NUKUU: Kupima na kutambua tatizo lako la uvimbe kwenye mayai ni jambo la muhimu sana kwa ajili ya tiba, lakini wakati mwingine huwa ni rahisi sana kushindwa kuzigundua dalili hizi. Sasa hebu tuangalie jinsi zinavyokuwa:
Hivi leo tunaona idadi kubwa ya wanawake wamekuwa wakiathiriwa sana na ugonjwa wa uvimbe kwenye mayai au vifuko vya mayai(Ovarian Cysts). Kwa kawaida vifuko vinavyojaa majimaji katika maeneo hayo huwa vidogo sana, navyo huwa maeneo ya ndani au juu ya vifuko vya mayai. Hali hii mara nyingi husababishwa na mabadiriko badiriko ya vichochezi au homoni, na vinaweza kuendelea muda wowote katika umri wa wa kuzaa wa mwanamke.
NUKUU: Ingawa huwa sio tatizo kuwa la ki afya, lakini inafaa sana mwanamke kuwa anapata vipimo mara kwa mara ili kuweza kuvizuia visiweze kuendelea.
Dalili mbalimbali anapaswa mwanamke kuzitambua mapema, ingawa zingine zinaweza kuonyesha kuwepo wa uvimbe wenyewe katika mayai. Dalili hizi huwa kama ifuatavyo:
- Mabadiriko Katika Mkojo
Badiriko lolote katika mkojo linaweza kuwa ndio dalili ambayo itakayokuonyesha kuwa una matatizo mbalimbali katika afya ya mwili wako. Endapo utajisikia ghafla tu kuhisi kukojoa hata kama huwezi kujizuia, jitahidi kutambua kwasababu hali hiyo inaweza kusababishwa na uvimve kwenye mayai(ovarian cysts). Dalili hizi kadiri zinapokuwa zinaonyesha hali ya kuwaka moto wakati wa kukojoa, zinakutambulisha kwamba sehemu zako za misuli ya nyonga zimeshakuwa dhaifu au tayari zimeshaathirika.
Ikiwa kama tatizo litaendelea zaidi ya siku mbili, ni vyema kabisa kuwahi na kumuona daktari wa vipimo.
- Kutokwa Na Damu Isiyo Ya Kawaida
Moja ya dalili za matatizo ya homoni ambazo huwa wazi kabisa ni kutokwa na damu ya matone ambayo inaweza kujitokeza kabla ya kipindi chako cha hedhi hakijafika au mara baada ya kutoka hedhini unaweza kuona tena hali ya kutokwa damu. Ingawa huwa ni hali ya kawaida kwa wanawake wengi kupatwa na hali hii mara kwa mara, lakini inapojitokeza kwa kujirudia ni vyema kufika hospitali na kumuona daktari.
- Kuhisi Maumivu Wakati Wa Tendo La Ndoa.
Maambukizi sehemu za uke pamoja na hali ya uvimbe huwa ni sababu za msingi zinazoonyesha kwanini baadhi ya wanawake huhisi maumivu wakati wa tendo la ndoa. Lakini tatizo likiwa la kuendelea kiasi kwamba linaathiri hali yako ya kawaida ya kufanya tendo la ndoa, basi unapaswa kumuona mtaalam ili aweze kukusaidia kuondoa matatizo mengine yote.
- Kuhisi Kichefuchefu Na Kutapika
Kichefuchefu na kutapika huwa ni dalili ambazo wanawake wajawazito huzitapata. Kutokuwa na uwiano sawa wa vichochezi(hormonal imbalance) ambao husababisha vivimbe kwenye mayai(varian cysts) pia unaweza kusababisha dalili hizi kwa wanawake wenye ujauzito.
- Tumbo Kuvimba
Hii ni dalili ambayo mara nyingi hushindwa kuzingatiwa kwasababu kwa kawaida husababishwa na mambo mengine. Kuvimba kwa eneo la tumbo husumbua sana na pia kunaweza kuambatana na maumivu. Ikiwa kama unasumbuliwa na tatizo hili mara kwa mara na huoni nafuu yoyote ndani ya siku chache, basi ni ishara kwamba huenda kuna kitu kibaya kimejitokeza.
- Maumivu Ya Kiuno
Hali ya kuhisi kukaza kwa kiuno au maumivu sehemu za kiuno cha chini mara nyingi huwa haionyeshi kwamba una matatizo ya misuli. Wakati mwingine tatizo kama hili huwa linahitaji uchunguzi wa kina, kama inaweza kuwa ni matatizo ya figo au matatizo kwenye mfumo wa uzazi. Na ndio maana huwa napenda sana kuwashauri kina mama wenye dalili kama hizi kuenda kufanya vipimo kwanza.
- Ghafla Mwili Kuwa Na Uzito Mkubwa Au Kupungua Uzito
Hali ya mwili kupungua ghafla inaweza kuonekana kama vile ni mbaraka kwa mtu mwenye tatizo la unene. Lakini kama hutakuwa na juhudi ya kuweza kufanikisha kuliondoa, ni vyema kabisa ukalijali kwa tahadhari kwasababu hali yoyote mbaya inaweza kujitokeza. Mtu anaweza akapatwa na hali ya kuongezeka ukubwa wa mwili au unene kutokana na mitindo yake ya ulaji katika maisha yake. Kukosa hamu ya kula au kula mara kwa mara vyakula vingi kutokana na hali ya wasiwasi ni ishara kwamba unapaswa uwe makini kujilinda na magonjwa.
- Kuhisi Mwili Kuchoka
Hali ya msongo wa mawazo, ulaji wa vyakula duni, na kufanya kazi sana kuzidi kiwango ni mambo mojawapo ya kawaida ambayo husababisha uchovu wa mwili. Kutokuwa na uwiano sawa wa vichochezi(hormonal imbalance), hata hivyo kunaweza kuongeza daima hali ya mwili kuchoka choka sana. Kama ukihisi kuwa mwili wako hauna nguvu, umechoka, au una matatizo, basi unapaswa uwe makini kutambua kuwa kuna uwezekano wa kuwa na vivimbe kwenye mayai(ovarian cysts).
- Maumivu Ya Nyonga
Maumivu katika eneo la nyonga ni dalili tosha za vivimbe kwenye mayai(Polycystic Ovarian Syndrome) au kwa kifupi POS. Hali hii ikiwa inajitokeza wakati wa kipindi cha hedhi, basi yafaa ukamuona daktari kwa ajili ya vipimo.
NUKUU: Dalili zote tulizoorodhesha hapo juu zinaweza zikaja kwa njia tofauti tofauti, kutegemeana na tatizo. Wakati mwingine dalili zinaweza kuambatana na mabadiriko kwenye utumbo mpana au hata hali yoyote mbaya kujitokeza.
Kama vivimbe kwenye mayai havitasababisha madhara yoyote, bado ni wazo jema kwenda kufanya vipimo ili lisiweze kuwa tatizo kubwa. Kwa nyongeza napenda niseme kwamba, yafaa sana ukatumia tiba za asili ili kuzuia na kuliondoa tatizo hili.
Je, unahitaji huduma? Kwa mawasiliano tupigie namba hizi: 0752389252 au 0712181626
Arusha-Mbauda
Karibuni sana
Amen