Je, umewahi kufikiria namna gani mwili wako unapokuwa wenye afya, unashindwa hata kutambua sehemu zako za uke? Lakini hali inapokuwa mbaya, sidhani kama huwa ni vigumu mwanamke au binti kutojali jambo hili. Bacterial Vaginosis huwa ni maambukizi ya kawaida ukeni ambayo hupotea kwa nadra sana pasipo kugundulika. Bakteria hawa wakati mwingine wanaweza kuchangamana na maambukizi ya fangasi au ugonjwa wa zinaa kama vile malengelenge, lakini sio maambukizi ya zinaa.
NUKUU: Pamoja na bacterial vaginosis, ukuaji wa bakteria unaweza kusababisha dalili zenye masumbufu kabisa kama vile; kubadirika kwa uchafu unaotoka ukeni au harufu yake, mara nyingi huonekana kuwa wenye rangi nyeupe au wa kijivu, tena wenye harufu mbaya kama shombo ya samaki. Baadhi ya wanawake wanaweza kupatwa na hali ya uvimbe na muwasho, japokuwa hali ya muwasho huwa ya kawaida.
Je, Nini Husababisha Bacterial Vaginosis?
Viwango vya chini kabisa vya bakteria wa kawaida wakaao ukeni ambao wanaweza kusababisha tatizo la bacterial vaginosis kwa kawaida huonekana ndani ya uke. Huwa ni tatizo wakati bakteria wanapokuwa wengi.
Mambo kadhawakadha yanayoweza kusababisha kuongezeka kwa idadi ya bakteria huwa ni:
- Kujamiiana
Shahawa huongeza kiwango cha joto ukeni, hali ambayo inaweza kuchangia kiasi kikubwa cha ukuaji wa bakteria. Hivyo unapomaliza kufanya tendo la ndoa, hakikisha unasafisha uke wako. Usipende kulala na shahawa ukeni.
- Kuosha Sehemu Za Uke
Kuosha sehemu za uke kwa kutumia sabuni zenye madawa makali au kupulizia marashi, husababisha uvimbe na kunaweza kuongeza vihatarishi vya maambukizi. Hali hii pia inaweza kuondoa baadhi ya bakteria wazuri.
- Ubadirishaji Wa Milo
Kitu chochote kinachoweza kuathiri mfumo wa umeng’enyaji chakula tumboni ndani ya mfumo wa mwili wako, kinaweza kuathiri uwiano wa kawaida wa bakteria. Pia, chakula duni kinaweza kuathiri uwezo wa mwili wako kujirudisha katika hali ya kawaida.
- Chupi Zilizotengenezwa Kwa Nyuzi Za Nylon(Tights)
Uvaaji wa nguo za ndani zenye kubana kama vile tight zinaweza kuziba hewa isiweze kupita katika eneo la uke, hali ambayo inaweza kusababisha muongezeko wa bakteria kukua na kuwa wengi.
- Sabuni Zenye Marashi
Utumiaji wa sabuni zenye manukato makali kuoshea sehemu za uke husababisha mlipuko mkubwa wa bakteria ukeni.
- Kutokubadiri Nguo Ya Ndani
Bila shaka yawezekana ulikuwa unafanya kazi nzito tena ngumu na hivyo ukawa unatokwa na jasho jingi na kusababisha mpaka chupi kulowana. Hali hii pia huchangia sana bakteria kukua ndani ya uke na kuongezeka.
Je, unahitaji huduma? Tupigie kwa namba 0752389252 au 0712181626
Arusha-Mbauda
Karibuni sana