Kwa nini Unapaswa Kutumia Majani ya Mpapai Na Vitunguu?

Mwishoni  mwa makala hii, msomaji ataweza kujua majibu ya maswali yafuatayo:

  • Je, majani ya mpapai yaliyochemshwa yanatibu nini?
  • Je, majani ya mpapai yanafaa kwa ini?
  • Ni wakati gani tunaweza kunywa juisi ya majani ya mpapai kila siku?
  • Je, jani la mpapai huongeza shinikizo la damu?
  • Je, majani ya mpapai yanafaa kwa figo?
  • Je, unywaji wa juisi ya majani ya mpapai una madhara gani?

Papai (pawpaw) ni miongoni mwa mazao yanayolimwa sana duniani. Matunda, mbegu, na majani ya papai hutumiwa sana kutengeneza dawa zenye ufanisi mkubwa.

Jani la mpapai lina baadhi ya virutubisho ambavyo vimeonyesha uwezo fulani wa kifamasia katika masomo ya wanyama. Majani ya papai hutumika kuandaa chai, madawa ya vidonge, na juisi na hutumiwa kutibu magonjwa mengi na huchochea uwezo wa kupona kwa haraka.

Vitunguu pia vina faida nyingi mbali na kusaidia macho. Vinaweza kusaidia ukuaji wa nywele, na kuondoa kikohoi kigumu pamoja na homa. Wakati vitunguu vinapochanganywa  na majani ya mpapai, matokeo yake huwa ni ya kushangaza. Katika makala hii, nitakufundisha  jinsi ya kutumia kwa ufanisi majani ya mpapai pamoja na vitunguu na faida zake utaziona.

Jinsi Ya Kuandaa Majani Ya Mpapai Na Kitunguu Maji.

  1. Pata majani ya mpapai, yaoshe vizuri, kisha yakatekate vipande vidogo.
  2. Menya kitunguu chako, kioshe na pia kikatekate vipande vidogo vidogo.
  3. Chukua halafu changanya pamoja kwenye  blender yako.
  4. Mimina kwenye kikombe au chombo.

MATUMIZI: Kunywa nusu glasi kutwa mara mbili kabla hujala chakula.

 

Faida Za Kiafya Za Kutumia Majani Ya Mpapai Pamoja Na Vitunguu

  1. Hurekebisha kiwango cha sukari mwilini
  2. Husaidia ukuaji wa nywele
  3. Husaidia usagaji chakula tumboni
  4. Husaidia kutibu homa
  5. Huboresha ngozi yako
  6. Huzuia magonjwa ya saratani yasiendelee (kwa wagonjwa wa saratani unapotumia tiba, usisahau kutumia juisi ya mchanganyiko huu)
  7. Hupunguza maumivu wakati wa hedhi
  8.  Hutibu malaria

Rafiki msomaji, nakusihi sana uzidi kujifunza kuwa na maarifa ya kuandaa dawa mwenyewe nyumbani mwako. Kipindi na nyakati tulizo nazo ni mbaya tena zinazidi kutisha mno.

Magonjwa hayatapungua bali yatazidi kuongezeka kwa kasi mno kutokana na mitindo mibaya ya maisha tuliyo nayo. Hivyo, basi “Kila mtu anapaswa awe na maarifa ya msingi ya tiba za asili na namna ya kuzitumia.” E.G.White; Ministry of Healing, p. 127.

Kuna mimea na mizizi myepesi ambayo kila familia inaweza ikaitumia yenyewe na siyo kumwita tabibu…” E.G.White; Letter 17a, 1893.

Rafiki mpendwa, naomba niishie hapa, nikukaribishe tu kwa maswali na maoni yako.

Neno La Faraja: Hata siku ya mwisho, siku ile kubwa ya sikukuu, Yesu akasimama, akapaza sauti yake, akisema, Mtu akiona kiu, na aje kwangu anywe. Aniaminiye mimi, kama vile maandiko yalivyosema, mito ya maji yaliyo hai, itatoka ndani yake. Yohana 7: 37, 38.

Ikiwa kama unahitaji huduma juu ya magonjwa makubwa kama vile uvimbe tumboni, saratani, Kisukari, magonjwa ya moyo, nk, basi wasiliana nasi kwa namba hizi: 0768 559 670/0712 181 626.

Arusha-Mbauda,

Karibu sana!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *