JIFUNZE UJUE FAIDA YA CHAKULA CHA NYAMA

Ili kiumbe hai chochote kiweze kuendelea kuishi kinahitaji pumzi na lishe au chakula. Ndivyo ilivyo kwa mwanadamu. Mungu alipokwisha kumuumba mtu, hakumwacha bila chakula. Alimpatia chakula katika bustani ya Edeni. Hata hivyo hakumruhusu kula chochote, bali alimuelekeza nini ale na nini asile. Katika jalada hili mada kuu itakayoongelewa ni juu ya ulaji wa nyama. Kabla hatujaanza kuangalia ulaji wa nyama, tujiulize maswali haya: nini maana ya chakula?

Chakula cha asili/awali katika uumbaji kabla ya dhambi kilikuwa nini? Chakula baada ya dhambi kilikuwaje? Chakula baada ya dunia kuangamizwa kwa gharika kilikuwaje? Ulaji wa nyama ulianzaje na uliruhusiwaje? Nini maana ya Wanyama safi na najisi (wasio safi)? Mwili wa mwanadamu umetengenezwa kwa madini gani na unapaswa kula nini?

Maana Ya Chakula

Neno Chakula linaweza kutafsiriwa kama:

  1. kitu chochote chenye uwezekano wa kugeuzwa na mnyama kuweza kutoa nguvu na kujenga tishu.
  2. Kitu chochote kigumu ambacho hutumika kama chanzo cha virutubisho.
  3. Kitu chochote kinachotoa kichocheo cha fikra za kiakili(huchochea fikra za kiakili) Kwa kuzingatia tafsiri tatu hapo juu, tunaweza kuhitimisha kwa kusema kuwa ili kiitwe chakula ni kitu chochote kinachofaa kuliwa ambacho kinaweza kuupa mwili nguvu na kuujenga, kuupatia virutubisho na kuwezesha kujenga au kukuza akili au uwezo wa kufikiri. Hivyo basi bila kujali ni chakula gani, kama hakitakuwa na hivyo vigezo, basi hicho sio chakula. Unaweza kushiba tu lakini ukawa hujala kitu chochote, matokeo yake mwili utaanzakudhoofika na hatimaye kupatwa magonjwa kama sio kupelekea kifo kabisa iwapo hatua Madhubuti hazitachukuliwa.

Uumbaji Wa Mwanadamu

Mungu alimuumba mwanadamu kwa kutumia mavumbi ya ardhi +pumzi akawa nafsi hai.(Mwanzo 2:7). Kama mavumbi ya ardhi ndiyo yalitumika kummuumba mwanadamu, je, katika ardhi kuna nini? Kuna madini mbalimbali kama vile calcium,phosphorus, potassium,iron n.k; kwa lugha rahisi tunaweza kusema hayo ndiyo madini aliyoumbiwa nayo mwanadamu, na ndiyo maana hata chakula chake lazima akipate kinacholandana na materials aliyoumbiwa kwayo.

CHAKULA KABLA YA DHAMBI/CHA AWALI

Katika Mwanzo 1:29-“Mungu akasema, Tazama, nimewapa kila mche utoao mbegu, ulio juu ya uso wa nchi yote pia, na kila mti, ambao matunda yake yana mbegu; vitakuwa ndivyo chakula chenu” hiki ndicho chakula cha awali kabisa, ambacho mwanadamu alipewa na Mungu, mara baada ya uumbaji. Ilikuwa ni matunda na chakula cha mimea itoayo mbegu, kama karanga, n.k; isitoshe Adamu hakuruhusiwa kula matunda yote, kuna mti wa ujuzi wa mema na mabaya hakupaswa kula kabisa, lasivyo ingeleta dhambi na mauti na ndicho kilichotokea. Nyama haikuwa katika orodha ya vyakula.

Hii ni kumaanisha kwamba,mwili wa mwanadamu haukuhitaji matumizi au ulaji wa nyama kabisa kabla dhambi haijaingia. Swali la kujiuuliza; miili tuliyonayo sasa imebadilika kiasi cha kuhitaji nyama ili iweze kuwa na afya bora, kuliko ile ya wazazi wetu wa kwanza? Ni jambo zito na la kuchukua tahadhari, ikiwa dhambi iliingia kupitia chakula, Yesu naye akiwa jangwani alijaribiwa kwa chakula, kizazi cha Nuhu Biblia inasema moja ya dhambi ilikuwa ni juu ya ulaji na unywaji, na hata kizazi chetu hiki Yesu alitabiri akasema itakuwa kama wakati wa Nuhu, hatari iliyoje!!(Mwanzo 6; Mathayo 24:37-38).

CHAKULA BAADA YA DHAMBI

Mara baada ya dhambi kuingia kupitia ulaji wa chakula, ardhi ililaaniwa, pia hata utaratibu wa chakula uliongezewa tofauti na awali(mboga za kondeni ikawa pia ni sehemu ya chakula cha mwanadamu tofauti na awali, pia chakula kingepatikana kwa jasho tangu wakati huo mpaka mtu atakapoyarudia mavumbi- mwanzo 3:17-18) Wanadamu walipozidi kuongezeka na maasi nayo yaliongezeka, utaratibu wote ambao Mungu aliuweka ukavunjwa, watu wakafanya yale yanayowapendeza macho yao. Utaratibu wa Ndoa, chakula, Ibada na kila kitu kikafanywa kinyume. Watu wakaanza kula vyakula ambavyo Mungu hakuruhusu, na kama tulivyoona hapo awali kuwa chakula kina athari kimwili, kiroho na kiakili, hivyo kutokana na ulaji mbaya wanadamu wakaharibikiwa akili, wakatenda maovu kiasi cha Mungu kuona hakuna haja ya kumwacha tena mwanadamu aendelee kuishi.(mwanzo 6).

Biblia inasema, siku zote mawazo ya mwanadamu yakawa ni mabaya. Huu ni uthibitisho tosha kabisa ya kuwa uwezo wa kifikra ulikuwa umeshaharibiwa kutokana na ulaji na unywaji mchafu waliokuwa wameuendekeza wakafika hatua ya kila wazo likawa ni ovu tu. Neno linasema “Basi, chochote mfanyacho iwe ni kula au kunywa, fanyeni kwa utukufu wa Mungu. (1 Kor. 10:31 AJKK).

CHAKULA BAADA YA GHARIKA

Kizazi chote cha wakati wa Nuhu kiliangamizwa kwa gharika. Kila kiumbe hai na mmea, viliangamizwa kwa maji ya gharika isipokuwa Wanyama wale ambao Mungu alimwelekeza Nuhu waingie katika Safina. Mungu alitoa maelekezo ya kuingiza katika Safina Wanyama safi na wasio safi(Mwanzo 7). Hapa ilikuwa kabla hata ya Ibrahimu wala wana wa Israeli ambao baadae alikuja kuwapa sheria na maagizo ya kufuata juu ya afya zao hususani katika suala la ulaji. Wapo watu hudai kuwa Wanyama safi na najisi walikuwa kwa ajili ya wana wa Israeli, lakini hapa inadhihirika wazi, Wanyama najisi walitambulika toka kizazi cha Nuhu, na Nuhu mwenyewe alikuwa anajua na vizazi vyake.

Baada ya dunia kuwa imeharibiwa kwa kila kitu juu ya uso wa nchi, basi Mungu akaruhusu sasa ulaji wa nyama. Lakini ni Wanyama walio safi, ambao nao walipaswa kuliwa kwa kufuata kanuni za afya, yaani ilikuwa marufuku kula nyama Pamoja na damu, wala kula Pamoja na mafuta yake.(kumbukumbu 14:3-21; Law 11:2-47; Mwanzo 7:2;9:3,4) Baada ya gharika Mungu akaruhusu ulaji wa nyama. Kila kiendacho kilicho hai kitakuwa chakula chenu, kama nilivyowapa mboga za majani, kadhalika nawapeni hivi vyote” Fungu hili halina maana ya kula kila kitu kilicho juu ya nchi kama wengine ambavyo hudhani. Kwani katika sura ya 7, Nuhu alielekezwa kuingiza Wanyama safi na wasio safi, hivyo Wanyama safi ndio aliopaswa kuwatumia. Haikuwa na maana kwamba achinje nyani ale, au nyoka, panya nk; isipokuwa ni Wanyama safi ambao Mungu alikuwa ameshamjulisha.

NYAMA KIPINDI CHA WAISRAELI

Hapo awali Mungu alikuwa anatoa maelekezo kupitia manabii au Malaika, hivyo hakuwa amewaandikia, lakini baadae alipowakomboa waisraeli kutoka misri, ndipo alipowapa sheria mbalimbali na kuamuru wazifuate. Kulikuwa na sheria za Amri kumi(sheria ya maadili) ambayo ni agano la milele, sheria za maagizo, Pamoja na sheria za Afya. Hakuna amri iliyotupiliwa mbali isipokuwa kutimilizwa. Sheria ya amri kumi hapo zamani zilikuwa zimeandikwa katika mbao mbili za mawe, lakini zamani hizi zimeandikwa katika mioyo; sheria za maagizo-zilitolewa ili kubeba laana ya torati, kwa maana ya kwamba mvunjani wa torati alikuwa amehesabiwa amelaaniwa au alistahili adhabu ya kifo, hivyo sheria za maagizo zilitumika kumlinda mkosaji, lakini baada ya kifo cha Yesu aliondoa laana ya Torati, na hizo sheria za maagizo ambazo ni hati ya mashitaka ziligongomelewa msalabani Pamoja na sikukuu zake na vyakula na vinywaji, ambavyo vilimwakilisha Yesu. Sheria za afya zinabaki kama zilivyo, kwa maana ya kwamba, Yesu hakufa msalabani ili kutakasa vyakula najisi, tunapokula na kunywa yatupasa kuyafanya yote kwa utukufu wa Mungu(1kor 10:31).

ULAJI WA NYAMA SAFI ULIPASWA NA UNAPASWA UZINGATIE HAYA BILA MAFUTA (Law 3:17): mafuta ya mnyama husababisha magonjwa ya moyo nk.kumbuka: lakini tunapaswa kula protini ya ardhini kama vile parachichi, karanga, zeituni n.k. (Mwanzo 45:18)

PASIPO DAMU (Law 3:17): moja ya visababishi vikuu vya saratani ni ulaji wa nyama nyekundu(damu)

ASIWE KILEMA (Law 3:1)

BILA KUNYONGA(mdo 15:20)

Lazima iliwe kwa siku tatu-isizidi siku tatu (Law 19:5-7)

Isijifie yenyewe(nyamafu) (kumbukumbu 14:21)

Note: Kumbuka!!! Kama tukitaka kuwa na afya, lazima tufuate sheria hizi za ulaji wa chakula cha nyama. Kama hatutaki kufuata sheria hizi, huwezi kuwa na afya. Na vilevile kumbuka!!! Ni miaka 70-80 tu imeahidiwa kwa walaji wa nyama. Sayansi imethibitisha kwamba walaji wa mimea wanaweza kuishi zaidi ya 100%. Hivyo basi Pamoja na kwamba nyama safi imeruhusiwa katika Biblia, haina maana kwamba inapaswa kuliwa tu bila utaratibu. Mnyama yoyote ambaye ni safi, kama akiugua au kupatwa na ugonjwa huwezi ukamwita tena huyo ni safi, hapana, huyo anakuwa najisi kama Wanyama wengine. Watu wanapaswa kuelewa nyama najisi haina maana kwamba ukila utakufa, au ni chungu, isipokuwa nyama najisi inadhuru afya haifai kwa chakula kwa mwanadamu. Pamoja na kwamba mnyama atakuwa ni yule safi, kama akiwa ana ugonjwa huyo sio safi tena, ni sawa na kundi la Wanyama wengine wasio safi. Kwa hiyo watu wanapaswa kuelewa Wanyama wasio safi sio tu wale waliotajwa bali hata wale ambao wana kasoro za kiafya nao pia sio safi hawafai kutumiwa kwa chakula cha mwanadamu.

Lengo la mafundisho ya matengenezo ya afya kwa mtu wa Mungu ni kuwafanya waweze kutumia vizuri uwezo wao wa akili, roho, na mwili ili kuonyesha utukufu au tabia ya Mungu kwa kila wanachokifanya. Ili tuweze kumtukuza Mungu kwa kila tunachofanya hatuna budi kujifunza na kuishi kwa kanuni bora na matengenezo ya afyaambazo zimejumuishwa katika gurudumu la afya lenye njukuti nane ambazo ni mfano wa dawa nane za asili, nazo ni:-

  • Hewa safi [2] Mwanga wa jua [3] Kiasi, [4] Pumziko [5] Mazoezi ya mwili [6] Chakula bora [7] Kutumia maji [8]Kutegemea uwezo wa Mungu – hizi ndizo dawa za kweli (MH, uk. 127).

Kutojua, kukataa, kutojali kutumia mojawapo ya dawa hizi za asili kutaathiri afya ya mwili, akili na roho. Hivyo hatatuonyesha utukufu wa Mungu katika mambo tunayofanya. Katika somo hili nitajadili juu ya ujukuti mmoja tu ambao, kwa maoni yangu wengi hatuuelewi vizuri, wachache wameulegeza, na wengine ambao wamepata nafasi ya kuujua hawautumii vizuri kwa utukufu wa Mungu. Ujukuti huo ni chakula bora, yaani; nile chakulagani kinachofaa ili nimtukuze Mungu?

CHAKULA BORA

Chakula bora au kifaacho ni kipi?

  1. Ni kile ambacho kina virutubisho (nutrients) ambavyo vinawezesha mwili ufanyiwe mambo matatu ya usalama.
  • Mwili ujengwe na ukue
  • Mwili utiwe nguvu na joto
  • Mwili ulindwe
  1. Virutubisho muhimu ambavyo vinaweza kupatikana katika chakula ni kama vifuatavyo:-
  • Protini – Kukuza na kujenga mwili
  • Hamirojo au kabohaidreti – kuupa mwili nguvu na joto
  • Mafuta – kuupa miwli nguvu na joto
  • Vitamini – kuukinga mwili usipatwe na magonjwa
  • Madini – Kuukinga mwili usipatwe na magonjwa
  • Nyuzinyuzi (roughage)-Kusafisha na kurainisha mkondo wa umeng’enyo wa chakula
  • Maji safi na salama Mungu mwenyewe anasema, “Ni sikilizeni kwa bidii, mle kilicho chema, na kujifurahisha nafsi zenu kwa unono”. 55:2.
  • Ingawa fungu hili linaweza kukaziwa zaidi kwa kutafuta mema yanayolisha maisha ya kiroho zaidi kuliko ya kimwili; linaweza kutumiwa pia kuonya watu wasiolisha miili yao kwa chakula bora. Kwa hiyo inatupasa tumsikilize Mungu tunapohitaji kujua ni chakula gani bora kinachoweza kurutubisha, kufurahisha nafsi zetu kwa “unono” yaani kustawisha miili yetu.
  • Ili kujua vyakula vilivyo bora lazima tujifunze mpango wa kwanza wa Mungu wa chakula cha mwanadamu. Mungu alivyomuumba mwanadamu na anayefahamu mahitaji yake ndiye alimchagulia Adamu chakula chake, akasema, “Tazama, nimewapa kila mche utoao mbegu, ulio juu ya uso wa nchi yote pia, na kila mti, ambao matunda yake yana mbegu; vitakuwa ndivyo vyakula vyenu (Mwa. 1:29) Adamu alipondoka Edeni ili aishi kwa kuilima ardhi iliyokuwa imelaaniwa kwa sababu ya dhambi, aliruhusiwa kula pia “mboga za kondeni” (Mwa. 3:18). Kwa hiyo kwa kumsikiliza Mungu alivyosema hapo mwanzo, tunaweza kusema kula chakula bora alichokusudia tule ni nafaka, matunda kokwa (karanga, jungu na sina zote za maharagwe) na mboga.
  1. Je, tukichambua mpango wa kwanza wa chakula tunaweza kupata virutubisho au viasili vyenye kujenga, kukuza, kutia mwili nguvu na joto, na kuukinga na maradhi?
  2. Kwa kuchambua fungu la Mwa. 1:29 na 3:18; tunaweza kutoa mifano ya vyakula vya mimea na miti ambavyo vinajenga na kuukuza mwili, vinaupa mwili nguvu na joto na vinalinda mwli kama ifuatavyo:-
  • Kujenga na kukuza mwili – vyenye virutubisho vya protini kama; njugu, maharagwe, mbaazi, dengu, choroko, kunde, maharagwe ya soya, na vingine vya aina hiyo.
  • Kutia nguvu na joto mwilini – vyenye virutubisho vya hamirojo kama: nafaka zote, mahindi, mchele, mtama, ngano, na uwele. Vile vile vinatokana na mimea ya mizizi kama mihogo na viazi vya aina zote. Sukari inapatikana katika miwa, na baadhi ya matunda. Kirutubisho cha mafuta tunaweza kukipata kutokana na karanga, korosho, ufuta,. Kwema, mawese, pamba, alizeti n.k.
  • Kulinda mwili – vyenye virutubisho vya vitamin na madini; vitamin – inapatikana kutokana na matunda na mboga za kijani kibichi. Madini hutokana na mboga na baadhi ya nafaka.
  • Kwa nini vyakula vinavyotokana na wanyama na samaki havikutajwa katika mpango wa kwanza wa chakula bora cha mwanadamu?

1.Kwa sababu “ilikuwa kinyume cha mpango wake kuua kiumbe chochote. Nuru kwa Kanisa uk. 251, (chapa mpya). Hivyo haikuwa kwa ajili ya utukufu wa Mungu mtu kuua wanyama ili awatumie kwa chakula chake. 2.Mungu Muumbaji wa mwanadamu na viumbe vyote alijua kwamba chakula cha nyama si chakula bora chenye kujenga na kukuza mwili, akili na roho kwa sababu Roho ya Unabii imefunua madhara yafuatayo:-

[i] Madhara kwa akili

  • Hupunguza uwezo wa akili CD. Uk. 389, Nuru kwa Kanisa uk. 253. [b] Hutia giza ubongoni ili usielewe mambo dhahiri 2T, 62, CD. 389
  • Huzuia uwezo wa akili kukua CD, 402, 7T 134
  • Hufifisha wepesi wa akili wa kuhisi au kutoa hisia njema CD, 395, 2T 63.
  • Hudhoofisha uwezo wa akili wa kumjua Mungu na kuelewa ukweli CD, 384.

[ii] Madhara ya kiroho na kiakili

  • Huzuia kukua kwa uwezo wa maadili – uwezo wa kutambua mema na mabaya 7T, 134.
  • Hufisha, hupunguza, hudhoofisha uwezo wa maadili CD. 269 2T 352., [c] Hufifisha wepesi wa kutoa hisia za maadili, 2T 64.
  • Huzuia kukua kiroho CD 402
  • Hutunyang’anya hisia za kupendana na kuhurumiana 9T, 159 CD 404, Nuru kwa Kanisa, uk. 259,
  • Hudhoofisha tabia na uwezo wa kiroho, CD 389,Ev. 663.

[iii] Madhara ya Kimwili

  • Hukuza na kuimarisha unyama zaidi kuliko utu, CD. 383, CD 390, 259. [b] Hukuza, huamsha, huimarisha anasa na tamaa za kimwili CD 390, CD 384, 2T 63.
  • Huzuia kukua kwa nguvu za kimwili CD 402. [d) Huzimisha, uharibu, huchafua damu na hivyo hupunguza ubora wake, CD 387, 391, 2T 368, 64.
  • Hupunguza nguvu za kimwili, CD 487, 269, 2T, 64.
  • Hukuza mara kumi uwezekano wa kupatwa na magonjwa CD 386, 2T 61

g]Hupanda mbegu za magonjwa mwilini na kupunguza nguvu za kupigana na magonjwa, CD 386-7, samaki pia huleta magonjwa CD 394.

[h] Huficha hamu ya kutaka chakula bora, CD 158.

[i] Huvuruga kazi ya tumbo na kulidhuru, CD 266, 268-9, 2T 486. [j]Hushitua neva na kuziwasha, CD 236, 397 [k]Hufupisha maisha, CD 373.

  1. Ikiwa chakula cha nyama kinadhuru mwili, akili na roho, kwa nini Biblia inasema tule wanyama na samaki safi? Ruhusa hii ilitolewa lini? 1.Mungu alimruhusu mwanadamu kula nyama kama chakula chake cha muda wakati wa dhiki, wakati baada ya gharika ambapo gharika iliangamiza chakula cha mimea. Mwa. 9:3,4.
  • “Mungu hakumruhusu mwanadamu kula nyama mpaka baada ya gharika. Kila kitu ambacho mwanadamu angeweza kujilisha kwacho kilikuwa kimekwisha haribiwa. Kwa sababu ya dhiki waliyopata, Bwana akamruhusu Nuhu kula wanyama wasafi alioingia nao Lakini nyama haikuwa chakula bora cha kumpatia afya mwanadamu”. (CD 373, Nuru kwa Kanisa 251, Tazama pia PP uk. 107).
  • “Kwa sababu uharibifu wa muda uliotokea kwa mimea katika gharika na kumalizika kwa chakula kilichoingizwa safinani, shida ya dharura ilitokea ambayo Mungu aliikabili kwa kuruhusu kula nyama”. (SDA Bible Commentary), uk. 263.
  1. Sababu ya pili ya kuruhusu nyama ilikuwa kufupisha maisha ya dhambi. “Baada ya gharika watu walikula nyama kwa wingi…… Na Mungu akawaruhusu watu wale waliokuwa wenye maisha marefu kula chakula cha nyama ili afupishe maisha yao ya dhambi”. CD 373.
  2. Wakati mwingine ambao Mungu alilazimika kumruhusu mwanadamu ale nyama ni wakati Waisraeli walipokuwa jangwani (Kut. 16:8; 11-15; Hesabu 11).
  • Mungu alipowakomboa Waisraeli kutoka Misri hakupenda kuwapa nyama. Baada yake aliwapa mana – mkate wa mbinguni. Kwa nini? [a] Kingezuia kusudi la Mungu la kuwafanya Waisraeli kuwa taifa teule, takatifu, safi lenye furaha na afya kamili ya kimwili, kiakili na kiroho, taifa ambalo lingeonyesha ulimwengu mwenendo ambao ungewavuta wengine kwa utukufu na utakatifu wa Mungu (Kut. 19; Zab. 67:2). [b]Alikusudia kuifanyia matengenezo tama yao ya chakula iliyokuwa imeharibiwa, ili waweze kupendezwa na chakula cha mimea.

Dondoo:

“…….Mungu hakuwapa watu wake nyama jangwani, kwa sababu alijua kwamba kukitumia chakula hiki kungeleta magonjwa na uasi. Ili kubadilisha tabia zao na kufanya uwezo wa akili wa kutenda mema kutumika kwa juhudi, aliwanyima nyama. Aliwapa chakula cha malaika, maana kutoka mbinguni”. CD 375.

“………Mungu angeweza kuwapa nyama kwa urahisi kama alivyowapa mana. Lakini aliwanyima kwa ajili ya faida yao. Kusudi lake llikuwa kuwapa chakula kilichofaa zaidi mahitaji yao kuliko chenye kuleta harara ambacho wengi wao walikuwa wamekizoea Misri. Tamaa yao ya chakula iliwapaswa ibadillishwe katika hali ya kiafya zaidi, ili waweze kufurahia chakula ambacho mwanadamu alipewa mwanzoni”. CD 378.

[ii] Waisraeli hawakuridhika na chakula cha kutia afya walichopewa na Mungu, wakaichukia mana. Walifanya nini?

  • Walinung’unika – Hes. 11:1

[b] Wageni Wasio Waisraeli walitamani kwanza nyama. (Hes. 11:4) Hawa walikuwa Wamisri waliofuatana na Waisraeli wakiwa wanatamani kufika Kanani, nchi ya wateule, lakini hawakuwa tayari kuishi kwa kanuni na desturi za watu wlaiokuwa wanatazamiwa kufika huko.  [c]Chachu ya wageni ilichachua kundi lote la Waisraeli, nao wakasema, “Nani atakayetupa nyama tule?(Hes. 11:4).

4. Kutoamini kwao kulizaa manung’uniko na tamaa, na dhambi hii ilizaa dhambi zifuatazo: (Taz. Mathew Henry’s Bible Commentary, uk. 152; Hes. 11:4-6).

[i]Walikitukuza chakula kizuri na tele cha Misri “kana kwamba Mungu alikuwa amekosea sana kuwatoa huko”. Walisahau taabu iliyowafanya watolewe Misri.

[ii]Walikinaiwa na chakula bora ambacho Mungu alikuwa amewapa (fungu la 6) “ Kilikuwa mkate kutoka mbinguni, chakula cha malaika ……. Lakini walikildharau kana kwamba kilifaa kuwa chakula cha nguruwe”.

[iii]Hawakuweza kuridhika na kushiba mpaka walipopata nyama ya kula. [iv]Hawakuamini uwezo na wema wa Mungu kwamba angeweza kuwapatia mahitaji yao (fungu la 4).

[v] Walitoa madai yao kwa kung’ang’aniza na ukaidi.Walitamani nyama si kwa ajili ya utukufu wa Mungu. Nyama inaweza kuwa halali kuliwa. Lakini kutamani nyama kulionekana dhambi kwao. Kwa nini? “Kilicho halali kinaweza kuwa kiovu kwetu ikiwa ndicho Mungu hakutugawia ingawa tunakitamani sana”.

III. FUNDISHO KWETU LEO

Kutokana na historia ya chakula cha Biblia, baada ya gharika na jangwani, tunapata fundisho gani kwetu sisi Waisraeli wa kiroho?

A. Chakula cha Edeni

  1. “Tena na tena nimeonyeshwa kwamba Mungu anajaribu kutuongoza hatua kwa hatua kwa mpango wake wa mwanzoni – kwamba mwanadamu ajilishe kutokana na mazao ya asili ya ardhi – mboga, matunda na nafaka vingefanywa chakula chetu. Hata wakia moja ya nyama isingeingizwa katika matumbo yetu. Ulaji wa nyama si wa asili. Hatuna budi kurudia kusudi la kwanza la Mungu katika uumbaji wa mwanadamu”. CD 380.
  2. Tuanze kuwa na uhusiano mwema kwa viumbe vyake – huruma na upendo, na kuonja maisha ya Edeni tangu sasa. “Inawezekanaje kwa wale wanaotaka kuwa safi kutakaswa, na watakatifu ili waweze kuwa na ushirika pamoja na malaika wa mbinguni, waendelee kutumia kama chakula chochote ambacho kinadhuru mwili na roho? Wanawezaje kuua viumbe vya Mungu ili watumie nyama kama chakula cha anasa? Afya na kitamu alichopewa mwanadamu mwanzoni, na wajizoezoe kutumia na wafundishe watoto wao kuhurumia wanyama ambao Mungu amewaumba na kuwaweka chini ya utawala wetu”. CD 380.
  3. Chakula cha wanaojitayarisha kuchukuliwa katika Edeni ya pili ni nini?

[a“] Nafaka, matunda, mboga na kokwa ambavyo vimetayarishwa bila mafuta ya wanyama, na katika hali ya kawaida kadiri iwezekanavyo, ndivyo vinapaswa kuwa vyakula katika meza ya wote wanaodai kuwa wanajitayarisha kuchukuliwa mbinguni”. (CD 314).

(a). Bila kuonja kifo “Miongoni mwa wale wanaongojea kuja kwa Bwana, wataachilia mbali kula nyama hatimaye; nyama itakoma kuwa sehemu ya chakula chao”. (Nuru kwa Kanisa, uk. 255, CD 380).

Kwa siku zetu leo gharika ni mfano wa sehemu ambazo chakula bora hakipatikani kabisa au hakitoshi, mwili ambao kwa sababu fulani unadhurika ukilishwa protini ya mimea, na hali ya kimaskini ya kutoweza kulima au kununua vyakula badala ya nyama. Katika hali kama hizi za shida Mungu alilazimika kuhalalisha ulaji wa nyama ingawa si chakula bora ili mtu aweze kupata riziki. Kadhalika mtu ambaye ameacha kula nyama anaweza kulazimika kula nyama anapopatwa na shida kama hizi. Katika muda huo kula kwake nyama ni halali kwa sababu anakula kwa ajili ya utukufu wa Mungu, si kwa ajili ya utukufu wake, yaani kuridhisha uchu wake wa kutaka nyama tu. Nyama ili kukidhi haja, siyo kuridhisha uchu/tamaa.

(b). “Katika hali fulani za ugonjwa au uchovu inaweza kuwa jambo bora kula nyama, lakini uangalifu mwingi uchukuliwe kupata nyama ya wanyama wenye afya bora. Ni afadhali kutokula nyama kabisa kuliko kula nyama ya wanyama wagonjwa”. CD 394.

Katika maisha ya Elen G. White [b]“Nilipokosa chakula nilichohitaji, mara nyingine nimekula nyama kidogo, lakini ninazidi kuiogopa”. CD 394.

“Mara moja niliondoa nyama katika orodha ya vyakula vyangu. Wakati mwingine baada ya hapo, niliwekwa mahali nilipolazimika kula nyama kidogo”. (CD 487, Appendix 1:10).

(c). Ingawa nyama si miongoni mwa vyakula bora sana vinavyofaa kwa afya, lakini sipaswi kuchukua msimamo kwamba kila mtu aache nyama. Wale wenye matumbo ya kusaga chakula yaliyo dhaifu wanaweza kula nyama mara kwa mara, wakati ambapo hawawezi kula mboga, matunda au uji wa nafaka iliyopikwa (bokoboko)” CD 395.

(d). “Siku moja Sara aliitwa kwa familia moja kule Dora Greek ambamo kila mtu wa familia hiyo alikuwa mgonjwa….. katika wakati huu wa ugonjwa hapakuwemo chakula cha kufaa nyumbani mwao. Na walikataa kula chochote tulichowapelekea. Walikuwa wamezoea kula nyama. Tulijisikia kwamba lazima kitu fulani kifanywe. Nilimwambia Sara, chukua kuku nyumbani mwangu, watengenezee mchuzi wa nyama na mboga. Hivyo Sara aliwatibu ugonjwa wao, na kuwalisha mchuzi wa nyama na mboga. Mara walipona”. “Hii ndio njia tuliyotumia. Hatukuwaambia, lazima msile nyama. Ingawa sisi wenyewe hatukula nyama, lakini tuliwapa tulichoona kwamba ni cha lazima kwao katika muda huo wa ugonjwa wao”. CD 466.

3. Hizi ni hali za kipekee za shida ambazo inaweza kuwa halali kwa ajili ya utukufu wa Mungu, kula nyama. Lakini wengine kwa kuridhisha tamaa zao za chakula cha nyama, wamedhani kwamba wakati wowote ni wakati wa kula nyama. Mtazamo huo una makosakama tunavyoona katika historia ya Waisraeli jangwani.

C. Chakula cha Waisraeli Jangwani

  1. Mungu alipokomboa miili ya Waisraeli kutoka utumwani Misri, hakutaka nyama iingizwe katika miili yao kwa sababu chakula hiki kingefisha lengo la kuwafanya taifa teule, takatifu na lenye afya bora. Alitaka waanze kuzoea chakula cha asili cha Edeni. Kadhalika na sisi leo. Miili yetu imekombolewa kwa bei kubwa (1 Kor. 6:20). Hivyo Mungu anapenda tutunze miili yetu ili ifae kuwa makao yake, ifae kutangaza fadhili zake, (1 Kor. 3:16; War. 12:1) (1 Pet. 2:9).
  2. Mungu aliwapa mana, badala ya nyama. Hivyo hawakuwa na sababu ya kuhitaji nyama.

(a). Mahali ambapo kunapatikana maziwa bora na matunda kwa wingi, kwa nadra upo udhuru wa kula nyama; siyo lazima kuwa kiumbe chochote cha Mungu kukidhi mahitaji yetu ya kawaida”. CD 394.

(b). “Hatuchori mstari halisi wa kufuatwa katika chakula, lakini tunasema kuwa katika nchi zenye matunda, nafaka, na mbegu za jamii ya njugu na karanga, kwa wingi, nyama si chakula bora kwa watu wa Mungu”. CD 404.

4. Wageni waliofuatana na Waisraeli walianza kutamani nyama. Hawa walikuwa Wamisri waliokuwa wanapenda kufika Kanaani, lakini hawakuwa tayari kuamini kanuni na maisha ya watu waliotazamiwa kuishi Kanaani. Kadhalika miongoni mwa Waisraeli wa kiroho leo, wapo wageni wanaosafiri pamoja na Waisraeli halisi. Ni Wakristo waliobatizwa lakini hawajajua na kuamini kabisa mafundisho mengine au yote ya Roho ya Unabii. Kwa hiyo, hata kama utawapatia vyakula vyote vyanafaka, mboga na kokwa, bado watadai nyama. Je, wewe ni mmoja wao?

5. Chachu ya hao wageni iliambukiza Waisraeli wote. Inawezekana pia kwamba Wakristo ambao wanatamani kurudia mpango wa Mungu wa kwanza wa chakula, wakageuzwa nia zao na kurudia vyungu vya Misri. Simama imara.

6. Waisraeli kwa ujumla walidharau mana kana kwamba ni chakula cha mbwa, kwamba hakikufaa kwa mahitaji yao. Hata leo wapo Wakristo wanakiita “chakula cha wafungwa na wanafunzi wa shule”. Wanaiona nyama kama chakula cha fahari kama Waisraeli walivyoona nyama na samaki za Misri. Unafikiriaje chakula cha nyama ukilinganisha na chakula asili?

7. Kula nyama kunaweza kukawa dhambi au kusiwe dhambi kwetu leo kutegemeana na sababu inayotusukuma kula. Kwa Waisraeli kula nyama jangwani kulihesabiwa dhambi kwa sababu walinung’unika na kung’ang’ania kutamani kitu ambacho hakikuwa lazima kwao wakipate. Hawakuwa katika shida yoyote ya hukosefu wa hitaji muhimu la maisha yao. Hivyo walidai nyama siyo kwa sababu ya hitaji, bali uchu. Ndivyo tulivyo wengi wetu leo. Tunadai nyama wakati isipohitajika mwilini. Kwa mfano, umekaribishwa katika mezayenye chakula cha nyama, mboga na maharage au kunde. Tamaa yako ya chakula itakuelekeza ule nini? Nyama au vingine? Kwa nini? Je, unapofika hotelini, ni chakula gani unaanza kutafuta? Wali kwa nyama au wali kwa maharagwe? Kwa nini? Unapoenda mikutano ya wafanyakazi, unawatafutia chakula gani kwanza? Kwa nini? Tukila nyama kwa ajili ya utukufu wetu ni dhambi.

8. Tamaa ya chakula iliyosababishwa na kutomwanini Mungu iliwafanya Adamu na Hawa wapoteze Edeni. Kadhalika Waisraeli wengi jangwani walipoteza Kanaani, Edeni ya pili, kwa sababu walitamani kitu ambacho Mungu hakuwagawia wakati ambao walikuwa na kitu bora zaidi.

(a). “Watu wengi ambao sasa wameongoka nusu tu juu ya suala la kula nyama wataachana na watu wa Mungu wasitembee pamoja nao tena”. CD 382.

(b). “Kama vile Wazazi wetu wa kwanza walivyopoteza Edeni kwa njia ya tama ya chakula, tumaini letu tu la kupata tena Edeni ni kwa njia ya kujikana tamaa ya chakula na uchu”. CD 59.

8. Ingawa Waisraeli waling’ang’ania wapewe nyama, Mungu aliwapa kuonyesha upendo na huruma yake. Upendo wa Mungu haulazimishi, unampa nafasi mtu achague njia anayopenda na kisha avune matokeo yake mwenyewe.

(a). “Mungu aliwapa Waisraeli kile ambacho hakikuwa kwa ajili ya manufaa yao sana kwa sababu waling’ang’ana kukitamani. Hawakuweza kuridhika na vitu ambavyo vingewaletea faida. Tamaa zao za wazi ziliridhishwa, lakini walivuna madhara yake”. (PP 382, Zab. 106:14, 15).

(b). Hii inatufundisha kwamba watu wa Mungu wafundishwe ubaya wa kula nyama na wazoeshwe kupewa vyakula vya asili. Lakini wanapong’ang’ana kutamani kiasi cha kuvuruga amani, basi wapewe. Nao watavuna matokeo yake!

IV.KUTOKA ULAJI WA NYAMA HADI ULAJI WA MBOGA (VEGETERIANNISH)

Iwapo kama umezoelea kula nyama, lakini sasa unataka kurudia mpango wa Mungu wa chakula cha mwanzoni. Ufanye nini? Au umeshaamua tayari kuacha nyama, Je, uendelee kufanya nini na mwelekeo wako kwa wale wanaokula nyama uwe upi?

A.Kwanza elimisha dhamiri na tamaa yako kuhusu chakula cha nyama kwa kusoma juu ya suala lenyewe, kuomba, kuuliza maswali.

(a). “Katika hali zote, elimisha dhamiri, tumia uwezo wa kuchagua, jipatie vyakula bora vyenye kuleta afya na badiliko litafanyika kwa urahisi, na tamaaya kutaka nyama itakwisha mara”. CD 398.

(b). “Watu wa ulimwengu wanatawaliwa na kanuni za kidunia; hawawezi kukabili zingine. Lakini Wakristo hawapaswi kuongozwa na kanuni hizi. Hawapaswi kujiimarisha wenyewe katika kutekeleza wajibu kwa njia nyigine badala ya upendo wa kutii kila takwa la Mungu lililomo katika neon lake na linaloongozwa na dhamiri iliyoelimishwa”. 2T 488.

B. Utakula nini badala ya nyama?

(a). Kula aina nyingi za vyakula vya mimea kwa kubadilisha milo yake. “Nyama inapokataliwa, weka badala yake aina nyingi za nafaka, kokwa, matunda na mboga, vyakula ambavyo vitakuwa vyenye kuulisha mwili na kuleta hamu ya kula.

(b). Uvipike vizuri ili tumbo lisivichukie. “Lazima kitu fulani kitayarishwe badala ya nyama, na vitu hivi vilivyo badala ya nyama lazima vitayarishwe vizuri, kusudi nyama isitamanike tena”. CD 398.

(c). Maziwa na mayai yanayotokana na wanyama na kuku wenye afya bora na yaliyopikwa au kuchemshwa vizuri yanaweza kutumika badala ya nyama. Hasa kwa wale ambao hawajafikia hatua ya matengenezo ya afya ya kuwa wala mboga halisi (pure vegeterians) (Taz. CD 351, 353, 357, 394).

C. Epuka tabia ya kuzidi kiasi (Extremes)

  1. Mungu alipokomboa miili ya Waisraeli kutoka utumwani Misri, hakutaka nyama iingizwe katika miili yao kwa sababu chakula hiki kingefisha lengo la kuwafanya taifa teule, takatifu na lenye afya bora. Alitaka waanze kuzoea chakula cha asili cha Edeni. Kadhalika na sisi leo. Miili yetu imekombolewa kwa bei kubwa (1 Kor. 6:20). Hivyo Mungu anapenda tutunze miili yetu ili ifae kuwa makao yake, ifae kutangaza fadhili zake, (1 Kor. 3:16; War. 12:1) (1 Pet. 2:9).
  2. Mungu aliwapa mana, badala ya nyama. Hivyo hawakuwa na sababu ya kuhitaji nyama.

(a). Mahali ambapo kunapatikana maziwa bora na matunda kwa wingi, kwa nadra upo udhuru wa kula nyama; siyo lazima kuwa kiumbe chochote cha Mungu kukidhi mahitaji yetu ya kawaida”. CD 394.

(b). “Hatuchori mstari halisi wa kufuatwa katika chakula, lakini tunasema kuwa katika nchi zenye matunda, nafaka, na mbegu za jamii ya njugu na karanga, kwa wingi, nyama si chakula bora kwa watu wa Mungu”. CD 404.

  1. Wageni waliofuatana na Waisraeli walianza kutamani nyama. Hawa walikuwa Wamisri waliokuwa wanapenda kufika Kanaani, lakini hawakuwa tayari kuamini kanuni na maisha ya watu waliotazamiwa kuishi Kanaani. Kadhalika miongoni mwa Waisraeli wa kiroho leo, wapo wageni wanaosafiri pamoja na Waisraeli halisi. Ni Wakristo waliobatizwa lakini hawajajua na kuamini kabisa mafundisho mengine au yote ya Roho ya Unabii. Kwa hiyo, hata kama utawapatia vyakula vyote vyanafaka, mboga na kokwa, bado watadai nyama. Je, wewe ni mmoja wao?
  2. Chachu ya hao wageni iliambukiza Waisraeli wote. Inawezekana pia kwamba Wakristo ambao wanatamani kurudia mpango wa Mungu wa kwanza wa chakula, wakageuzwa nia zao na kurudia vyungu vya Misri. Simama imara.
  3. Waisraeli kwa ujumla walidharau mana kana kwamba ni chakula cha mbwa, kwamba hakikufaa kwa mahitaji yao. Hata leo wapo Wakristo wanakiita “chakula cha wafungwa na wanafunzi wa shule”. Wanaiona nyama kama chakula cha fahari kama Waisraeli walivyoona nyama na samaki za Misri. Unafikiriaje chakula cha nyama ukilinganisha na chakula asili?
  4. Kula nyama kunaweza kukawa dhambi au kusiwe dhambi kwetu leo kutegemeana na sababu inayotusukuma kula. Kwa Waisraeli kula nyama jangwani kulihesabiwa dhambi kwa sababu walinung’unika na kung’ang’ania kutamani kitu ambacho hakikuwa lazima kwao wakipate. Hawakuwa katika shida yoyote ya hukosefu wa hitaji muhimu la maisha yao. Hivyo walidai nyama siyo kwa sababu ya hitaji, bali uchu. Ndivyo tulivyo wengi wetu leo. Tunadai nyama wakati isipohitajika mwilini. Kwa mfano, umekaribishwa katika meza yenye chakula cha nyama, mboga na maharage au kunde. Tamaa yako ya chakula itakuelekeza ule nini? Nyama au vingine? Kwa nini? Je, unapofika hotelini, ni chakula gani unaanza kutafuta? Wali kwa nyama au wali kwa maharagwe? Kwa nini? Unapoenda mikutano ya wafanyakazi, unawatafutia chakula gani kwanza? Kwa nini? Tukila nyama kwa ajili ya utukufu wetu ni dhambi.
  5. Tamaa ya chakula iliyosababishwa na kutomwanini Mungu iliwafanya Adamu na Hawa wapoteze Edeni. Kadhalika Waisraeli wengi jangwani walipoteza Kanaani, Edeni ya pili, kwa sababu walitamani kitu ambacho Mungu hakuwagawia wakati ambao walikuwa na kitu bora zaidi.

(a) “Watu wengi ambao sasa wameongoka nusu tu juu ya suala la kula nyama wataachana na watu wa Mungu wasitembee pamoja nao tena”. CD 382.

(b). “Kama vile Wazazi wetu wa kwanza walivyopoteza Edeni kwa njia ya tama ya chakula, tumaini letu tu la kupata tena Edeni ni kwa njia ya kujikana tamaa ya chakula na uchu”. CD 59.

  1. Ingawa Waisraeli waling’ang’ania wapewe nyama, Mungu aliwapa kuonyesha upendo na huruma yake. Upendo wa Mungu haulazimishi, unampa nafasi mtu achague njia anayopenda na kisha avune matokeo yake mwenyewe.

(a). “Mungu aliwapa Waisraeli kile ambacho hakikuwa kwa ajili ya manufaa yao sana kwa sababu waling’ang’ana kukitamani. Hawakuweza kuridhika na vitu ambavyo vingewaletea faida. Tamaa zao za wazi ziliridhishwa, lakini walivuna madhara yake”. (PP 382, Zab. 106:14, 15).

(b). Hii inatufundisha kwamba watu wa Mungu wafundishwe ubaya wa kula nyama na wazoeshwe kupewa vyakula vya asili. Lakini wanapong’ang’ana kutamani kiasi cha kuvuruga amani, basi wapewe. Nao watavuna matokeo yake!

IV.KUTOKA ULAJI WA NYAMA HADI ULAJI WA MBOGA (VEGETERIANNISH)

Iwapo kama umezoelea kula nyama, lakini sasa unataka kurudia mpango wa Mungu wa chakula cha mwanzoni. Ufanye nini? Au umeshaamua tayari kuacha nyama, Je, uendelee kufanya nini na mwelekeo wako kwa wale wanaokula nyama uwe upi?

A. Kwanza elimisha dhamiri na tamaa yako kuhusu chakula cha nyama kwa kusoma juu ya suala lenyewe, kuomba, kuuliza maswali.

(a). “Katika hali zote, elimisha dhamiri, tumia uwezo wa kuchagua, jipatie vyakula bora vyenye kuleta afya na badiliko litafanyika kwa urahisi, na tama ya kutaka nyama itakwisha mara”. CD 398.

(b). “Watu wa ulimwengu wanatawaliwa na kanuni za kidunia; hawawezi kukabili zingine. Lakini Wakristo hawapaswi kuongozwa na kanuni hizi. Hawapaswi kujiimarisha wenyewe katika kutekeleza wajibu kwa njia nyigine badala ya upendo wa kutii kila takwa la Mungu lililomo katika neon lake na linaloongozwa na dhamiri iliyoelimishwa”. 2T 488.

B. Utakula nini badala ya nyama?

(a). Kula aina nyingi za vyakula vya mimea kwa kubadilisha milo yake. “Nyama inapokataliwa, weka badala yake aina nyingi za nafaka, kokwa, matunda na mboga, vyakula ambavyo vitakuwa vyenye kuulisha mwili na kuleta hamu ya kula.

(b). Uvipike vizuri ili tumbo lisivichukie. “Lazima kitu fulani kitayarishwe badala ya nyama, na vitu hivi vilivyo badala ya nyama lazima vitayarishwe vizuri, kusudi nyama isitamanike tena”. CD 398.

(c). Maziwa na mayai yanayotokana na wanyama na kuku wenye afya bora na yaliyopikwa au kuchemshwa vizuri yanaweza kutumika badala ya nyama. Hasa kwa wale ambao hawajafikia hatua ya matengenezo ya afya ya kuwa wala mboga halisi (pure vegeterians) (Taz. CD 351, 353, 357, 394).

C. Epuka tabia ya kuzidi kiasi (Extremes)

Kuzidi kiasi katika matengenezo ya afya ni kumzidi Mungu anavyosema katika Biblia na Roho ya Unabii kuhusu suala la nyama na mambo mengine. Au kumzidi Mungu alivyokabili suala la kula nyama baada ya gharika na jangwani. Au kuzidi Roho ya Unabii inavyoshauri kukabili ulaji wa nyama katika hali ya shida na zisizo za shida. Tabia ya kuzidi kiasi inaweza kujionyeha katika makundi ya aina tatu za watu yenye mwelekeo wa mawazo, hisia na matendo kama:-

  1. Kundi moja la wanaozidi kiasi ni wale wagumu katika kutekeleza mawazo yao yanayolemea upande mmoja tu wa matengenezo na kulazimisha wengine wayafuate. (CD uk. 190).

(a). Hufikiri na kufundisha kwamba wote wanaokula nyama wanafanya dhambi, na hivyo hawataingia mbinguni. Mtazamo huu unavuka mpaka kwa sababu zifuatazo:-

(i). Sababu (motive) ya kula nyama au kutokula nyama ndio inaweza imfanye mtu awe au asiwe na hatia mbele za Mungu. Mwanadamu hawezi kujua nia ya moyoni mwa mwenzake. Je, hivyo utajuaje kwamba mimi ninayekula nyama nafanya au sifanyi dhambi? Mungu peke ndiye anajua.

[ii] Tunaokolewa kwa neema kwa njia ya imani katika Kristo, si kwa matendo ya sheria. Gal. 2:16; Efe. 2:8,9. Hivyo kudai kwamba wanaokula nyama wote hawataenda mbinguni ni kama kuwaambia watu waache nyama ili waende mbinguni. Kutokula nyama si pasipoti ya kuingia mbinguni.

[iii]Kazi ya mwanamatengenezo au mwalimu wa matengenezo ni kufundisha, kuongoza, kuonya, kushauri kwa upendo, na siyo kuhukumu tabia ya watu. Mwongozo huu unaelezwa katika Biblia na Roho ya Unabii (Taz. Mat. 7:1-5; War. 14:1-12; Nh. 156-157). Dhamiri za watu zielimishwe a zenyewe zitahukumu matendo yao, kwa njia ya Biblia na Roho ya Unabii.

(b). Huwalazimisha wengine wafuate msimamo wao mwema au mbaya. (CD 198).

Watu ambao dhamiri zao hazijaguswa kuona ubaya wa kula nyama unawatendeaje? Unawazuia wasile nyama wanapoitamani?

(c). Huchukia wanaokula nyama, na kupenda kujitenga nao.

(d). Hufikiri na kufundisha kwamba wote wanapaswa wasile nyama katika hali zote. Mungu kwa njia ya Roho ya Unabii ashauri hivyo.

2. Kundi la pili ni wapinzani wasioishi kufuatana na nuru ambayo Mungu ametua. CD 196, 212.

Hawa hujionyesha kwa mawazo, hisia na matendo kama:-

(a). Hupinga fundisho la ubaya wa kula nyama lisifundishwe. Ellen G. White amesema juu ya kundi hili kuwa “wengine wanasema kwamba baadhi ya ndugu zetu wamesisitiza maswali haya ya matengenezo ya afya kwa nguvu mno. Lakini mtu yeyote hathubutu kuzuia ukweli juu ya somo hili kwa sababu wengine hawakutumia busara katika kusisitiza mawazo yao juu ya matengenezo ya afya?”. CD 212.

(b). Hufikiri na kufundisha kwamba wote wanaokula nyama hawana hatia mbele za Mungu. Wanajuaje? Kama tulivyokwishaona hapo awali ni kwamba sababu ya kula nyama ndiyo inaweza ionyeshe kwamba mtu ana hatia au la. Wapo ambao wanakula kwa sababu ya uchu. Wengine kwa sababu ya haja. Mungu pekee ndiye awezaye kuhukumu sababu ya moyoni.

(c). Miongoni mwa kundi hili ni wale ambao waliacha nyama kwa kufuata mkumbo, na sasa wamerudi nyuma (backslided). Hawakuwa na sababu imara ya kuacha nyama. Hawakuchunguza wenyewe na kuelewa dhahiri kanuni za matenenezo ya afya kuhusu suala la nyama. (Taz. CD 196)

(d). Hufikiri na kufundisha kwamba Tanzania ni nchi ya kimaskini kwa hiyo watu wake wasifundishwe kuacha nyama kwa sababu hawana vyakula vilivyo badala ya nyama. Ni kweli Ellen White anaongelea juu ya watu maskini ambao hawapaswi kufundishwa kuacha nyama (CD 462-

(e). Lakini umaskini unaozungumzwa hapa ni ule ambao nyama ndio chakula rahisi na vyakula vingine ni ghali. Katika hali hii mtu hawezi kuwa na uewzo wa kununua vyakula vya badala ya nyama. Kumnyima nyama ni kumweka katika shida zaidi. Lakini kutumia hali hii ya kimaskini iwape uhuru watanzania wasionywe juu ya ubaya wa nyama ni kupotosha maana ya somo juu ya ulaji wa nyama. Watanzania wengi hawana uwezo wa kununua nyama. Kwa hiyo hawa ndio wangefaa sana kufundishwa kutumia ardhi yao vizuri, wajipatie vyakula vya asili kwa urahisi.

(f). Hufikiri kwamba vyakula vilivyo badala ya nyama havina virutubisho vya kulisha mwili. Ni kweli? Sikiliza, “Ni kosa kudhani kwamba nguvu ya misuli hutegemea juu ya kula nyama.

Mwili unaweza kupatiwa mahitaji yake vizuri zaidi, na kuwa na afya bora bila kutumia nyama. Nafaka, matunda, jamii ya karanga na njugu (kokwa), mboga, vina virutubiso vilivyo muhimu kuifanya damu iwe nzuri. Virutubisho hivi havipatikani vizuri au kamili katika nyama. Kama kula nyama kungelikuwa muhimu kwa afya na nguvu, nyama ingelikuwa miongoni mwa chakula alichopewa mwanadamu, mwanzoni”. MH 316.

(g). Hufikiri na kusema kwamba suala la kula na kutokula nyama ni suala la afya, na ni mashauri tu. Na hivyo hakuna umuhimu sana wa kufuata mashauri hayo na wala hakuna haja ya kufundisha mara kwa mara kwani kutoyafuata au kufuata ni uamuzi wa mtu binafsi. Huongeza kusema kuwa kwa vile ni mashauri ya afya tu kutoyatii hakuwezi kukaathiri maisha ya kiroho. Hoja kama hizi hutolewa na watu wasioelewa lengo la Mungu kutupatia nuru ya matengenezo ya afya. Sababu kubwa ya kuwafundisha watu waache nyama sio kwa sababu tu nyama inaleta magonjwa, bali ni kwa sababu kula nyama kunazidisha ugumu wa kukuza maisha ya kiroho ya kuwa na tabia ya Kristo – kuumbika kamili katika sura ya Mungu.

“Disemba 10, 1972 nalionyeshwa tena kwamba matengenezo ya afya ni sehemu moja ya kazi kuu ambayo itawafanya watu wa Mungu wafae kwa kuja kwa Bwana. Inahusiana sana na ujumbe wa malaika wa tatu kama mkono ulivyo pamoja na mwili”. 3T 161.

“Wahubiri wetu wanapaswa kufundisha matengenezo ya afya, lakini wasilifanye jambo hili kuwa kuu kuchukua mahali pa ujumbe. Mafundisho haya ni baadhi ya yale yaelezayo kazi ya kujitayarisha kukutana na mambo yaletwayo na ujumbe, tunapaswa kuyashika mafundisho haya kwa bidii. 1T 559.

(h). Wengine hutoa hoja kwamba kwa vile Yesu alikula nyama au samaki alipotembelea Ibrahim na alipolisha watu elfu tano hakuna haja ya kuwaambia watu waache nyama kwa sababu Yesu ndiye kielelelzo chetu. Maswali haya yanaweza kusaidia kujibu hoja hii: Yesu ni nani? Roho ya Unabii ni nini? Je, tutahukumiwa Kwa nuru ya wakati huu tuliopewa au na nuru ya wakati wa Nuhu au Ibrahim ambayo hatukupewa? Yesu ni Mungu(Yohana 1:1). Roho ya Unabii ni ushuhuda wa Yesu (Ufu. 19:10).

Roho ya Unabii ni maneno, ni ujumbe, ukweli unaoshuhudia mambo ambayo Yesu anataka tujue na kufanya. Ni ujumbe kutoka kwa Mungu kwenda kwa watu wake kupitia kwa Manabii (Wanadamu) wenye kipawa cha Roho Mtakatifu, na ni kipawa hicho kinawawezesha kunena mamlaka kuwa kama wasemaji wa wajumbe wa Mungu. Tutahukumiwa kwa nuru ya wakati wetu na tuliopewa. Yesu aliishi katika kipindi ambacho nuru yake iliruhusu kula nyama. Hivyo alikula. Kama Yesu angetembea na Waisraeli kutoka jangwani kimwili, unafikiri angekula mana au nyama? Kama Yesu angeishi kimwili katika nuru hii ya matengenezo ya afya, je, asingefuata nuru hii? Bila shaka jawabu ni Hapana; Yesu kama kielelezo angeliishi kwa kufuata Nuru iliyopo ili kuwa kielelezo kwa wote wamwaminio.

3. Kundi la tatu ni wenye mawazo potofu juu ya matengenezo ya afya, CD 196.

(a). Hupika vyakula vilivyo badala ya nyama ovyo ovyo9T161-162.

(b). Hawajali kutafuta vyakula vilivyo badala ya nyama vinavyolisha mwili na mwisho hula vinavyodhoofisha na mara nyingi vya aina moja tu (CD 198 – 199).

(c). Hula chakula kichache sana. Kwa kuzingatia kuwa Huduma ya Kristo alihudumia mwanadamu Kamili; kanisa la waadventista wa sabato kwa kufuata kielelezo chake utume wake unalenga zaidi kuwahudumia wanadamu kumwili, kiakili na kiroho pia. Huduma ya uponyaji sharti ijikite pia katika kuhudumia na kuwajali wagonjwa na wanaoumia kwa magonjwa yawapatayo ikiwepo tatizo hili la utumiaji sugu wa vyakula visivyoujenga Mwili. Kwa kujifunza mafundisho chanya ya kanuni za afya na kuishi kwa kufuata kanuni za Kiroho katika mtindo wa maisha ya kile tulavyo na tunyavyo ndiyo njia pekee na salama ya kulinda afya zetu. Na Neema ya Bwana itamiminika maishani mwetu kutupatia burudiko nafsini mwetu.

MWISHO

  • KULA NYAMA/WANYAMA NAJISI NI DHAMBI BILA KIPENGELE.
  • KULA NYAMA/WANYAMA WALIO SAFI SIO DHAMBI IKIWA TARATIBU ZOTE ZA ULAJI NA KIAFYA ZITAFUATWA KAMA ILIVYOTAJWA JUU/KATIKA MAANDIKO MATAKATIFU.
  • UJUMBE WA MATENGENEZO YA AFYA KUTOKA ROHO YA UNABII HAUPINGANI NA BIBLIA HATA CHEMBE ISIPOKUWA NI TAFSIRI ZA WATU AU KUWA NA UELEWA MDOGO WA KUELEWA UJUMBE HUO, HIVYO =USICHUKULIWE KAMA MASHAURI BALI KAMA NENO LA MUNGU.
  • HAKUNA MSITARI KWA WALA NYAMA NA WASIOKULA NYAMA.
  • KWA NYAKATI TUNAZOISHI HASA KWA NCHI NA MAENEO AMBAPO MBOGA MBOGA ZINAPATIKANA KWA WINGI, NI VEMA KUJIEPUSHA NA ULAJI WA NYAMA YOYOTE KWANI MAGONJWA NI MENGI SANA KWA WANYAMA, AMBAPO KUPITIA ULAJI HUO WA NYAMA TUNABEBA MAGONJWA NA KUYALETA MWILINI MWETU
  • WANYAMA NAJISI SIO WALE TU WALIO NAJISI ASILIA, BALI HATA WALE PIA AMBAO NI SAFI LAKINI WANA KASORO KAMA VILE UGONJWA, NYAMAFU, WAKIWA NA MAFUTA, AU WAKILIWA PAMOJA NA DAMU. KULA WANYAMA KAMA HAO NI KULA NYAMA NAJISI NA NI DHAMBI BILA KIPENGELE.
  • SUALA LA KUACHA KULA NYAMA LISIWE SHURUTI AU KUTISHIA WATU, HUO NI USHUPAVU WA DINI. WATU WAFUNDISHWE ATHARIZA ULAJI WA NYAMA KISHA WACHUKUE UAMZI WAO WENYEWE BILA KULAZIMISHWA.
  • KUJITENGA NA KANISA KWA SABABU YA KULA NYAMA HUO USHIRIKINA WA KIROHO, HAKUNA NURU HAPO ZAIDI YA USHUPAVU NA UMIZIMU WA KIROHO.
  • UNAPOACHA KULA NYAMA HAKIKISHA UNA VYAKULA MBADALA, NA TENA VIPIKWE VIZURI, LA SIVYO UTAKUWA UMETABISHA NAFSI YAKO BURE NA HAKUNA MATENGENEZO YA AFYA UTAKAYOKUWA UMEYAFANYA.
  • MATENGENEZO YA KIAFYA NI PAMBANO LA KIROHO, HIVYO OMBA ROHO MTAKATIFU AKUSAIDIE NA KUKUONGOZA UNAPOFANYA JAMBO LOLOTE. Mungu awabariki sana.

Ninakukaribisha kwa maswali na maoni yako!

Je, unahitaji huduma kutoka James Herbal Clinic? Basi, wasiliana nasi kwa namba hizi: 0768 559 670/0712 181 626,

Arusha-Mbauda,

Karibu sana!