Hii huwa ni ile hali ya tezi dume kuathirika kutokana na vyanzo mbalimbali kwa mfano; bakteria, nk. Kuathirika kwa tezi dume kunaweza kusababisha hata utendaji kazi wake kupungua, na inapatikana chini ya kibofu cha mkojo na kazi yake kubwa ni kuzarisha manii kwaajili ya kurutubishana kusafirisha mbeguza kiume kutoka kwenye korodani. Tatizo hili linawaathiri wanaume wengi bila kujali lika lakini wanaume kuanzia miaka 50 wameonekana kuathiri zaidi na hili la tatizo.
CHANZO CHA TATIZO
Chanzo kikubwa cha tatizo hili nikushambuliwa kwa tezi dume na bakteria mbalimbali ambao wanaweza kuwa ni visababishi vya magonjwa mbalimbali ya zinaa mfano, kaswende, kisonono, pangusa, au bakteria wanaoshambulia mfumo wa mkojo (UTI), wanaweza kupenya na kufikia tezi dume na kuishambulia. Vyanzo vingine ni kushuka kwa kinga za mwili na ajali zinazopelekea kuumia katika eneo ambalo tezi dume ipo, pia kuna mazingira hatarishi yanayopelekea mwanaume kuathirika na hili tatizo. Ikiwa kama mwanaume aliwahi kupata tatizo hili na hajawahi kupata matibabu sahihi au;
- Kuwa na maambukizi katika kibofu cha mkojo au mrija unaotiririsha mkojo(urethra),
- Kutokunywa maji ya kutosha,
- Kuwa na wapenzi wengi na kushiriki tendo la ndoa na mpenzi mwenye maambukizi ya magonjwa ya zinaa na HIV/AIDS.
DALILI ZAKE
Dalili za tatizo hili kwa kawaida huwa kama ifuatavyo;
- Maumivu wa katiwa kutoa haja ndogo au kuhisi kama mkojo ni wa moto na Maumivu wakati wa kufika kileleni.
- Kwenda haja ndogo mara kwa mara
- Mtiririko wa mkojo kuwa dhaifu
- Maumivu chini ya kitovu
- Maumivu ya kiuno na chini ya mgongo
- Maumivu ya sehemu ambayo iko katikati ya korodani na sehemu ya kutolea choo kubwa
- Maumivu ya korodani na uume
- Homa za mara kwa mara.
JE, NINI MADHARA YAKE?
Madhara makubwa yatokanayo na ugonjwa huu huwa kama ifuatavyo:
- Kusambaa kwa bakteria mbalimbali katika damu
- Kuwa na jipu kwenye tezi dume(prostatic abscess)
- Ugumba kutokana na kuathirika kwa manii na mbegu za kiume.
Tatizo hili linapokosa suluhisho linaweza kusababisha kansa ya tezi dume.
James Herbal Clinic tuna tiba asili zenye uwezo wa kuondoa tatizo la tezi dume. Unahitaji huduma tafadhari tupigie: 0752389252 au 0712181626