Kipimo cha damu ya uzazi hutumika kupima kiwango chako cha homoni na mara nyingi huwa ni kipimo cha kwanza kabisa ambacho daktari wako atakuelezea kama unashindwa kupata ujauzito na kuhisi kuwa huenda una tatizo la ugumba.
Matokeo ya kipimo cha uzazi kwanza hutumiwa ili kupima visababishi vya homoni katika ugumba. Kipimo cha damu huchukuliwa siku za mwanzo za mzunguko wako wa hedhi(yaani siku ya 2-5) na kisha kupima kiwango cha homoni inayosimamia utengenezaji wa yai(Follicle Stimulating Hormone au FSH), homoni inayochochea nguvu katika upevushaji wa yai(Leutenizing Hormone au LH) na wakati mwingine homoni ya prolactin.
NUKUU: Ni njia rahisi ya kugundua kwanini wakati mwingine unapata ujauzito, na wakati mwingine usipate? Na hiki ndio kitakuwa kielelezo tosha cha chanzo cha tatizo. Vipimo vya damu mara nyingi hufanywa pamoja na vipimo vya manii ambayo humuwezesha daktari wako kugundua huenda tatizo linatokana na uzazi wa mwanamke au mwanaume.
- Kiwango Cha LH na FSH
Kubainisha uwiano sawa kati ya homoni inayosimamia utengenezaji wa yai(Follicle Stimulating Hormone) na homoni inayochochea nguvu katika upevushaji wa yai(Luteinizing Hormone) itamfanya daktari kuweza kugundua kama una vivimbe vingi vidogovidogo kwenye vifuko vya mayai(Polycystic ovarian syndrome au PCOS). Uwiano sawa wa homoni inayosimamia utengenezaji wa yai(Follicle Stimulating Hormone) na homoni inayochochea nguvu katika upevushaji wa yai(Luteinizing Hormone) unapaswa kuwa 1:1 na kama kiwango cha homoni inayochochea nguvu katika upevushaji wa yai(Leutenizing Hormone) kiko mara mbili zaidi ya kile cha homoni inayosimamia utengenezaji wa yai(Follicle Stimulating Hormone), basi hali hii inaweza kuonyesha uwiano wa homoni kuwa hauko sawa(Hormone Imbalance) ambao mara nyingi hugundulika kwenye vivimbe vinavyojitokeza kwenye vifuko vya mayai(Polycystic Ovarian Syndrome). Ikiwa kama kuna sababu ya kuamini kwamba hili ni tatizo, basi hatua inayofuata ni kupima kwa Ultrasound ili kuthibitisha kipimo.
- Kiwango Cha Prolactin
Tofauti na homoni zingine, kiwango cha prolactin kwenye damu yako kinaweza kugunduliwa kwa namna yoyote kwenye mzunguko wa hedhi. Kwa kawaida kiwango kikubwa cha homoni ya prolactin kinaweza kusababisha matatizo ya upevushaji mayai kwa mwanamke.
- Kupima Nguvu Uwezo Wa Vifuko Vya Mayai
Kipimo cha uwezo au nguvu za yai hutolewa kwa wanawake wanaohitaji tiba kwa ajili ya uzazi kama vile njia itumikayo kurutubisha yai kwa mbegu za mwanaume kwa kutumia test tube mahali popote nje ya mwili( In Vitro Fertilization au IVF). Nguvu ya yai inaweza kukadiriwa huenda kwa kipimo cha viwango vya homoni inayosimamia utengenezaji wa yai(Follicle Stimulating Hormone) au AMH.
NUKUU: Madaktari wanaweza kutumia uwezo wa yai ili kuonyesha jinsi unavyoweza kukubariana na matibabu yanayotumika ili kuchochea mayai yako kwa njia ya kurutubisha yai kwa mbegu za mwanaume kwa kutumia test tube mahali popote nje ya mwili( In Vitro Fertilization au IVF)
- Upimaji Wa Homoni Ya Progesterone Kupitia Damu
Upimaji wa homoni ya progesterone kupitia damu kwa kawaida hufanywa katikati ya hatua ya luteal, hali hii itamsaidia daktari wako kuona kama yai lako limepevuka au kama mabaki ya yai(corpus luteum) yanatengeneza viwango vya homoni ya progesterone vinavyotarajiwa.
NUKUU: Homoni ya progesterone huandaa mji wa mimba kwa ajili ya kushikiza yai lililorutubishwa. Kipimo mara nyingi hukadiriwa kwenye siku ya 21(ambayo ni wiki tatu), lakini hii itategemeana na urefu gani mizunguko yako ya hedhi ilivyo na lini yai lako hupevuka katika mzunguko wako wa hedhi.
- Kupima Homoni Ya Thyroid Kupitia Damu
Kipimo hiki cha damu kinaweza kufanywa kwa namna yoyote katika mzunguko wako wa hedhi.Viwango visivyo vya kawaida vya homoni ya thyroid(TSH), vinaweza kuathiri mzunguko wako wa hedhi na nafasi zako za kupata ujauzito. Kama tatizo likionekana, basi matibabu yanaweza kufanyika ili kusaidia viwango vya thyroid ambavyo vitarejesha uwezo wa kupata ujauzito.
- Vipimo Kwa Ajili Ya Maambukizi Ya Magonjwa Ya Zinaa
Maambukizi ya pangusa(Chlamydia) yanaweza kuharibu mirija ya uzazi na kuzuia yai kusafiri kwenye mrija, hali ambayo inaweza kupunguza kabisa viwango vya mwanamke kupata ujauzito.
NUKUU: Kama kipimo cha damu kitaonyesha kiwango kikubwa cha vimelea vya ugonjwa wa pangusa, basi mnashauriwa mume na mke kupata matibabu haraka sana.
Je, unahitaji kupata huduma? Tupigie kwa namba: 0752389252 au 0712181626
Arusha-Mbauda
Karibuni sana
Ikiwa mwanamke amebeba ujauzito kipimo hicho kinapofanyika anaweza kugundulika kuoitia uchunguzi huo?
Aisha ni mapaka upate vipimo kwanza
Ikiwa mwanamke amebeba ujauzito kabla ya kufanyiwa kipimo hicho kuna uwezekano wa kugunduliwa au hakuna? Naombeni jibu
Ni vigumu kugunduliwa ni mpaka pale utakapopata vipimo
Naomba kuuliza je hormone in balance inagundulika kwa kutumia kipimo gani
Au ni kwa maelezo tu unayompatia doctor
Hata ultrasound inaonyesha pia au kupitia kipimo cha damu
Jee kipimo cha ujauzito cha mkojo kikionesha positive halaf huna mimba ndio una hili ttzo
Vipimo vya damu vinagarimu shingap na mbona wengne wanasema Hadi kipimo Cha damu na Wala sio ultrasound
Magreth unapima damu kwa ajili ya nini?