JE, UNAJUA VYANZO NA DALILI ZA KUTOKWA DAMU KWENYE FIZI(GINGVITIS)?

 

Fizi kutoa damu ni jambo la kawaida na inaonekana kama ugonjwa husababisha masumbufu, kwakuwa fizi hubadirika na kuwa nyekundu sana, pia kuvimba. Yafaa kuwa makini mara uonapo dalili hizi na kuanza kuzitibu mapema tena kwa haraka bila kuchelewa. Hali ya fizi kutoa damu inaweza kusababisha magonjwa mengine mabaya na kufanya meno kung’oka.

Inaonekana kuwa chanzo kikubwa cha fizi kutoa damu ni kutokana na hali ya kutokujali usafi, kama vile kupiga mswaki baada ya kula, au kuchukua nyuzi ili kusugua meno, kunaweza kusaidia fizi kushindwa kutoa damu.

 

 

 

 

Je, Dalili Zake Zinakuwaje?

 

Fizi zenye afya imara ni zile  zenye rangi ya pinki ya weupe na iliyokaza kabisa kwenye meno. Ishara na dalili za fizi zinazotoa damu ni pamoja na:

 

  • Fizi kuvimba

 

  • Fizi kuwa nyekundu sana

 

 

  • Kutokwa damu mara upigapo mswaki

 

  • Harufu mbaya kinywani

 

 

  • Fizi kuwa laini

 

Wanawake wajawazito kwa kawaida huathiriwa na tatizo hili mara kwa mara. Ukiwa mjamzito tunza afya yako ikiwa pamoja na meno.

 

 

Je, Hatua Ya Pili Ya Ugonjwa Wa Ufizi Huwa Hatari Sana Inakuwaje?.

Waweza kuwa na ishara au dalili zilizotajwa hapo juu, japo utaziona zingine hapo chini nazo ziko kama ifuatavyo:

 

  • Usaha kutoka kwenye meno na ufizi

 

  • Meno kulegea

 

 

  • Nafasi kubwa katikati ya meno mahali ambapo ufizi inapaswa kuwa

 

  • Kutokuwepo na tofauti katika mpangilio wa meno ukiyauma chini.

 

Kama nilivyoeleza mwanzo, kuwa chanzo kikubwa cha tatizo hili ni kutokufanya usafi ambao husababisha ukoko(plague) kukusanyikana kwenye meno, na kusababisha uvimbe kwenye tishu za fizi. Hapo chini ndipo unaweza kuona ukoko au utando unavyoweza kusababisha kutokwa na damu kwenye fizi:

 

1. Utando Au Ukoko Hujengeka Kwenye Meno Yako

 

 

 

Utando huu unaogandamana na kushikamana kwenye meno mara nyingi huwa na bakteria ambao huzariana kwenye meno yako wakati unapokula vyakula vyenye sukari na wanga na hivyo kushindwa kuyasafisha meno yako.

 

Utando wa meno unapaswa kuwa unatolewa kila siku kwakuwa hujengeka haraka mno.

 

 

2. Utando Hubadirika Na Kuwa Ugwagwa Au Ukoga

 

Utando unaokaa kwenye meno yako unaweza kugandamana na kuwa mgumu kabisa kwenye fizi zako na baadaye kuwa ugwagwa(tartar), ambao hukusanya bakteria.

 

Ugwagwa huufanya utando au ukoko kwenye meno kuwa mgumu zaidi na kushindwa kutolewa, kwani hutengeneza ngome ili bakteria wasiweze kuingia na kusababisha masumbufu makubwa kwenye fizi zako. Hivyo unahitaji kumuona daktari mtaalam wa wa kusafisha meno yako ili kuondoa ugwagwa.

 

 

 

  1. Fizi Huvimba

 

Kadiri ugwagwa na utando wa meno unavyozidi kukaa kwa muda mrefu bila kuondolewa, ndivyo huharibu fizi zako na kusababisha uvimbe.  Kwa kawaida fizi zako huvimba na kutoa damu kwa urahisi sana.

Pia inaweza kujitokea hali ya meno kuoza. Ugonjwa huu usipotibiwa, basi hali ya kuvimba kwa fizi inaweza kuongezeka, meno kulegea na hata kung’oka.

 

 

Je, Ni Nini Vihatarishi Vyake?

 

Hali ya fizi kutoa damu ni jambo la kawaida, na kila mmoja anaweza kupatwa na hali hii. Mambo yanayoweza kuongeza vihatarishi vya fizi kutoa damu ni:

 

  • Kutokufanya usafi wa meno
  • Uvutaji sigara au kutumia ugoro
  • Umri mkubwa
  • Mdomo kukauka
  • Lishe duni, hasa kupungukiwa na vitamini C.
  • Kubadirika kwa vichochezi(hormonal change), hasa kwa kina mama wajawazito, mzunguko wa hedhi au matumizi ya madawa ya uzazi wa mpango
  • Madawa mbalimbali ya vidonge, kama vile phenytoin, nk, ambayo hutumika kwa ajili ya wagonjwa wa kifafa, pamoja na baadhi ya madawa ambayo huzuia kuingia kwa madini ya Kalisiam mwilini, madawa yatumikayo kwa ajili ya shinikizo la juu la damu.

 

Tahadhali

 

 

Na ieleweke kuwa, ili kuondokana na tatizo hili, kila mmoja anapaswa afanye mambo yafuatayo:

 

  • Kufanya usafi wa meno kwa muda wa dakika 2 angalau mara mbili kila siku baada ya kumaliza kula, asubuhi baada ya kupata kifungua kinywa na jioni baada ya kupata mlo wa jioni.

 

  • Jihadhari sana na vyakula vyenye wingi wa sukari kama vile keki, chokleti, nk.

 

TIBA YAKE

 

James Herbal Clinic tuna dawa nzuri ya meno pamoja na magonjwa mbalimbali ya kinywa, nk, nayo ni RIGTH HERBS, jipatie  kwa shilingi 5000 tu, uondoe tatizo lako la meno.

 

 

Kwa mawasiliano tupigie: 0752389252 au 0712181626-Arusha

 

Karibuni sana!!!

15 thoughts on “JE, UNAJUA VYANZO NA DALILI ZA KUTOKWA DAMU KWENYE FIZI(GINGVITIS)?

  1. Mm nina ugonjwa wa fizi yangu imeota kinyama kwa juu kias imefunika jino kdg imevimba pia imeweka usaha hyo dawa kama inasaidia tafafhal nitumie nipo dar

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *