JE, UNAJUA VYANZO NA DALILI ZA UGONJWA WA GOUT? JE, NINI MADHARA YAKE?

 

Ugonjwa wa gouti ni aina ya uvimbe unaofanana kama ugonjwa wa baridi yabisi, ambao mara nyingi huwapata watu wanaopenda kula vyakula  vya nyama mara kwa mara hasa ya mbuzi, swala au nyama choma, au vyakula vyenye vikolezo vingi, na vinywaji kama vile pombe. Na mara nyingi watu wenye tatizo hili pia huwa wenye uzito mkubwa, yaani wanene.

 

Je, Dalili Za Ugonjwa Huu Zinakuwaje?

 

 

 

Kwa kawaida dalili za ugonjwa huu huwa kama ifuatavyo:

 

  • Maumivu makali kwenye jointi za mifupa hasa wakati wa usiku wa manane
  • Kuhisi maumivu makali na uvimbe kwenye vidole vya mikono au miguu
  • Uvimbe kwenye magoti, viwiko vya mikono, na nyonga pia
  • Maumivu kuongezeka wakati wa kutembea
  • Ngozi kuwasha na kubanduka mara baada ya kusinyaa
  • Kukosa hamu ya kula
  • Kupatwa na matatizo ya tumbo kama vile kukosa choo, nk.
  • Kuhisi homa
  • Kukojoa mara kwa mara.

 

 

 

Je, Nini Husababisha Ugonjwa Huu?

 

 

 

Ugonjwa wa gauti husababishwa na mkusanyiko wa uric acid kwenye damu. Kiwango hiki cha uric acid kinapopanda juu na kufikia hatua ambayo figo hushindwa kabisa kuichuja, basi ndipo uric acid hukusanyika na kuzama ndani ya jointi za mifupa zilizoathirika, na hivyo kusababisha maumivu makali yenye kuutesa mwili sana. Mkusanyiko huo wa uric acid unaweza pia kujengeka kwenye viungo vingine muhimu vya mwili na kusababisha uharibifu mkubwa sana.

Hata hivyo, mwili hushindwa kuvumilia na kuhimili mkusanyiko wa uric acid inayotokana na nyama, na ndio maana hukusanyika na kukaa mwilini.

 

Ugonjwa wa gauti kwa kawaida hushambulia viungo vidogo vidogo vya mikono na miguu, hasa kidole kikubwa cha mguu. Uric acid hujaa kwenye jointi za mifupa na kusababisha uvimbe, hali ya wekundu kwenye jointi, na kuhisi hali kama vile moto pamoja na maumivu makali.

 

 

NUKUU: Ugonjwa huu huwaathiri sana wanaume,nao huanza pale afikishapo umri wa miaka 35-45. Lakini pia wanawake hupatwa na ugonjwa huu mara wakaribiapo umri wa kukoma hedhi au baada ya kukoma hedhi.

 

Tiba Yake

 

 

 James Herbal Clinic tuna dawa za asili zenye mchanganyiko wa vyakula na mimea ya sili, zenye uwezo wa kuondoa tatizo la gauti, nazo ni NEOTONIC, FRESH HERB na PURE HEALING POWDER.

 

Je, unahitaji huduma? Tupigie kwa namba hizi: 0752 389 252 au 0712 181 626

 

Arusha-Mbauda

 

 

Karibuni sana.