Jinsi Ya Kuandaa Ugali Mzuri Wenye Virutubisho.

Ugali ni chakula kinacholiwa na jamii za kiafrika. Chakula hiki chenye virutubisho vya wanga hutokana na unga wa nafaka (kama mahindimtamauwele) au muhogo.

Unaweza kuandaa ugali wako mzuri utakaokufanya uishi kwa muda mrefu bila kupatwa na magonjwa mara kwa mara kwa kutumia nafaka hizi:

  1. Mtama mweupe kilo 2
  2. Uwele kilo 1
  3. Ngano au muhogo kilo 1

Changanya vitu hivyo vitatu halafu visage pamoja upate unga safi wa ugali.

Pia unaweza kuandaa ugali wako mzuri wenye nguvu kwa kutumia vitu hivi:

  1. Mtama mwekundu kilo 2
  2. Muhongo kilo 1

Changanya vitu hivyo, saga halafu pata unga safi wa ugali mzuri tena wenye afya kabisa.

Jinsi Ya Kuandaa Ugali

Ugali hutayarishwa kwa njia ifuatayo: kwanza unachemsha maji kwenye sufuria, baada ya kuchemka unachanganya unga kidogo na maji ya baridi pembeni, kisha unatia mchanganyiko huo kwenye maji ya moto yaliyo jikoni huku ukikoroga. Utatokea mchanganyiko wa unga na maji ambao unaitwa uji, acha uji huo uchemke kwa muda kisha tia unga kiasi kulingana na uji wako huku ukisonga kwa kutumia mwiko. Endelea kusonga mpaka mchanganyiko ushikamane, mchanganyiko huu ndio hutoa kitu kinaitwa ugali. Hakikisha unasonga ugali huu kwa muda mrefu kidogo maana ni wa mtama na nafaka zingine, unahitaji moto mkali kidogo.

Je, Nini Faida Ya Ugali Wa Mchanganyiko Na Mtama?

Ugali uliochanganyikana na mtama una faida nyingi sana kwa mlaji, nazo ni kama hizi zifuatazo:

  • Huimarisha mifupa
  • Huboresha ubongo
  • Huimarisha kinga ya mwili na hivyo kuzuia magonjwa
  • Hukufanya usizeeke mapema
  • Huboresha macho
  • Huboresha ngozi
  • Hukufanya kuonekana kijana tu
  • Hukupatia nguvu
  • Huzuia magonjwa kama vile kansa, kisukari, presha, nk
  • Huboresha mfumo wa uzazi kwa mwanamke na mwanaume pia
  • Huzuia unene au kitambi
  • Hukufanya kuwa na kumbukumbu nzuri,
  • Huondoa makunyanzi usoni,
  • Hutengeneza umbo la mwili kuwa zuri,
  • Humfanya mama mjamzito kuwa na damu nyingi mwilini na hivyo kuzaa mtoto mwenye nguvu, nk

Je, Ugali Huu Unapaswa Kuliwa Na Mboga Gani?

Ugali huu unafaa kuliwa na mboga za asili japo wengi hupenda kula na dagaa. Lakini kama unataka ufaidi vizuri lishe hii, itumie kwa mboga hizi zifuatazo:

  • Njegere
  • Matembele
  • Mnafu
  • Dengu
  • Majani ya maboga
  • Sukuma wiki
  • Mchicha pori
  • Mchungachunga, nk

463,000+ Woman Cooking Stock Photos, Pictures & Royalty-Free Images -  iStock | Woman cooking in kitchen, Black woman cooking, Asian woman cooking

NUKUU: Unapoandaa mboga hizi usiweke viungo vingi mno, bali weka vitu hivi vifuatavyo:

  • Karanga au tui la nazi
  • Pilipili hoho
  • Kitunguu maji (usikiunguze)
  • Nyanya
  • Bizari mbichi (hasa kwenye njegere au dengu),
  • Karoti

Unapotumia aina ya mboga hizo utapata faida kubwa mno katika mfumo kinga wako wa mwili, damu, na ubongo na pia kwenye mfumo wa uzazi na umeng’enyaji chakula.

Kimaeneo kuna aina mbalimbali za ugali kutegemeana na aina za mazao yanayopatikana.

  • Udaga (muhogo)ni ugali unaopikwa kwa kuchanganywa na ulezi, hupatikana zaidi maeneo ya Musoma kwa Wakulya.

Ugali huweza kuliwa na mboga ya aina yoyote kama nilizozitaja hapo juu, lakini kuna mazoea ya watu kulingana na amaeneo waliyokulia, mfano; kanda ya ziwa wanapenda kula ugali kwa samaki za aina zote. Kule Musoma wanapenda kula ugali kwa nyama hasa za mbuzi au ng’ombe.

Lakini kama unataka kutunza afya ya mwili wako na kujiepusha na magonjwa mbalimbali, basi unaweza kufuata kanuni niliyoeleza hapo mwanzo.

Kawaida ugali huliwa kwa mikono mitupu. Tonge la ugali hufinyangwa kwa mkono kisha kuchovya kwenye mboga uliyoandaa. Ugali, mapishi yake na jinsi unavyoliwa, hufanana kwa kiasi fulani na foufou toka Afrika Magharibi, na polenta toka Italia. Ugali hujulikana kama nshima nchini Zambia au nsima nchini Malawi.

Ugali ni chakula kizuri kinafahamika hata kwenye maandiko ya Biblia, ukisoma katika kitabu cha Hagai 2:12 utaona.

Mungu akubariki sana msomaji, nipende kukaribisha kipindi cha mswali kutoka kwako.

Pia unaweza ukatuma namba ya WHATSAP ili uweze kuunganishwa na darasa letu la masomo ya afya.

Je, unahitaji huduma? Basi tupigie: 0768 559 670/0712 181 626,

Arusha-Mbauda,

Karibu sana.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *