JE, WAJUA VYANZO NA DALILI ZA KUVIMBA KWA TEZI DUME? JE, NINI MADHARA YAKE?

Je, Tezi Dume Ni nini? 

Tezi dume ni sehemu mojawapo ya mfumo wa uzazi wa kiume. Inaundwa na sehemu mbili, lobes, ambazo zimeunganishwa na kufunikwa kwa nje kwa utando wa tishu. Tezi hii ipo mbele kidogo ya puru (rectum) na chini kidogo ya kibofu cha mkojo. Tezi dume inauzunguka mrija unaounganisha kibofu cha mkojo na uume (urethra).

Prostate cancer symptoms: What are the signs, how to check and when to get  the test | Express.co.uk

NUKUU: Mojawapo ya kazi za tezi dume ni kutoa majimaji yanayochanganyika na mbegu za kiume (sperms) wakati wa kilele cha tendo la ngono. Mchanganyiko huu wa mbegu pamoja na majimaji hayo hufanya shahawa (semen). Aidha majimaji hayo husaidia kuzipa mbegu za kiume nguvu ya kusafiri kwenye uke mpaka kufikia kwenye mirija ya mayai tayari kwa utungisho na yai la kike. Vilevile husaidia kupunguza hali ya kitindikali iliyopo katika uke, ambayo kama isiporekebishwa, huweza kuua mbegu nyingi za kiume na kufanya utungisho kuwa wa taabu.

Je, Tezi Dume Inavimbaje?

Kwa kadiri mwanaume anavyozeeka, ni jambo la kawaida pia kwa tezi dume kuongezeka ukubwa na kuvimba. Ukuaji wa tezi dume hupitia hatua kuu mbili. Hatua ya kwanza hutokea kipindi cha balehe wakati tezi dume linapoongezeka ukubwa na kuwa mara mbili ya lilivyokuwa hapo awali. Baada ya hapo ukuaji husimama kwa muda mpaka kijana anapofikisha miaka 25 hadi 30 ndipo hatua ya pili ya ukuaji huanza tena.

Picha ile upande wa kulia ndio inaonyesha jinsi uvimbe wa tezi dume unavyokuwa, na jinsi mkojo unavyoshindwa kutoka ama kuhisi maumivu makali.

NUKUU: Ukuaji huendelea kwa viwango na kasi tofauti kati ya mtu na mtu na hatimaye kusababisha kuvimba katika umri wa utu uzima, yaani uzeeni.

Wakati tezi dume linapokua na kutanuka, utando wa tishu unaolizunguka hutanuka pia. Hata hivyo ingawa tezi dume huendelea kukua, hufikia wakati utando wake huacha kutanuka na kufanya tezi dume kubana mrija wa kutolea mkojo kutoka kwenye kibofu. Hali hii husababisha kibofu cha mkojo kuwa na ngozi ngumu. Hali hii hufanya kibofu cha mkojo kuhisi kutaka kutoa mkojo nje hata kama kiasi cha mkojo ndani yake ni kidogo sana. Hufikia wakati, kibofu huwa dhaifu na kupoteza uwezo wake wa kuhisi kutoa mkojo na hivyo kumfanya mtu anapokojoa kushindwa kutoa mkojo wote na badala yake hubakiza kiasi fulani cha mkojo ndani ya kibofu.

Je, Nini Husababisha Tezi Dume Kuvimba?

Chanzo halisi cha kuvimba kwa tezi dume hakijajulikana kwa uhakika. Kwa muda mrefu imekuwa ikichukuliwa kuwa kuvimba kwa tezi dume hutokea kwa wanaume wenye umri mkubwa tu. Aidha imewahi kuonekana huko nyuma kuwa kuvimba kwa tezi dume hakutokei tu wanaume ambao wamewahi kufanyiwa oparesheni ya kuondoa korodani au wale ambao walizaliwa bila korodani. Hali imepelekea baadhi ya watafiti kuamini kuwa kuvimba kwa tezi dume kuna uhusiano mkubwa na umri wa mtu pamoja na uwepo wa korodani.

Je, Dalili Za Ugonjwa Huu Zinakuwaje?

Dalili za kuvimba kwa tezi dume hutokea kwa sababu ya kubanwa kwa njia ya kutoa mkojo nje ya mwili (urethra) au kibofu kushindwa kuthibiti mkojo. Aidha dalili hizi hutofautiana kati ya mtu na mtu, ingawa karibu wagonjwa wote, nazo huwa kama ifuatavyo:

  • Kukojoa mkojo unaokatika katika
  • Kukojoa mkojo wenye mtiririko dhaifu
  • Kusita kabla ya kuanza kukojoa
  • Hali ya kujihisi kubanwa na mkojo kila mara
  • Kushindwa kuthibiti mkojo kiasi cha mkojo kutirika wenyewe
  • Hali ya kuhisi mkojo haujaisha kwenye kibofu
  • Kukojoa mara kwa mara hasa nyakati za usiku
  • Kushindwa kukojoa kabisa (urine retention)

Je, Nini Madhara Yake?

Kuvimba kwa tezi dume ni kama ilivyo saratani ya tezi dume, inaweza kumletea mgonjwa madhara kadhaa. Madhara hayo ni pamoja na;

  • Mkojo kushindwa kutoka (retention of urine)
  • Mgandamizo kwenye kibofu cha mkojo
  • Vijiwe kwenye kibofu cha mkojo
  • Uambukizi katika njia ya mkojo (UTI)
  • Madhara katika figo au kibofu
  • Shinikizo la damu
  • Kushindwa kutoa shahawa kwenye uume (retrograde ejaculation)
  • Maambukizi mbalimbali
  • Damu kuganda
  • Uhanithi

Je, Tiba Yake Inakuwaje?

James Herbal Clinic tuna dawa nzuri za asili zenye uwezo mkubwa wa kuondoa matatizo ya uvimbe kwenye tezi dume na matatizo mengine mbalimbali.

 

Kwahiyo napenda niishie hapa katika makala hii, nikaribishe kipindi cha maswali, karibuni sana!

Pia unaweza kutuma namba yako ya WHATSAP ili uweze kuunganishwa katika darasa letu uweze kupata masomo mbalimbali juu ya matatizo ya fya.

Je, unahitaji huduma, basi wasiliana nasi kwa namba hizi: 0752389252 au 0712181626,

Arusha-Mbauda,

Karibuni sana!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *