Hii ni aina ya vivimbe vinavyoota kwenye misuli laini ya mfuko wa uzazi.
Tatizo hili huwakumba wanawake wengi ambapo huwapata kwa 5% wanawake wenye umri wa miaka 20-30 na 20% kwa wanawake wenye umri wa miaka 30-40 na zaidi ya 40% ni kwa wale wenye umri zaidi ya 40 hivyo kwa ujumla tatizo la fibroids huwapata wanawake wengi hasa katika umri wa kuzaa (reproductive age). Hii inamaana kuwa kadri umri unavyokuwa mkubwa mwanamke ana nafasi kubwa ya kupata uvimbe.
Tafiti zinaonyesha kuwa tatizo hili huwapata zaidi wanawake wa kiafrika kuliko wazungu pia, huwapata zaidi wanawake ambao hawajazaa kabisa au wale ambao wamekaa Muda mrefu Bila kuzaa, pia wanawake wanene, na wale waliopata hedhi mapema wapo katika hatari ya kupata ugonjwa huu
Aina Kuu Za Fibroids.
- Submucosal Fibroids: Hii hutokea ndani ya kizazi
- Intramural Fibroids: Hii hutokea ndani ya nyama ya kizazi
- Subserol Fibroids: Hii hutokea nnje kwenye ukuta wa kizazi
Uvimbe huwa na ukubwa tofauti kwani huanza mdogo na baadae kuwa mkubwa sana na hata wakati mwingine mwanamke huweza kuonekana mjamzito, kwani uvimbe huu huweza kuwa mmoja mkubwa na wakati mwingine huwa zaidi ya mmoja na kutanda katika mfuko wa kizazi
Watu wengi wamekuwa wakihisi uvimbe wa fibroids kuwa ni kitu ambacho sio kweli kwasababu fibroids sio kansa bali ni uvimbe wa kawaida ambao hukua kwa kutegemea kichocheo au hormone ya Istrojeni na ndio maana wakati wa kupata tatizo hili huwa ni kipindi cha kubalehe mpaka kukoma kwa hedhi.
Je, Nini Visababishi Vyake?
Kuna sababu ambazo huweza kusababisha mwanamke kupata fibroids, nazo ni kama ifuatavyo:
- Wingi wa homoni ya Istrojeni ambayo ipo katika mwili wa mwanamke na ndiyo hufanya kazi ya kusababisha mwanamke kupata hedhi, pia mara nyingi uvimbe huu hukua mkubwa sana kipindi cha ujauzito kwasababu vichocheo vya Istrojeni huongezeka na kuwa vingi ili kulinda makuzi ya mtoto, pia ni mara chache watu walio kikomo cha hedhi kupata fibroids na wakipata kuna hatari ya kuwa kansa.
- Matumizi ya madawa ya majira wa uzazi wa mpango, nk.
Dalili Zake
Dalili za uvimbe katika kizazi cha mwanamke hushindwa kuonekana iwapo uvimbe ni mdogo na pia dalili hutegemea sehemu ilipo kwenye mfuko wa kizazi. Dalili hizi huwa kama ifuatavyo:
- Kutokwa na damu yenye mabonge kwa muda mrefu
- Kutokwa na damu katikati ya mwezi na hedhi kutokuwa na mpangilio
- Kupata Maumivu ya kiuno hasa wakati wa hedhi
- Kupata Maumivu makali wakati wa tendo la ndoa
- Maumivu ya mgongoni
- Kukojoa mara kwa mara
- Mimba kuharibika mara kwa mara
- Kupungukiwa na damu mara kwa mara
- Miguu kuvimba
- Mkojo kubaki kwenye kibofu
- Haja kubwa kuwa ngumu
- Ugumba
Je, Nini Madhara Makubwa Ya Fibroids?
Uvimbe huu usipotibiwa na kuondolewa chanzo chake, mwanamke humpatia madhara yafuatayo:
- Husababisha mimba kutoka mara kwa mara na hatimaye mtu kuwa mgumba,
- Husababisha salatani ya shingo ya kizazi
NUKUU: Ndugu rafiki hakikisha unaenda kupima Afya yako kila mwezi ili kujua maendeleo ya Afya yako kwani wengi huwa hawajitambui kuwa wana tatizo hili la fibroids.
Kwa mawasiliano tupigie kwa namba zifuatazo: 0752389252 au 0712181626
Karibu sana kwa maswali, na maoni.