Madhara 3 Mabaya Ya Ugonjwa Wa Pangusa (Chlamydia) Kwa Mwanaume.

Ugonjwa wa pangusa (Chlamydia) kwa kawaida huwa ni maambukizi ya zinaa unaosababishwa na bakteria wadogo sana, ambao kitaalamu huitwa Chlamydia trachomatis. Ni ugonjwa ambao pia umepewa jina la utani, “Maambukizi Ya Kimya kimya” kwakuwa unaweza ukaonyesha dalili kwa mbali au usionyeshe kabisa. Karibia asilimia 25%-50% ya wanaume wanaopatwa na maambukizi ya ugonjwa huu hushindwa kugundulika kwa urahisi kuwa wana maambukizi hayo.

Unaweza ukarejea katika makala yetu ya dalili za pangusa kwa wanawake, utaona pia kuwa nao huhangaika sana kuja kutambua kuwa wana ugonjwa wa pangusa. Mgonjwa anaweza kwenda kufanya vipimo lakini cha ajabu likaonekana tatizo la UTI au fangasi. Atachukua muda mwingi kwenda na kurudi lakini majibu yatakuwa yaleyale, na hatimaye tatizo litaonekana mwishoni kabisa kuwa ni maambukizi ya ugonjwa wa pangusa yakiwa tayari yamemuathiri.

NUKUU: Pia unaweza kubonyeza link hiyo hapo chini ili ujue zaidi kwa upande wa wanawake:

  1. Fahamu Madhara 6 Ya Ugonjwa Wa Pangusa (Chlamydia) Kwa Mwanamke.

Je, Ni Dalili Za Aina Gani Za Ugonjwa Wa Pangusa Zinazompata Mwanaume?

Dalili za maambukizi kwa wanaume huwa ni vigumu kuzitambua. Dalili zinaweza zisiwe za mara kwa mara na hazina utaratibu, ambazo wakati mwingine humpelekea mgonjwa kuamini kuwa sio maambukizi.

Dalili za maambukizi ya pangusa kwa wanaume huwa kama ifuatavyo:

  • Kutokwa uchafu mweupe, au wenye ukijivu au majimaji kwenye uume
  • Kuhisi maumivu, kutojisikia raha au kuhisi kuwaka moto kwenye uume hasa wakati wa kukojoa
  • Uvimbe sehemu za korodani na kuhisi maumivu sehemu hizo

Dalili hizi zinaweza kuonekana ndani ya wiki 1-3. Dalili za ugonjwa wa pangusa kwa mwanaume huwa hazionekani sehemu za uume tu bali zinaweza kuonekana pia kwenye koo, macho na sehemu za njia ya haja kubwa. Inategemea na jinsi maambukizi yalivyoingia.

Dalili zifuatazo za maambukizi ya pangusa zinaweza pia kujitokeza:

  • Maumivu katika njia ya haja kubwa, kutokwa uchafu au damu
  • Matatizo ya macho kutokuona vizuri
  • Koo kuwasha

Je, Nini Kitakachotokea Ikiwa Kama Tatizo Hili Halitatibiwa?

Maambukizi ya pangusa kwa wanaume yanaweza kuharibu mbegu za mwanaume na kusababisha majeraha katika mrija wa uzazi, hali ambayo inaweza kupelekea ugumba wa moja kwa moja.

Wanaume wenye ugonjwa wa pangusa pia hupatwa na matatizo ya miguu kuuma sehemu za jointi, macho kuwasha, mrija wa mkojo kuvimba, nk.

Je, Wanaume Wenye Maambuki Ya Pangusa Wanapataje Vipimo?

Kufanya vipimo mapema bila kuchelewa ni jambo moja la maana sana. Ikiwa kama ulifanya ngono na mpenzi mpya bila kutumia kinga, yaani mtu Yule una mashaka naye kuwa anaweza kuwa na maambukizi, japo ulikuwa hujawahi kufanya vipimo vya magonjwa ya zinaa, basi unapaswa ufanye vipimo bila kuchelewa.

Ieleweke kuwa maambukizi ya ugonjwa wa pangusa huenea zaidi kwa vijana wenye umri wa miaka 16-25.

Je, Nini Vinavyohitajika Kwaajili Ya Vipimo Vya Maambukizi Ya Ugonjwa Wa Pangusa?

Mgonjwa unahitaji kutoa mkojo ili upimwe, unaweza kujizuia kukojoa angalau kwa muda wa masaa 2 ili mkojo unapopimwa uweze kupata majibu sahihi. Ikiwa kama uliwahi kujishirikisha katika mambo ya ngono kinyume na maumbile na unaziona dalili zake, basi unahitaji kupata vipimo sehemu za njia ya haja kubwa au kwenye koo.

Je, Suluhisho Lake Ni Nini?

James Herbal Clinic tuna dawa za asili zenye mchanganyiko wa vyakula na mimea ya asili, nazo zina uwezo mkubwa wa kuondoa ugonjwa huu.

Hivyo, unahitaji huduma wasiliana nasi kwa namba hizi: 0768 559 670/0712 181 626,

Au unaweza kutuma namba yako ya WHATSAP ili tukuunganishe na darasa letu la masomo ya afya.

Arusha-Mbauda,

Karibu sana!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *