Uvimbe wa fibroid unaweza kutokea ndani au ya kizazi au kwenye mlango wa kizazi. Hivi sasa tatizo la uvimbe limekuwa la kawaida sana asilimia 80% kwa wanawake walio katika umri wa kuzaa.
NUKUU: Tuliwahi kujifunza tukaona kuwa kuna aina tatu za vivimbe vya fibroid vinavyomtia changamoto mwanamke katika maisha yake, tukaona aina hizi ni pamoja na;
- Subserosal
- Intramural
- Submucosal
Makala hii leo nitazungumzia kuwa ni lini na jinsi gani uvimbe wa fibroid unaweza kusababisha mwanamke asipate ujauzito, jinsi unavyoweza kutibu tatizo hili, na matarajio ya kupata ujauzito endapo kama una uvimbe wa fibroid.
Je, Uvimbe Wa Fibroid Na Uzazi Inakuwaje?
Wanawake wengi wenye tatizo la uvimbe wa fibroid bado wanaweza kuwa na uwezo wa kupata ujauzito kwa asili yao. Uvimbe wa fibroid unaweza kuwa ni chanzo cha mwanamke kutokupata ujauzito kwa asilimia 1% hadi 3% kwa wanawake ambao tayari wanao. Wanawake wengine wanaweza wakapata ujauzito hata kama wana uvimbe.
NUKUU: Uvimbe wa fibroid unaweza kuathiri uwezo wako wa kupata ujauzito kwa namna mbalimbali, kutegemeana na ukubwa wake, mahali ulipo na aina ya uvimbe wenyewe. Uvimbe aina ya submucosal hasa ndio aina ya uvimbe ambao unaweza kuota ndani ya kizazi na unaweza kuchangia kabisa mwanamke kutokupata ujauzito au mimba kutoka.
Maeneo ambapo uvimbe unajitokeza yanaweza kuathiri uwezo wa mwanamke kupata ujauzito . Baadhi ya vivimbe vinaweza kuziba mirija ya uzazi au vinaweza kubadiri kabisa umbo la mfuko wa uzazi na kuzuia kiinitete kisiweze kujipachika kwenye mfuko wa uzazi. Ukubwa wa uvimbe wa fibroid pia unaweza kuharibu uwezo wa mwanamke kupata ujauzito. Uvimbe unapofikisha sentimita 4 au zaidi, mwanamke huwa ni vigumu sana kutarajia kubeba ujauzito.
Je, Nini Husababisha Mwanake Kushindwa Kubeba Ujauzito?
Wanawake wenye matatizo ya uvimbe wa fibroid wanaweza kuathiriwa na mambo mengine yanayochangia ugumba au kutokupata ujauzito. Baadhi ya mambo mengine yanayosababisha mwanamke mwenye uvimbe kushindwa kupata ujauzito ni kama haya yafuatayo:
- Mayai kushindwa kupevuka
- Matatizo ya mzunguko wa hedhi
- Vivimbe kwenye mayai
- Mayai kushindwa kukomaa
- Maambukizi ya magonjwa ya zinaa
- Kuharibika kwa mirija ya uzazi
Je, Jinsi Gani Uvimbe Wa Fibroid Unaweza Kumfanya Mwanamke Asipate Ujauzito?
Uvimbe wa fibroid unaweza kuharibu uwezo wako wa kupata ujauzito kwa namna nyingi mbalimbali kama hivi ifuatavyo;
- Mirija ya uzazi inaweza kuziba na kuzuia yai lishindwe kufika kwenye kizazi
- Kubadirika kwa umbo la mlango wa uzazi kutokana uvimbe kunaweza kuathiri kiwango cha mbegu za mwanaume zinazoingia ukeni.
- Kubadirika kwa umbo la mfuko wa uzazi kutokana na uvimbe kunaweza kuzuia mbegu kushindwa kuingia au yai kujipachika kwenye kizazi.
- Ukuta wa mfuko wa uzazi unaweza kuathiriwa na uvimbe
- Mtiririko wa damu kwenye mfuko wa uzazi huathiriwa na uwepo wa uvimbe wa fibroid
Kwa kifupi:
- Uvimbe wa fibroid umekuwa ni wa kawaida na unaweza kuathiri uwezo mwanamke kupata ujauzito. Uvimbe unaweza kuathiri mbegu za mwanaume kushindwa kukutana na yai, pia unaweza kuathiri yai lishindwe kujipachika kwenye mfuko wa uzazi, na pia uvimbe unaweza kuathiri mimba isiweze kuendelea, na mwisho kabisa inaweza kuathiri ujauzito usiweze kukua.
Je, Unahitaji Kupata Huduma?
Tupigie kwa namba hizi: 0752389252 au 0712181626-Arusha Mbauda
Pia unaweza kutuma namba yako ya WHATSSAP au TELEGRAM tukakuunganisha kwenye group letu ili uweze kuendelea kupata elimu juu ya matatizo ya afya.
Karibu sana!