JE, WAJUA CHANZO CHA KUVURUGIKA KWA MZUNGUKO WA HEDHI?

 

Mzunguko wa hedhi umegawanyika katika maeneno makuu mawili;

  • Upevushaji mayai(Ovulatory Circle)
  • Kutopevusha mayai(Anovulatory Circle)

Mzunguko wa mwanamke unaopevusha mayai unatoa ute wa uzazi unaovutika kama ute mweupe wa yai la kuku, na anaweza kupata ujauzito.

Mzunguko Wa Mwanamke Usiopevusha Mayai

Mwanamke hawezi kupata ujauzito ingawa katika mizunguko yote hiyo miwili mwanamke anapata damu ya hedhi kama kawaida. Mwanamke ambaye mzunguko wake hapati ute wa uzazi, hawezi kupata ujauzito. Hii inatokana na mabadiriko katika mfumo wake wa homoni.

Kwa kawaida ute wa uzazi umegawanyika katika makundi matatu, nayo ni;

  • Ute mwepesi
  • Ute unaovutika
  • Ute mzito

Mwanamke asiyepevusha mayai hawezi kupata ujauzito, hivyo hapati ute wa uzazi. Wengine hupata ute mzito daima kama uchafu fulani unaotoka ukeni hauna halufu wala muwasho.

Kuvurugika kwa mzunguko  maana yake inamaanisha mwanamke hapati siku zake katika utaratibu unaoeleweka.

Jinsi Ya Kutambua Mzunguko

 

Mzunguko wa hedhi uwe umepevusha mayai au haupevushi, nao umegawanyika katika mizunguko midogo mitatu, nayo iko kama ifuatavyo:

  • Mzunguko mfupi ambao ni siku 22-27
  • Mzunguko wa kawaida ambao ni siku 28-30
  • Mzunguko mrefu ambao ni siku 31-35

Kila mwanamke ana mzunguko wake, nafikiri makala zilizopita tuliwahi kuelekezana.

Faida Za Kufahamu Mzunguko Wa Hedhi

Kufahamu vizuri mzunguko wa hedhi kunasaidia mambo yafuatayo;

  • Kupanga uzazi na kuepuka kutumia dawa za kupanga uzazi ambazo wengine huwaathiri ki afya.
  • Kupangilia jinsia ya mtoto unayeweza kumpata, kama unataka kuchagua mtoto wa kike au wa kiume.

Ili kufahamu mzunguko wako ukoje, ni vyema kutumia kalenda na ukahesabu siku ya kwanza ni ile unayoona damu, na siku ya mwisho ni siku moja kabla hujaona damu kwa mwezi unaofuata. Kwa mfano; damu kwa mwezi uliopita umeona tarehe 3, na mwezi huu umeona tarehe kumi, unahesabu kuanzia tarehe 3 mwezi uliopita hadi tarehe 9 mwezi huu.

Chanzo Cha Kuvurugika Kwa Hedhi

 

Kuvurugika kwa mzunguko wa hedhi kunaweza kusababishwa na mambo yafuatayo:

  • Hofu au wasiwasi
  • Kuwa na hamu ya kupata ujauzito
  • Matumizi ya madawa ya vidonge vya mpango wa uzazi, nk.

Mwanamke mwenye hamu sana ya kupata mimba anaweza kajikuta anapata siku zake au anakosa lakini hana mimba, pia anayehofia kupata mimba anajikuta anapitiliza siku zake lakini hana mimba. Naomba mpendwa unayesoma ulitambue hilo pia.

Chanzo kingine ni mabadiriko ya kimwili, hii inatokana na mambo yafuatayo:

  • Kubadirisha hali ya hewa,
  • Matumizi ya baadhi ya madawa, hasa dawa za homoni, mfano vidonge na sindano za homoni, vidonge na sindano za kupanga uzazi, na baadhi ya dawa za tiba ambazo zina kemikali.

Magonjwa pia yanaweza kuleta mabadiriko mwilini, mfano magonjwa ama matatizo katika mfumo wa uzazi. Magonjwa sugu yanayoweza kuathiri mfumo wa homoni mwilini mfano, maambukizi ya HIV, uvimbe ndani ya kizazi, kisukari, moyo, nk.

Dalili Zake

Mwanamke ambaye mzunguko wake haueleweki hawezi kupata ujauzito au atapata ujauzito bila kutarajia, hali hii husababisha siku zisitokee kwa mpangilio, wengine hulalamika Maumivu ya tumbo chini ya kitovu ama Maumivu makali wakati wa hedhi. Hali ya kuvurugika kwa mzunguko wa hedhi huambatana na uwepo wa matatizo mengine ya uzazi, damu inaweza kutoka nyingi au kidogokidogo kwa muda mfupi au mrefu.

Tiba Yake

James Herbal Clinic tuna dawa nzuri za asili zenye uwezo wa kuondoa matatizo haya, nazo ni PHYTOGUARD, REDEEMR na CARD HERB.

Kwa mawasilino tupigie kwa namba zifuatazo: 0752389252 au 0712181626