Hili ni taitizo ambalo huwakumba wanawake wengi katika nyakati tofautitofauti. Mwanamke hutokwa na damu nyingi wakati wa hedhi pia inaweza kudumu kwa wiki moja na zaidi. Mwanamke mwenye tatizo hili anapokuwa kwenye kipindi cha hedhi hushindwa kufanya kazi zake za kawaida kwa siku kwasababu hutokwa na damu nyingi na kupatwa na vichomi kama vile chango la uzazi. Hali hii isipopatiwa ufumbuzi huweza kuleta madhara makubwa sana kwa mwanamke ambayo hupelekea vifo.
Dalili Zake
Kwa kawaida dalili za tatizo hili mara nyingi huwa kama ifuatavyo:
- Kutumia pedi 1 au zaid kila saa kwa mfululizo wa masaa kadhaa.
- Kutokwa na damu kwa muda mrefu, zaidi ya siku 8 wakati wa hedhi.
- Uhitaji wa kuamka usiku kubadili pad.
- Kutoshiriki shughuli za kila siku kutokana na damu nyingi kutoka
- Kutokwa na mabonge makubwa ya damu
- Kuchoka sana
- Kupungukiwa damu mwilini
- Kizunguzungu
- Tumbo kuuma
- Dalili za kuishiwa damu, kama kuchoka, ama kupumua kwa shida.
Visababishi Vyake
Kwa upande mwingine naweza kusema kwamba visababishi vya tatizo hili havijaeleweka bado, lakini zipo hali ambazo husababisha tatizo hili nazo ni kama ifuatavyo:
- Kubadirika Uwiano Wa Vichocheo(Hormone Imbalance): Katika mzunguko wa kawaida wa hedhi, uwiano katika vichocheo vya estrogen na progesterone hurekebisha utando unaokuwa kwenye ukuta wa kifuko cha kizazi(endometrium), ambao huambuliwa wakati wa kipindi cha hedhi. Inapotokea hali ya kubadirika kwa uwiano wa vichocheo hivi, ukuta wa kizazi huendelea kuvimba na hatimaye hujiumbua kwa njia ya kutokwa na damu nyingi wakati wa hedhi. Hali mbalimbali zinazoweza kusababisha kuvurugika kwa vichocheo ni vifuko vya mayai kuwa na vivimbe, unene,au matatizo ya insulin.
- Matatizo Ya Ovary: Ovari ni sehemu muhimu sana katika katika kuandaa na kukuza yai na badae kutolewa likiwa kamili kuingia katika mirija ya mayai tayari kwa safari kuelekea mfuko wa kizazi. Ikiwa kifuko cha yai cha mwanamke kinaposhindwa kuachia yai wakati wa hedhi, mwili hushindwa kuzarisha homoni za progesterone kama inavyozarisha wakati wa mzunguko wa hedhi wa kawaida. Hali husababisha kuvurugika kwa homoni(hormone imbalance) na inaweza kusababisha kutokwa na damu nyingi wakati wa kipindi cha mzunguko wa hedhi.
- Uvimbe kwenye shemu ya kizazi (Fibroids): Fibroids siyo saratani bali huwa ni uvimbe wa kawaida ambao hubaki sehemu moja (benign), ambayo hutokea katika umri wa uzazi. Na hii husababishwa na vichocheo kutokuwa katika usawa(Hormone Imbalance) na huweza kusababisha damu nyingi kutoka wakati wa hedhi.
- Uvimbe Katika Mlango Wa Kizazi(Adenomyosis): Hali hii pia hujitokeza wakati tezi zinazokuwa kwenye ukuta wa kizazi zinapokuwa ndani ya msuli wa kifuko cha kizazi, mara nyingi husababisha kutokwa na damu nyingi na maumivu makali wakati mwanamke anakuwa hedhini.
- Saratani Ya Shingo Ya Kizazi(Cervix Cancer): Salatani ya shingo ya kizazi inaweza kusababisha kutokwa na damu nyingi wakati wa kipindi cha hedhi, hasa mwanamke anapokuwa ameshakoma hedhi.
- Magonjwa ya kurithi: Matatizo ya damu kutoganda kutokana na hii husababishwa na ukosefu wa vigandishi vya damu.
MADHARA YAKE
Tatizo hili lisipotatuliwa mapema husababisha madhara yafuatayo:
- Upungufu wa madini ya chuma ambayo ni madini muhimu katika damu ambapo husaidia katika kubeba hewa ya oksijeni, kukosekana ama kupungua kwake maisha huwa hatarini.
- Maumivu makali wakati wa hedhi ambayo wakati mwingine huhitaji kutumia dawa za kutuliza maumivu hayo.
- Mwili wa mwanamke huhitaji uangalizi wa hali ya juu.
James Herbal Clinic tunapenda kushauri kuwa uonapo dalili za tatizo hili tafadhali fika katika hospitali za wilaya ama Mkoa, onana na madaktari wa kinamama ili upate vipimo.
MATIBABU
James Herbal Clinic tuna tiba za asili zenye mchanganyiko wa vyakula vya matunda na mbogamboga na asali, ambazo zina uwezo mkubwa wa kuondoa tatizo hili. Unahitaji huduma tupigie: 0752389252 au 0712181626