JE, WAZIJUA SABABU ZA MWANAMKE KUKOSA HEDHI(AMENORRHEA)?

 

Je, Amenorrhea Ni Nini?

Kwa kawaida hii ni hali ya mwanamke ambaye amepevuka na kukomaa maumbile yake ya Uzaz kushindwa kupata hedhi au kupitiliza siku za hedhi.

Kwa ufupi tatizo hili limekua likiwakumba na kuwaletea usumbufu wa kisaikolojia wanawake wengi wakidhani kwamba wamepata ujauzito nk, hata hivyo tatizo hili la kukosa hedhi linaweza kutokea awali au baadae kabisa maishani.

 

Kuna aina mbili za tatizo hili (amenorrhea)

  1. Primary Amenorrhea: Hii ni hali ya kukosa hedhi inayomtokea mwanamke au msichana aliye katika umri wa kuvunja ungo ambapo Hali hii huweza kuendana na kutopata mabadiliko ya kimaumbile yanayoambatana na kuvunja ungo kama vile kuota nywele sehemu za siri, kuota matiti, nk ila bado hapati siku zake.

 

  1. Secondary Amenorrhea: Hii ni hali ya kukosa hedhi inayomtokea mwanamke ambaye si mjamzito wala hanyonyeshi na ambaye hajakoma hedhi na wala hatumii dawa za Uzazi wa mpango ambapo awali alikua akipata hedhi kama kawaida Lakini akasimama kwa muda huenda ni miezi au mwaka mzima hapati hedhi mpaka sasa.

 

Namna Ambavyo Mwanamke Hupata Hedhi.

Kwa Kawaida ili mwanamke apate hedhi katika mzunguko ulio sawa ni lazima tezi ya hypothalamus na pituitar pamoja na kiwanda cha mayai(ovaries) viwe vinafanya kazi kwa ushirkiano yaani sawasawa.

Vyanzo Vya Tatizo Hili

Vyanzo vya tatizo hili vyaweza kuwekwa katika Makundi makuu matatu ambayo ni vile vinavyohusisha matatizo katika

  • Mfumo wa homoni,
  • Tezi ya pituitar,
  • Mfumo wa uzazi

 

Mambo yanayohusisha mabadiliko katika mwili wa mwanamke na  visababishi hivyo ni kama ifuatavyo:

  • Matatizo katika hypothalamus ambapo matatizo haya husababisha uvimbe katika ubongo karibu na tezi ya pituitar,
  • Ukosefu au upungufu wa homoni zinazochochea kukua na kufanya kazi kwa via vya uzazi.
  • Uzito mdogo kuliko Kawaida
  • Tezi ya pituitar kushindwa kufanya kazi vizuri baada ya seli zake kufa hii ni iwapo mama alipoteza damu nyingi wakati wa kujifungua.
  • Kuwepo kwa kiwango kikubwa cha homoni ya prolactin katika damu kitaala tunaita Prolactinemia. Proclatin ni homoni inayochochea uzalishaji wa maziwa wakati wa kunyonyesha hivyo  hali ya kuwa na  proclatin nyingi katika damu husababisha kukosa hedhi
  • Kuwa na msongo wa mawazo ni hatari
  • Kuziba kwa utando unaozunguka uke yaani kitaalam tunaita Hymen,  na hivyo kukosekana tundu la kupitishia damu.
  • Mazoezi makali ya mwili na ulaji mdogo wa Chakula, tabia hii hushusha homoni ambayo inahusika na kuweka siku zako katika hali nzuri kwani hufanya leptin kuwa katika kiwango cha chini sana hivyo ni hatari
  • Ugonjwa wa kurithi wa Galactosemia unaoambatana na kuwa na kiwango kidogo cha sukari aina ya Galactose katika damu
  • Baadhi ya magonjwa ya viungo vya uzazi yamekua yakiambatana na kusimama kwa hedhi mfano wa magonjwa hayo ni Polycstic Ovarian Syndrome.

 

KUKOMA HEDHI(MENO PAUSE)

                
Hii ni hali ambayo hutokea kipindi cha miaka 42-55, homoni zinazohusika na kupata hedhi huwa kwenye kiwango cha chini sana kiasi kwamba huwa haziwezi kufanya kazi sawasawa.

 

Dalili Za Tatizo Hili

 

 

Dalili za tatizo hili huwa kama ifuatavyo:

  • Mwanamke kuwa na vinyweleo vingi na kuota ndevu, hii  inamaanisha na kuashiria kuwepo kwa kiwango kikubwa cha homoni za kiume za Androgen.
  • Kuongezeka uzito kupita kiasi
  • Matiti kutoa maziwa wakati mwanamke si mjamzito wala hanyonyeshi
  • Mwanamke kuwa na mhemko kuliko Kawaida
  • Uke kuwa mkavu
  • Kutokwa jasho sana wakati  wa usiku
  • Mabadiliko katika kupata usingizi vinaweza kuashiria kuwepo kwa tatizo katika ovaries
  • Kutokupata hedhi katika mpangilio

 

JE, KUNA MADHARA GANI YANAYOWEZA KUTOKEA IWAPO TATIZO HILI HALITAPATIWA MATIBABU?

 

  1. Mwanamke kuchelewa kuingia kukoma hedhi(menopause) hali hii ni mbaya kwani husababisha ugonjwa wa Saratani ya Matiti kwa kiasi kikubwa.

 

  1. Mwanamke kupata maumivu wakati wa tendo la ndoa kwasababu ya kupungua kwa hamu ya kufanya mapenzi na uke kuwa mkavu husababisha matatzo ya kutopata usingizi, na hivyo matiti husinyaa na kupata hedhi bila mpangilio.

 

MATIBABU

Ndugu msomaji, James Herbal Clinic tunazo tiba asili kwa ajili ya kuondoa matatizo haya ya uzazi. Unahitaji huduma, tafadhari tupigie namba hizi: 0752389252 au 0712181626