Hali ya kujaa maji kwa mirija ya uzazi ya wanawake huitwa kitaalamu huitwa, “hydrosalpinx”. Ni tatizo ambalo hujitokeza kwa wanawake kutokana na maambukizi ya magonjwa ya zinaa ambayo yamekaa muda mrefu bila kutibiwa, kama vile kisonono, pangusa, malengelenge, nk, ambayo kwa ujumla tunaweza kuita maambukizi katika via vya uzazi yaani PID (pelvic inflammatory disease), bila shaka tutayazungumzia baadaye katika makala zinazofuata kwa kuchanganua ugonjwa mmoja baada ya mwingine na tutaona madhara yake na dalili zake pia. Mara nyingi matatizo haya husababisha tatizo la ugumba na maumivu ya kiuno.
NUKUU: Mirija ya uzazi hujishikiza kwenye upande wa kulia na kushoto wa tumbo la uzazi, nao hupitisha mayai kila mwezi kutoka kwenye ovari ama kifuko cha yai, kwenda kwenye mji wa uzazi. Urutubishaji wa yai la uzazi hutokea katika mirija hii.
Je, Nini Cahanzo Cha Mirija Ya Mayai Kujaa Maji
Mara nyingi mirija ya uzazi kuziba hutokana na magonjwa yafuatayo;
- Maambukizi katika via vya uzazi au PID(Pelvic inflammatory disease)
- Maambukizi ya magonjwa ya zinaa ambayo yamekaa muda mrefu bila kutibiwa kama vile kisonono na klamidia au pangusa.
- Upasuaji maeneo ya kiunoni (pelvic surgery)
- Saratani ya mirija ya uzazi, nk.
Je, Dalili Zake Zinakuwaje?
Wanawake wengi wanaweza wasiwe na dalili zozote, isipokuwa kupata matatizo katika kupata mtoto. Dalili zinazojitokeza mara nyingi huwa ni;
- Maumivu ya kiuno, nayo hujitokeza mara kwa mara hasa siku chache kabla au baada ya kuingia kwenye hedhi.
- Uchafu kutoka sehemu za siri.
- Kutokushika ujauzito
Je, Unawezaje Kuligundua Tatizo Hili?
Kuna vipimo kadhaa vya kuwezesha kujua kama mirija yako ya uzazi imeziba na kujaa maji, nayo ni;
- Hysterosalpingogram(HSG)
Hii ni aina maalumu ya X-ray ya kiuno, ambayo kimiminika maalumu huingizwa ndani ya mji wa uzazi kwa kupitia shingo ya uzazi.
Kama mirija haijaziba, kimiminika huweza kupita mpaka ndani ya kiuno na kama imeziba, kimiminika hicho hushindwa kupita. Hii itaonekana kwenye hiyohysterosalpingogram
- Ultrasound Ya Kiunoni (Pelvic Ultrasound)
Ultrasound itaweza kuonesha kama mirija yako imeziba na kujaa, na ukubwa wake. Pia itaweza kuonesha kama kuna matatizo mengine kwenye via vya uzazi vya ndani.
- Upasuaji wa Tumbo(Laparoscopy):
Upasuaji huu hufanyika kwa kutumia mirija maalumu yenye kamera ili kutazama mirija hiyo. Matundu mawili hutobolewa tumboni ili kupitisha mirija hii.
Tatizo Hili Likitibiwa, Je, Mama Anaweza Kupata Ujauzito?
NUKUU: Na ieleweke kuwa, tatizo hili likitibiwa unaweza ukapata ujauzito. Lakini pale mirija inapokuwa imeharibika sana uwezekano wa kupata ujauzito huwa ni mdogo kwa mwanamke.
Je, Nini Madhara Ya Mirija Inapojaa Maji?
Mirija ya uzazi ikiziba, mayai ya uzazi hushindwa kusafiri kutoka kwenye ovari kwenda kwenye mji wa uzazi. Hivyo, mwanamke hupatwa na madhara yafuatayo:
- Tatizo la ugumba hujitokeza.
- Mimba kutunga nje ya mfuko wa mimba (Ectopic pregnancy)
- Maumivu ya kiuno
- Kusinyaa kwa uke na kushindwa kufanya tendo la ndoa(Vaginal Atrophy).
- Kukosa hamu ya tendo la ndoa
- Kuwa mkavu ukeni, na
- Kuhisi maumivu makali wakati wa tendo la ndoa.
TIBA ZAKE
James Herbal Clinic tuna dawa za asili zenye uwezo wa kuondoa tatizo hili bila kufanya upasuaji kwani zina uwezo wa kunyonya majimaji yanayosababisha mirija kutuna, pia vimelea wote wanaosababisha tatizo hilo. MULTI-CURE POWDER, FRESH HERB, na NEOTONIC.
Je, unahitaji huduma? Tupigie kwa namba hizi: 0752389252 au 0712181626
Arusha-Mbauda