JE, WAJUA VYANZO, DALILI NA MADHARA YA UGONJWA WA PANGUSA(CHLAMYDIA)?

 

JE, WAJUA VYANZO, DALILI NA MADHARA YA UGONJWA WA PANGUSA(CHLAMYDIA)?

 

Pangusa ama kitaalamu wanaita Chlamydia trachomatis, ni ugonjwa  wa zinaa wa kawaida  kabisa, nayo huwa ni maambukizi yanayosababishwa na bacteria aina ya pathogen ambao wanaweza kuharibu mlango wa kizazi ama shingo ya kizazi(cervix) wa mwanamke, mrija wa mkojo pamoja na njia ya haja kubwa pande zote mbili, kwa wanawake na kwa wanaume pia. Kwa kawaida sehemu zingine za mwili hasa sehemu za kope za macho, koo na njia ya haja kubwa zinaweza kuathiriwa na ugonjwa huu. Huu ni miongoni mwa magonjwa yanayosababisha PID, umekuwa ukisumbua wengi sana katika jamii.

Tukiangalia tunaona taarifa hutolewa kila mwaka ya zaidi ya wagonjwa milioni 90 wanaopatwa na maambukizi ya ugonjwa huu. Takwimu inaonyesha kuwa vijana wengi wa kike na wakiume hupatwa na maambukizi haya, lakini pia hata watu wazima wenye umri wa kati. Takribani ya nusu ya wanaume na wanawake wengi walioathiriwa na ugonjwa wa Pangusa, huwa hawaoni dalili zozote zinazosababisha ugonjwa usiweze kutibika na kumuambukiza mwenza kirahisi. Ugonjwa wa pangusa unaweza kutibika kwa urahisi kabisa kwa kutumia NEOTONIC NA REDEEMER, vinginevyo kunaweza kukawepo madhara makubwa katika mfumo wa uzazi wa mwanamke kama vile PID na hata ugumba.
Je, Ugonjwa Huu Huambukizwaje?

 

Ugonjwa wa pangusa huambukizwa kupitia njia ya kujamiiana. Zifuatazo ni njia za kawaida kabisa;

  • Sehemu za uke, mlango wa kizazi, uume au kinywa ikiwa kama kitaingia katika maeneo hayo, nikimaanisha kwamba ugonjwa huu pia unaweza kukupata hata kama uume au ulimi haujaingia sehemu za uke.
  • Kufanya mapenzi bila kutumia kinga
  • Bakteria wanaweza kusafiri kutoka ukeni na kuingia katika njia ya haja kubwa ya mwanamke hasa wakati anapojisafisha kwa kutumia toilet paper.
  • Kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto mchanga wakati wa kujifungua.
  • Maambukizi haya pia yanaweza kupatikana kupitia vidole vya mikono hasa unaposhika sehemu za uke kwa kuzichezea, hivyo yawezekeana mwanaume ukapatwa na maambukizi haya kupitia vidole hata kama hujajamiiana na mwanamke, kwa mfano ugonjwa wa pangusa unaweza ukaonekana katika kope za macho. Unaweza ukashikashika sehemu za uke za mpenzi wako ambaye tayari ana maambukizi hayo, halafu ukamuacha bila kujamiiana naye, lakini ukasahau kusafisha mikono yako na baadaye ukashika sehemu zako za macho, hivyo bakteria hao, watahamia machoni na kusababisha  maambukizi katika kope za macho.

 

 

Dalili Za Ugonjwa Wa Pangusa(Chlamydia)

                                                                       

Pangusa inaonekana kuwa ni ugonjwa unaoingia kimyakimya ambao unaweza usioneshe dalili kwa muda mrefu. Inakadiriwa kuwa asilimia 70%-95% ya wanawake na asilimia 50% ya wanaume wenye ugonjwa wa pangusa huwa hawaoni dalili za ugonjwa wa pangusa hata kidogo. Wakati mwingine dalili zinaweza kuwa za kawaida tu ambazo muhusika anaweza kwenda kupimwa akaambiwa mkojo mchafu ama UTI au wakati mwingine zisionekane. Sababu nyingine kwanini dalili zaweza kuwa sio njia sahihi za kuonyesha maambukizi ya ugonjwa huu ni kwamba, dalili zake zinafanana na ugonjwa wa kaswende.

 

Dalili Za Ugonjwa Wa Pangusa Kwa Wanawake:

 

  • Kutokwa na uchafu ukeni, wakati mwingine waweza kuwa wenye rangi ya njano na wenye harufu mbaya.
  • Kuhisi Maumivu na kukojoa mara kwa mara.
  • Kupata hedhi mara mbili ndani ya mwezi mmoja ama kabla ya wakati wake, au kupata hedhi yenye damu nyingi kwa muda mrefu(yawezekana kuwa siku 7 hadi zaidi. Hiyo ni hatari)
  • Kuhisi Maumivu wakati wa kujamiiana au kutokwa na damu baada ya kujamiiana.
  • Kuhisi Maumivu chini ya kitovu na wakati mwingine kuambatana na kichefuchefu na homa kwa mbali.
  • Kuvimba kwa ngozi laini ya ndani ya uke ama inayoyozunguka ndani ya njia ya haja kubwa.

Dalili Za Ugonjwa Wa Pangusa Kwa Wanaume:

 

  • Kutokwa na majimaji yenye rangi nyeupe au kijivu kwenye uume.
  • Kuhisi Maumivu kwenye uume wakati wa kukojoa
  • Kokwa kuuma ama kuvimba
  • Ngozi kuvimba sehemu ya njia ya haja kubwa(unus)

Kwakuwa maambukizi yaweza kuwa sehemu moja, hivyo, wanaume, wanawake na watoto wanaweza kupatwa na hali ya uvimbe katika njia ya haja kubwa(mkundu), mrija wa mkojo au kope za macho. Dalili za maambukizi sehemu za kinywa au koo huwa kwa nadra sana ingawa mtu anaweza kusumbuka na vidonda vya koo. Macho yaliyoathiriwa na ugonjwa wa Klamidia yanaweza kuwa na muwasho, kuvimba, kuwa na hisia za Maumivu, ama kutokwa na tongotongo. Maambukizi katika njia ya haja kubwa husababisha kutokwa na damu, uchafu wa Klamidia pamoja na Maumivu.

Kanuni Zinazotakiwa Kutumika Ili Uweze Kufanikiwa Kuondoa Ugonjwa Huu:

 

Yafaa sana mgonjwa ahudhurie hospitali ili kufanya uchunguzi hasa anapokuwa mjamzito ama akiwa na matatizo ya aleji. Haijalishi mgonjwa anatumia tiba gani ili kuondoa ugonjwa huu lakini masharti yafuatayo sharti yazingatiwe:

  • Usifanye tendo la ndoa wakati ufanyapo matibabu mpaka pale majibu yatakapopatikana baada ya vipimo kuwa ugonjwa umetoweka.
  • Yafaa kupata vipimo kila baada ya mwezi 1-2 baada ya matibabu ili kuhakikisha kuwa maambukizi yametoweka kabia.
    Wengi wanashindwa kupona haraka kwasababu wanashindwa kuzingatia masharti hayo hapo juu. Unakuta wanaendelea kujamiiana na wapenzi wao wenye matatizo hay ohayo pindi wanapofanya matibabu. Kumbuka, yafaa wote wawili mtumie tiba hata kama mmoja wenu tayari keshaonekana na maambukizi hayo.

 

Je, Nini Madhara Ya Klamidia(Pangusa)?

 

Kutokana na muonekano wake kuwa ni maambukizi ya kawaida, lakini mara nyingi ugonjwa huu huachwa bila kuchunguzwa ama kufanyiwa vipimo kwa uhakika, na kushindwa kutibiwa na matokeo yake husababisha kuenea kwenye mji wa kizazi(uterus), mirija ya uzazi na kusababisha madhara hata matatizo ya afya ya muda mrefu yasiyoisha.
Kwa upande wa wanawake ugonjwa wa Klamidia usipotibiwa unaweza kusababisha PID(Pelvic inflammatory Disease), maambukizi ambayo huharibu viungo vya uzazi hasa mji wa kizazi pamoja na mirija ya uzazi.

NUKUU: Hatari ama madhara ya PID ni:

 

  • Kubeba mimba nje ya kizazi(ectopic pregnancy)
  • Kuziba kwa mirija ya mayai(mirija inayobeba mbegu kutoka kwenye ovary na kupeleka kwenye mji wa uzazi), ambayo inaweza kusababisha mwanamke awe na usumbufu wa kubeba ujauzito ama kuwa mgumba daima.
  • Maumivu ya nyonga kwa muda mrefu.
  • Kuporosha mimba ama kuza mtoto kabla ya miezi tisa kutimia.

 

Sababu Zingine Zinazojitekeza Ikiwa Kama Ugonjwa Wa Klamidia haukutibiwa Ni:

 

  • Uvimbe katika kibofu cha mkojo(Cystitis)
  • Uvimbe katika mlango wa kizazi na kutokwa na uchafu wenye rangi ya njano pamoja na maumivu wakati wa tendo la ndoa.

 

Kwa Upande Wa Wanaume Klamidia Isipotibiwa Inaweza Kusababisha Yafuatayo:

 

  • Maumivu makali ndani ya uume ama kokwa wakati wa kukojo(Epididymitis), hali ambayo inaweza kusababisha mwanaume kuishiwa nguvu za kiume. Hali hiyo yaweza kusababisha Maumivu kwe nye jointi za viunganishi vya mifupa hasa kwenye magoti, hali ambayo inaweza kuleta usumbufu mkubwa.
  • Kuvimba kwa mirija ya mkojo(Urethritis) na kutokwa uchafu wenye rangi ya njano ambao ambao huonekana kwenye uume. Tatizo la kuvimba kwa njia ya mkojo lisipotibiwa husababisha mirija kuwa myembamba na kuasababisha Maumivu wakati wa kukojoa na huweza kusababisha matatizo ya figo.
  • Mara nyingi kunakuwepo hali ya Maumivu katika jointi za mifupa(arthritis), kuvimba kwa mirija ya mkojo pamoja na macho.

Jinsi Ya Kuepukana na Ugonjwa Wa Klamidia

 

Ilikuepukana na hatari ya kupatwa na maambukizi ya ugonjwa huu yapaswa ufuate njia zifuatazo:

  • Jiepushe na tabia ya mambo ya zinaa au kuwa na mpenzi mmoja tu unayemwamini.
  • Tumia kinga kila ufanyapo mapenzi kuanzia mwanzo mpaka mwisho kwani ugonjwa huu huweza kuingia hata kama uume ama ulimi haujaingia ndani moja kwa moja kwenye uke.
  • Hakikisha kabisa unajua kuwa mwenzi wako hana maambukizi ya ugonjwa huu.
  • Hakikisha unapata vipimo mara kwa mara pamoja na mwenzi wako.

 

Je, Nini Cha Kufanya Ili Kuzuia Kuenea Kwa Maambukizi Ya Ugonjwa Wa Klamidia?

 

Ni lazima kabisa kumjulisha mwenzi wako ikiwa kama umepima na ukaonekana kuwa una maambukizi ya Klamidia. Mpenzi wako unapomjulisha mapema ndivyo matatibabu yatafanyika kwa urahisi. Hakikisha pia mwenzi wako naye anapata vipimo na kufanya matibabu na kuepukana na kujamiiana mpaka pale mtakapomaliza matibabu wote.

 

Ugonjwa Wa Klamidia Na Ujauzito

Ipo hatari ya maambukizi ya ugonjwa huu kutoka kwa mama mjamzito na kuja kwa mtoto wakati wa kujifungua ambayo humfanya mama awajibike kuutibu ugonjwa. Matibabu huwa salama sana ikiwa mama atawahi mapema kutumia tiba.

Unahitaja huduma James Herbal Clinic, tafadhari tupigie: 0752389252 au 0712181626