JE, WAJUA CHANZO, DALILI ZA MADHARA YA KUKOSA CHOO(CONSTIPATION)?

 

Je, kukosa choo ni nini?

 

Kukosa choo maana yake ni kutokuwa na uwezo wa kwenda haja kubwa kutokana na kinyesi kukusanyikana sehemu moja tumboni na kuwa kigumu na kushindwa kutoka.

Kwa kawaida kinyesi tumboni kinapaswa kutoka kila siku kila baada ya kupata mlo, iwe ni mlo wa asubuhi, mchana au jioni. Hivyo, kila mtu anapaswa apate choo mara 2-3 kila siku. Lakini hali hii inapokosekana, vitu vibaya au vichafu pia huanza kusafiri taratibu na kuingia katika utumbo mpana. Utoaji kinyesi huwa wenye maumivu sana pindi muhusika anapoenda chooni kujisaidia, na hivyo sumu hunyonywa tena na kurudi tumboni, na kusababisha mzigo mkubwa katika utendaji kazi wa ini na figo. Na ieleweke kuwa, uchafu wote katika mwili wa mwanadamu unapaswa uondolewe ndani ya masaa 18-24 tu!!

Napenda kila mmoja wetu tuelewe kuwa, matatizo mengi ya magonjwa mbalimbali mara nyingi yamekuwa yakisababishwa na hali ya kukosa choo kutokana na milo yetu, kwa mfano:

 

  • Kutokwa na harufu mbaya mdomoni,
  • Mwili kutoa harufu, tumbo kujaa gesi, kichwa kugonga, mshipa wa ngiri,
  • Mishipa ya damu kuwa migumu na kusababisha shinikizo la juu la damu na miguu au mikono kufa ganzi,
  • Mwili kuwa mnene,
  • Kukosa usingizi, maumivu ya kiuno, mwili kuchoka,
  • Chakula kushindwa kurudiwa kumeng’enywa mara ya pili, na ulimi kuwa na utando mweupe.

Sumu inayonyonywa mara ya pili kutoka kwenye kinyesi kinachoshindwa kutoka tumboni, inaweza pia kusababisha hali ya kipanda uso, tumbo kujaa gesi mara kwa mara na kulifanya kuunguruma na hivyo kujamba hewa yenye harufu mbaya, homa ya uti wa mgongo au vimbe wa tando za uti wa mgongo na ubongo, nk.

 

Je, Nini Husababisha Kukosa Choo?

 

 

Kwa kawaida tatizo hili mara nyingi husababishwa na ulaji wa vyakula aina zifuatazo:

  • Vyakula vilivyokobolewa kama vile, ugali wa sembe, unga wa ngano(maandazi, chapatti, nk)
  • Chips mayai na juisi
  • Nyama nyekundu(mishikaki, supu, nk)hasa inapoliwa kwa mfululizo)
  • Vyakula vilivyosindikwa

 

 

 

Hali ya kukosa choo yaweza kuwa ya kawaida kwa mama mjamzito, nitaeleza baadaye pia kuhusu hali hii kwa mjamzito.

Watu wenye umri mkubwa au wazee mara nyingi hupatwa na tatizo la kukosa choo kutokana na mazoea ya kutokunywa maji mengi kwa siku.

 

Dalili Zake

 

Kwa kawaida dalili za tatizo hili huwa kama ifuatavyo:

  • Kinyesi kuwa kigumu, kikavu na sio cha mara kwa mara
  • Mchafuko wa tumbo
  • Mwili kuishiwa nguvu
  • Kichwa kugonga
  • Kukosa hamu ya kula
  • Maumivu ya kiuno.

 

 

 

Je, Nini Madhara Ya Kukosa Choo?

 

Madhara ya kukosa choo kwa muda mrefu kawaida huwa kama ifuatavyo:

  • Kuota nyamanya sehemu za njia ya haja kubwa, yaani bawasiri(haemorrhoid).
  • Kukosa hamu ya kula
  • Ini na figo kushindwa kufanya kazi vizuri
  • Mishipa ya damu kukakamaa au kuwa migumu na kusababisha matatizo ya moyo.
  • Saratani ya utumbo mpana

 

Tiba Zake

 

James Herbal Clinic tuna tiba nzuri zenye uwezo mkubwa wa kuondoa matatizo ya kukosa choo, nazo ni NEOTONIC, na CARD HERB.

Unahitaji huduma tunaomba utupigie kwa namba zifuatazo:

Arusha: 0752389252 au 0712181626