Magonjwa Matatu Yanayomfanya Mwanamke Kutokwa Na Damu Nying Ya Hedhi Kwa Mfululizo.

Kutokwa na damu ya hedhi kwa mfululizo au kujirudia rudia ndani ya mwezi mmoja, kitaalamu hujulikana, “intermenstrual bleeding, metrorrhagia au spotting. Kwa kawaida ugonjwa huu huwa ni wa kawaida na unaweza usiwe wa hatari mno katika afya ya mwanamke.

Wanawake wengi hutokwa na damu ya hedhi kwa kujirudiarudia katika miezi michache ya mwanzo wanapotumia madawa ya uzazi wa mpango. Lakini tukiangalia tunaona kwamba, uvimbe wa fibroid unapoota kwenye tumbo la uzazi huelekea kuwa chanzo kikubwa cha kutokwa na damu ya hedhi kwa muda mrefu.

17,844 Bleed Girl Royalty-Free Images, Stock Photos & Pictures |  Shutterstock

Wanawake wanaokaribia kukoma hedhi wanaweza kupata hedhi ya kujirudiarudia ndani ya mwezi mmoja. Hali hii husababishwa na mabadiriko ya asili ya vichocheo au homoni Pamoja na kuta za tumbo la uzazi kuwa nyembamba.

Walakini inaonekana kwamba kutokwa tokwa na damu ndani ya mwezi mmoja ndio dalili kuu ya magonjwa matatu, nayo ni kama haya yafuatayo:

  1. Mvurugiko Wa Homoni (Hormonal Imbalance)

Kutokwatokwa na damu ya hedhi mara kwa mara au kwa kujirudiarudia kunaweza kuwa ni dalili ya mvurugiko wa homoni. Mzunguko wa hedhi wa mwanamke hurekebishwa na vichocheo au homoni mbili, yaani estrogen na progesterone. Homoni ya estrogen husaidia kudhibiti ukuaji wa kizazi cha mwanamke wakati wa mzunguko wa hedhi. Homoni ya progesterone huandaa tumbo la uzazi kwa ajili ya ujauzito.

Vichocheo (homoni) vyote lazima vifanye kazi Pamoja ili kutengeneza mzunguko usibadirike. Wakati uwiano unapokuwa sio sawa, basi hali ya kutokwa na matone ya damu au hedhi ya mfululizo bila kukoma inaweza kutokea.

Mvurugiko wa hedhi kwa wanawake unaweza kusababisha matatizo makubwa ya kiafya, kuanzia uzito wa mwili kuongezeka, msongo wa mawazo na mashaka. Wanawake wajawazito wenye mvurugiko wa homoni hupatwa na matatizo ya kuharibika kwa mimba. Kutokwa na damu ukeni kwa wanawake wajawazito inaweza kuwa ishara kwamba mimba imeharibika.

2. Maambukizi

Kupata hedhi mara mbili kwa mwezi inaweza kuwa ni dalili ya maambukizi ukeni, hasa maambukizi ya fangasi na maambukizi yatokanayo na uchafu unaotoka ukeni. Maambukizi ya magonjwa ya zinaa kama vile pangusa (chlamydia) na kisonono (gonorrhea) husababisha ugonjwa wa PID. Hali hii husababisha makovu kwenye viungo vya uzazi, maumivu sugu ya tumbo la chini, na inaweza kusababisha ugumba.

Ugonjwa wa kisonono usipotibiwa mapema ukatoweka unaweza kusababisha maambukizi kusambaa kwenye viungo vya mwili wako hasa kwenye viungo vya mifupa na kwenye Ngozi. Ni hali inayotisha. Bonyeza pia hapa: Fahamu Madhara 6 Ya Ugonjwa Wa Pangusa (Chlamydia) Kwa Mwanamke.

3. Saratani Ya Kizazi

Kutokwa na damu ya hedhi kwa kujirudiarudia ndani ya mwezi mmoja inaweza kuwa dalili ya saratani ya kizazi. Saratani ya uke, mlango wa kizazi, tumbo la uzazi Pamoja na vifuko vya mayai vyote huchangia hali ya kutokwa na damu nyingi kwa muda mrefu kama dalili. Hali hizi za saratani mara nyingi huwa hazitoi dalili katika hatua za awali. Dalili za saratani ya kizazi kwa kawaida humaanisha kwamba saratani imeshakuwa kubwa na inapaswa kuanza kutibiwa haraka Zaidi.

Hata hivyo, haiwezi kuwa ni saratani ya kizazi ikiwa kama unatokwa na damu ya hedhi yenye kujirudiarudia ndani ya mwezi mmoja na kukufanya kuwa na mashaka. Wagonjwa wenye saratani ya kizazi mara nyingi hupatwa na dalili nyingi kama vile:

  • Maumivu ukeni wakati wat endo la ndoa
  • Kutokwa na ute mbaya ukeni
  • Tumbo la chini kuvimba
  • Nyonga kuuma
  • Uzito wa mwili kupungua na kuwa mwembambaa

Je, Tiba Yake Inakuwaje?

James Herbal Clinic tunazo dawa nzuri za asili zenye uwezo mkubwa wa kuondoa tatizo hili. Pia unaweza ukaungana nasi kwenye darasa letu la afya kupitia Group La WHATSAPP kwa kutuma namba zako za simu tu.

Unahitaji huduma basi wasiliana nasi kwa namba hizi: 0768 559 670 au 0712181626.

Arusha-Mbauda

Karibuni sana!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *