Wanawake wengi wanahitaji kufahamu, je vivimbe vya fibroid husababisha uzito wa mwili kuongezeka? Ndiyo, vivimbe vya fibroid vinaweza kusababisha kuwa mnene sana na uzito wa mwili kuongezeka moja kwa moja na kwa njia isiyo ya moja kwa moja.
Visababishi Vya Vivimbe Vya Fibroid, Je Vinaweza Kuufanya Mwili Kupata Uzito Wa Moja Kwa Moja Au Mwili Kunenepa Sana?.
Zipo njia mbili za msingi ambazo vivimbe vya fibroid vinaweza kusababisha moja kwa moja mwili kuwa na uzito mkubwa:
- Uzito wa uvimbe wa fibroid wenyewe
- Mvurugiko wa homoni (hormonal imbalance)
Je, Saizi Ya Fibroid Na Uzito Wa Mwili Vinakuwaje?
Saizi na uzito wa fibroid vinaweza kutofautiana sana. Baadhi ya vivimbe vya fibroid kamwe huwa havikui na kufikia ukubwa wa peasi na vinaweza kuendelea bila kutambulika kwa mgonjwa na hata kwa daktari. Na ndio maana wanaweza kuhangaika kupima kwa muda mwingi wasione tatizo la uvimbe lakini uzito wa mwili unazidi kuongezeka tu.
Vivimbe vingine hata hivyo, vinaweza kuku ana kufikia ukubwa wa tikiti maji na kuweza kuonekana kwenye kipimo chochote cha ultrasound, nk. Baadhi ya vivimbe vya fibroid huangukia mahali Fulani wa wigo kati ya sehemu hizi mbili muhimu sana.
Kadiri uvimbe unavyozidi kuwa mkubwa, ndivyo mwili wako unavyozidi kuwa na uzito mkubwa. Kwa kutegemeana na saizi yake na mahali ulipoota, uvimbe wa fibroid unaweza pia kuingiliana na kibofu cha mkojo au kinyesi, na kusababisha:
- Mkojo kutoka bila kujua, au
- Kushindwa kukojoa
- Kukosa choo
Dalili hizi zinaweza kutokea pale unapohisi mwili wako kuongezeka uzito.
Je, Vipi Kuhusu Mvurugiko Wa Homoni?
Tukiangalia tunaona kwamba mvurugiko wa homoni unaweza kusababisha uvimbe wa fibroid, na fibroid kwa upande mwingine inaweza kusababisha mvurugiko wa homoni. Mvurugiko huu unaweza kuathiri uunguzaji wa mafuta mwilini. Wakati baadhi ya mivurugiko ya homoni inaweza kusababisha uzito wa mwili kupungu, basi miingine husababisha uzito wa mwili kuongezeka kwa kupunguza uunguzaji wako wa mafuta mwilini na kuchochea mkusanyiko wa maji.
Mvurugiko wa homoni unaweza pia kuathiri kiwango cha ukuaji wa vivimbe vya fibroid. Muongezeko wa homoni ya estrogen unaosababishwa na ujauzito na kukaribia kukoma kwa hedhi kunaweza kuongeza kasi ya ukuaji wa uvimbe wa fibroid, ambao pia husababisha mwili kuwa na uzito wa haraka.
Sababu Zisizo Za Moja Kwa Moja Uvimbe Wa Fibroid Kukufanya Uwe Na Uzito Mkubwa.
Sababu zisizo za moja kwa moja za uzito wa mwili kuongezeka na kunenepa sana inahusiana na majibu ya kitabia kwa uvimbe wa fibroid na dalili zake. Hata kama hujapokea vipimo vya kitaalamu, bado unaweza kuwa unapatwa na baadhi ya dalili zifuatazo:
- Maumivu
- Kutokwa na damu nyingi sana wakati wa hedhi au katikati ya hedhi
- Kuhisi uchovu wa mwili sana
- Kukojoa mara kwa mara au kushindwa kukojoa
- Kukosa choo
- Kupungukiwa na damu mwilini
Pia unaweza kubonyeza link hizo hapo chini ili ujifunze zaidi juu ya matatizo na madhara ya uvimbe wa fibroid:
- Haya Ndio Madhara 4 Ya Uvimbe Wa Fibroid Kwenye Tumbo La Uzazi.
- Fahamu Aina Za Vivimbe Vya Fibroid, Dalili Na Tiba Zake.
Uchovu wa mwili, maumivu yasiyokoma, kuhisi kero, n ahata kushindwa kufanya kazi kutokana na dalili mbaya kunaweza kuibua viwango vya msongo wa mawazo.
Ili kukabiliana na dalili hizi, ni sharti uwe:
- Kula vyakula vizuri kama vile matunda, mboga za majani, nk
- Vyakula vya nafaka, nk
- Kufanya mazoezi mara kwa mara
Epuka sana vyakula vyenye wingi wa wanga kama vile ugali sembe, mikate myeupe, mandazi, chapati, tambi, nk. Hivi vyote husababisha uzito kuongezeka na kuwepo kwa uvimbe wa fibroid. Pia achana na vyakula vyenye sukari sana au chumvi za viwandani.
Je, Unawezaje Kupunguza Uzito Wa Mwili Na Kuondoa Uvimbe Wa Fibroid?
Mchanganyiko wa matibabu ya uvimbe wa fibroid na mabadiriko ya mtindo rahisi wa Maisha vinaweza kusaidia kupunguza uzito na kunenepa kwa mwili.
Hii ni Pamoja na:
- Dawa za asili zinazorekebisha mfumo wa homoni ili kutdhibiti kutokwa na damu nyingi na pia kuufanya uvimbe kusinyaa na kupotea kabisa
- Kutumia dawa za asili ili kuondoa uvimbe na kuzuia seli zinazofanya uvimbe kuota
- Kubadiri mtindo wako wa Maisha katika ulaji na unywaji pia
- Kufanya mazoezi hasa ya kutembea kwa mwendo wa kasi kila siku asubuhi na jioni.
Je, Nini Suluhisho Lake?
James Herbal Clinic tunazo dawa za asili zenye uwezo mkubwa wa kuondoa tatizo hili na madhara yake. Unaweza kutuma namba yako ya WHATSAP pia ili tukuunganishe na darasa letu la masomo ya afya.
Je, Unahitaji Huduma? Basi, wasiliana nasi kwa namba hizi: 0768 559 670/0712 181 626,
Arusha-Mbauda,
Karibu sana!