa Mwanamke?
Kwanza kabisa ni urutubishaji na upandikizaji wa yai kwenye ukuta wa mfuko wa uzazi. Mambo hayo ni ya muhimu sana ili kumfanya mwanamke kuwa mjamzito. Lakini yapo mambo muhimu mengine kama yafuatayo:
- Unahitaji Kupevusha Mayai Yako
Kwa kawaida ili mwanamke aweze kuwa mjamzito, vifuko vyake vya mayai(ovaries) vinapaswa vizarishe na kuachia yai litoke, kitendo ambacho kitaalam kinaitwa upevushaji(ovulation). Daktari anaweza kukupima na kuhakiki ikiwa kama kazi ya upevushaji inafanyika au haifanyiki katika mfumo wako wa uzazi.
- Mwenzi Wako Anapaswa Kutoa Mbegu
Wanandoa wengi yaweza kuwa hili likawa tatizo kwao ikiwa kama wana historia za maradhi au kama waliwahi kufanyiwa upasuaji. Lakini daktari wako anaweza kukufanyia vipimo ili kuona afya na uwezo wa mbegu za mwenzi wako kama zina uwezo wa kurutubisha yai.
- Unapaswa Kufanya Tendo La Ndoa Mara Kwa Mara
Ikiwa kama ni wanandoa mnapaswa kufanya mapenzi mara kwa mara hasa inapofikia siku za hatari. Ikiwa kama kuna tatizo linakusumbua katika kufahamu siku zako za hatari, basi daktari wako anaweza kukusaidia kuweza kuelewa ni kipindi gani cha siku za hatari mara baada ya kutoka hedhini.
- Mwanamke Unapaswa Uwe Na Mirija Ya Uzazi Iliyo Wazi Na Mfuko Wa Uzazi Ukiwa Katika Hali Ya Kawaida.
Yai na mbegu za mwanaume hukutana pamoja kwenye mirija ya uzazi, na kiinitete(embryo) kinahitaji mfuko wa kizazi wenye afya imara ambapo kinaweza kukua.
NUKUU: Ili ujauzito uweze kutokea, yafaa kila hatua za mfumo wa uzazi wa mwanamke ziweze kufanya kazi kwa usahihi. Hatua hizo ni kama ifuatavyo:
- Vifuko vyote viwili vya mayai sharti viwe na uwezo wa kukomaza yai na kuliachia
- Yai liweze kunyakuliwa na mrija wa uzazi
- Mbegu za mwanaume ziweze kuogelea mpaka kwenye mlango wa kizazi, kupitia mfuko wa kizazi na kuingia kwenye mrija wa uzazi ili kulifikia yai kwa ajili ya kulirutubisha.
- Yai lililorutubishwa sharti lisafiri kupitia mirija ya uzazi mpaka kwenye mji wa mimba.
- Yai lilorutubishwa shatri lijipachike na kukua ndani ya mji wa mimba.
NUKUU: Kwa upande wa wanawake, matatizo mengi yanaweza kuharibu kazi ya mfumo wa uzazi. Ugumba kwa mwanamke husababishwa na mambo yafuatayo hapo chini:
- Vivimbe kwenye vifuko vya mayai
- Tezi ya pituitary kushindwa kuzarisha vichochezi
- Yai kushindwa kukomaa
- Kuwepo kwa homoni nyingi ya prolactin
NUKUU: Unataka kujua zaidi juu ya mvurugiko wa homoni bonyeza hapa: Fahamu Dalili 16 Za Mvurugiko Wa Homoni(Hormonal Imbalance)
Je, Kuharibika Kwa Mirija Ya Uzazi Kunakuwaje?
Mirija iliyoharibika au kuziba huzizuia mbegu za mwanaume zisiweze kulifikia yai au kuziba njia kabisa ya yai lililorutubishwa lisiweze kuingia kwenye mfuko wa uzazi. Visababishi vya mrija wa uzazi kuziba au kuharibika vinaweza kuwa ni:
- Maambukizi katika via vya uzazi au PID kutokana na maambukizi ya magonjwa ya pangusa(Chlamydia), Kisonono au maambukizi mengine ya zinaa.
- Kufanyiwa upasuaji kutokana na mimba kutunga nje ya kizazi
Rafiki, naomba makala yetu iishie hapa, nikaribishe kipindi cha maswali na maoni yako.
Pia unaweza kutuma namba yako ya WHATSAP ili uunganishwe kwenye darasa letu uweze kupata mafunzo juu ya tiba, ushauri na vyanzo vya magonjwa mbalimbali.
Je, unahitaji huduma? Wasiliana nasi kwa namba hizi: 0768 559 670
Arusha-Mbauda
Karibu sana!