Idadi ndogo ya wanawake wajawazito wana uvimbe wa fibroid. Kama ni mjamzito na una vivimbe vya fibroid, haviwezi kusababisha matatizo kwako au kwa mtoto ikiwa kama utapata huduma.
Wakati wa ujauzito, uvimbe wa fibroid unaweza unaweza kuongezeka ukubwa. Ukuaji huu mara nyingi hutokana na mtiririko wad amu kwenye mfuko wa uzazi. Pamoja na mchanganyiko wa mambo mengine kwenye ujauzito, hivyo ukuaji wa uvimbe unaweza kusababisha masumbufu, kuhisi mgandamizo, au maumivu.
Mara nyingi uvimbe wa fibroid huwa haukui wakati wa ujauzito. Katika tafiti mbalimbali, vivimbe vingi vya fibroid hubaki katika ukubwa uleule. Kusinyaa kwa hiari kulipatikana katika takribani asilimia 80% ya wanawake wenye ujauzito wa miezi 6.
Je, Uvimbe Wa Fibroid Unaathiri Vipi Mimba?
Mara nyingi uvimbe wa fibroid huathiri ujauzito. Hata hivyo, unaweza kusababisha madhara kama haya:
- Mimba kuharibika
- Kujifungua mapema
- Kupasuka kwa mji wa mimba na kupelekea kumwagika kwa maji mapema
- Kutokwa na damu nyingi mapema kabla ya kujifungua
- Mtoto kukaa upande tumboni
- Kuharibika kwa mfumo wa mtiririko wa damu na kupelekea kufa kwa seli
Uvimbe wa fibroid wakati mwingine unaweza kuzuia mimba kwa kusababisha ugumba. Na hii hutokana kadiri uvimbe unavyozidi kukua tumboni na kuuathiri mwili.
Uvimbe wa fibroid unaweza kuathiri utungaji wa mimba kwa kuzia mirija ya uzazi, njia ambayo yai hupita kabla mbegu hazijalirutubisha. Kwahiyo yai lililorutubishwa linaweza lisiwe tayari kujipachika kwenye ukuta wat umbo la uzazi ikiwa kama uvimbe wa fibroid uko kwenye njia yake.
Nipende kuishia hapa ndugu msomaji nikaribishe kipindi cha maswali na maoni yako katika makala hii.
Pia unaweza kutuma namba yako ya WHATSAP ili uweze kuungana nasi kwenye darasa letu la afya uweze kupata ushauri na huduma ya afya pia.
Je, unahitaji huduma? Basi unaweza kuwasiliana nasi kupitia namba hii: 0752389252 au 0712181626,
Arusha-Mbauda,
Karibuni sana!