Mwili wako hufanya kazi muda wote. Hata kama umelala, damu yako husafiri kila mahali, ubongo wako hushughulika masaa yote, na tumbo lako la chakula hupumzika ifikapo mida ya usiku unapokuwa umepumzika kitandani mwako.
NUKUU: Unapokula kitu chochote, mwili wako huchambua vitu vizuri vyenye faida mwilini mwako kama vile protini na vitamini, na kisha huondoa makapi yote ambayo ndio uchafu. Hivyo basi, moja ya uchafu huo huwa ni asidi ya yurea. Asidi ya yurea hutengenezwa pale mwili wako unapokuwa ukimeng’enya chembechembe fulani kutoka katika baadhi ya vyakula, lakini pia huonekana pale seli zinapokufa na kisha kuondolewa na kuhifadhiwa pembeni. Asidi nyingi ya Yurea hutoka mwilini mwako pale unapokojoa, na baadhi pale unapoenda haja kubwa na kutoa kinyesi.
Kwahiyo, ikiwa kama una kiwango kikubwa cha asidi ya yurea, inaweza kuwa ishara au dalili ya ugonjwa kama vile jongo(Gout). Hapa ndipo unatakiwa kuhitaji vipimo vya damu, ambavyo hupima ni kiwango gani cha asidi ya yurea ulicho nacho kwenye damu yako. Unaweza pia kusikia kipimo hiki kinachoitwa, “Serum Uric Acid Test, au UA.
Unaweza ukaona hapo juu jinsi kipimo kinavyofanyika hap maabara.
- Gout
Huu ni muundo wa jongo ambapo chembechembe kutoka kwenye asidi ya yurea hujengeka kwenye viunganishi vya mifupa yako na kusababisha maumivu makali sana. Mara nyingi hali hii unaweza kuuhisi kwenye vidole gumba vyako, lakini unaweza kuyahisi kwenye viwiko vya mikono, miguuni, kwenye magoti, pamoja na kiunoni.
NUKUU: Maumivu haya yanaweza pia kusababisha uvimbe, wekundu fulani kwenye eneo la ngozi, na maumivu kwenye viunganishi vya mifupa hivyo, yanaweza kukufanya ushindwe hata kutembea.
- Mawe Kwenye Figo
Hivi huwa ni vitu vidogo vidogo vigumu kama mawe, ambavyo hujengeka kwenye figo zako wakati unapokuwa na kiwango kikubwa cha asidi ya yurea.
NUKUU: Mawe kwenye figo yanaweza kusababisha maumivu makali kiunoni mwako ambayo huja na kuondoka, damu kwenye mkojo, mchafuko wa tumbo, na kuhisi kukojoa hata kama huna mkojo.
TIBA ZAKE
James Herbal Clinic tuna tiba nzuri zenye uwezo mkubwa wa kuondoa matatizo haya ya asidi ya yurea, nazo ni MULTICURE POWDER, FRESH HERB na CARD HERB.
Je, unahitaji huduma? Tupigie kwa namba zifuatazo:
Arusha Mbauda: 0752 389 252 au 0712 181 626
Njombe-Makambako: 0744 531 152 au 0716 158 086
Karibuni sana!
You too